Dread locks zinavyofanya wadada wazeeke sura

Dread locks zinavyofanya wadada wazeeke sura

Jamani kuna ambao tuna dreads narural kabisa, Nyembamba na safi muda wote.
Halafu kuna hizi mnazoingelea ambazo zinabandikwa saloon ' fake dreadlocks' ambazo zimejaa mtaani wanazibana kichwani kama kata utadhani mtu anaenda kuchota maji. Hizo ndo nyingi hazipendezi.
Lakini pia kwa ambao tuna dreads kabisa tunahitaji usafi sana na maintenance. Maana dread ukiziacha kidogo tu zikachafuka unaonekana kama chizi alotoroka milembe[emoji85][emoji2].
Dreads ni nzuri ila unahitaji kuwa msafi na kuzihudumia na hapo pote ni pesa..uzioshe kila wiki, uzisokote, zikioteana katikati ufanye treaming walau kila mwezi nk. unahitaji pia kuwa na kofia nzuri ya kulalia material zinazofaa . Au ukilala bila kofia uwe tayari kuwa unazigharamia tena kutolewa nyuzi nyuzi zinazoingia kwemye nywele..otherwise ndo ile unaonekana smart kwa mbali halafu mtu akizisogelea dreads anaona zina kama mautango anadhani ni uchafu kumbe ni nyuzi za nguo. Hapo ndo shida inakuja na wengi wanafanya wenye dreads waonekane wachafu..natural dread usiwe bahili ..
Hizo fake dreads aisee zimevamia sana mtaani...na hazipendezi kama natural dreads. Na natural dreads ni safari ya uvumilivu wa hali ya juu sana..natural dreads sio za kila mtu aisee
Fake ndo zimetuharibia ma naturalista[emoji57][emoji1]
 
Aah hapo sawa, me nywele zangu za kujaa halafu tabu kweli kuchana nkabidi niweke locs
Ewaa hizo ndio nnazo zipenda mimi na zinapendeza kuweka rocks [emoji3526],hata natural curl zinanoga mnoo
 
Sana... Ila bado haziwezi kufanana na natural. Ndo maana muda wote wamezifungasha furushi kichwani kama mtu anayehama[emoji2]
[emoji2][emoji2][emoji2]hatarii
 
  • Kicheko
Reactions: Cyn
Kweli dread zinafanya muonekano fulani kama wakiutuuzima ila uwezi amini uo meonakano ndio uzuri wenyewe wa dread locks muonekano huo awe anavaa miwani aisee wananivutia.

Mfano mzuri tuseme Grace Matata ule muonekano wa kizee fulani wa dread ndio uzuri wa dread
 
Back
Top Bottom