Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) linatarajiwa kuanza kupata faida mwaka 2023, kulingana na Mpango wake wa kibiashara wa mwaka 2017/2022. Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema hivi sasa Shirika linajiendesha kwa hasara kutokana na madeni ambayo menejimenti mpya imeyakuta.
Matindi alisema kiwango cha hasara katika Shirika hilo lililoanza kufufuliwa mwishoni mwa mwaka 2016, kimepungua kutoka bilioni 14.2 mwaka huo hadi bilioni 4.3 mwaka 2017.
Hata hivyo, mapato yameongezeka kufikia bilioni 4.5 kwa mwezi mwaka 2017 kutoka milioni 700 mwaka 2016.