Mkuu naomba nifafanulie kidogo kuhusu hii vita ya Turkey na Armenia ni juu ya nini hasa?
RTI
Vita siyo kati ya Uturuki na Armenia bali ni kati ya Azebaijan na Armenia, Uturuki ni mshirika tu.
Kumbuka hizo nchi mbili yaani Armenia na Azabeijan zilisha kuwa chini ya imaya zenye nguvu kubwa duniani kwa nyakati tofauti yaan Ottoman na Usoviet.
Azabeijan na Uturuki ni marafiki wakubwa na wana shea vitu vingi kuanzia lugha,utamaduni ,dini na kinasaba yaan kiufupi ni watu wenye asili moja sema wana tenganishwa na mataifa yao tu ,ila Azebaijan wafuata uslam wa shia wakati Uturuki wakiwa ni suni.
Upande wa Armenia wao ni wakiristo na wanaegemea upande wa Urusi.
Sasa tuje kwenye chanzo cha uhasama kati jamii hizi mbili uhasama wao umeanzia mbali sana kipindi cha Ottoman ,kama nilivyo kueleza hapo mwanzo ni kwamba jamii zote hizi mbili zilishahi kutawaliwa na Ottoman.
Wakati wa vita ya kwanza ya dunia Ottoman ilifanya maangamizi makubwa dhidi ya watu wenye asili ya Armenia ikiwa watuhumu kwa usaliti baada ya kugundua ya kwamba walikuwa wakishirikaana na Urusi kuihujumu Ottoman mpaka kupelekea Ottoman kushwindwa vibaya sana kwenye vita vya dunia.
Zaidi ya Waarmenia million moja na nusu wali uawa na mamilion kukimbia ili kunusuru maisha yao na ndio maana Waarmenia ni jamii iliyo sambaa sana mashariki ya kati ukienda Iran,Syria,Iraq, Afghanistan utawakuta ila hizo nchi siyo asili zao bali walisambaa kwenye hizo nchi wakati wanakimbia maangamizi ya Ottoman.
Kwa hiyo Waarmenia wanawa tizama watu wenye asili ya kituruki kama maadui zao wakubwa kutokana na walicho wahi kufanyiwa na Ottoman .
Sasa tuje kwenye mgogoro unao endelea kwa sasa kumbuka pia hizi nchi zikuwa mojawapo ya majimbo ya ilyo kuwa Usoviet, baada ya Usoviet kuanguka na majimbo yaliyo kuwa chini yake kujitangazia uhuru wao.
Sasa upande wa Azabeijan kuna Jimbo moja lina itwa Nahgorobo karabhak,hili jimbo liko kwenye mipaka ya Azabeijan ila watu wake ni watu wenye asili ya Armenia na ni wakiristo kwahiyo baada ya mataifa hayo kujitangazia Uhuru kitoka Usoviet watu wa hilo jimbo wakawa hawataki kuwa chini ya Azabeijan bali wanataka kuwa chini ya Waarmenia wenzao kitu ambacho Azabeijan iligoma kabisa ,kugoma kwa Azabeijan kulisababisha kulipuka vita mwaka 1990 Armenia ililivamia hilo jimbo kwa kushirikiana wanamgambo wa eneo hilo na kufanikisha kuliteka eneo hilo kutoka kwa Azabeijan.
Azabeijan imesha fanya majiribio kadhaa ya kulikomboa jimbo hilo ila imekuwa ikigonga mwamba.
Hii vita ni kati ya Armenia na Azabeijan ila kila upande unaungwa mkono na mataifa yenye nguvu.
Upande wa Armenia anaugwa mkono na Urusi ,uku Azabeijan ikiungwa mkona na Uturuki.
Ila utofauti wa hii vita na vita ya uko nyuma ni kwamba Uturuki imejiingiza moja kwa moja kwenye hii vita wakati huko nyuma ilikuwa ina tuma silaha tu.
Kwa hiyo vita chanzo chake ni hilo jimbo liitwalo Noghorok karabhak.