Droo ya Kombe la klabu bingwa na Shirikisho Barani Afrika, Simba SC apewa kigogo

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Droo ya mechi za klabu bingwa na shirikishi barani Afrika imekamilika leo huko Misri. wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa ni Dar es Salaam ambao hatua ya awali wamepangiwa na St Louis kutoka visiwa vya sheli sheli, ambapo biola shaka ataweza kufuzu na ikiwa hivyo hatua ya pili ya mtoano anakutana na meshindi kati ya Township Roller (botswana) na El Merreikh (Sudan).

Mechi safi kabisa hii kati ya Mabingwa wa TZ Young Africans na El Merreikh ya SD.



Mtanange mwingine kwenye ni kwenye michuano ya kombe la shirikisho, ambapo Bingwa wa mwaka 2012 wa TZ atacheza na klabu kutoka Djibout iitwayo Gendermerie Tnale.

Bila shaka hapa mtani anapita. Ila kimbembe kipo pale atakapo kutana na mshindi wa mechi kati ya El Masry ya Egypt vs Green Buffalo ya Zambia. Bila shaka Falao hapa atachomoka na kuja kukutana na Simba mechi ya kwanza jijini Dar es salaam.



Mtani hapa ndio kipimo kizuri cha huo uchochoro wako ambao wakina Martin na Mwashiuya waliukosakosa wiki chache zilizopita...
 
Mtani mzee wa Historia atakwambia mwarabu hamsumbui hata kidogo mbali zaidi atakwambia waulize Zamalek na Ismailia kama vile bado kina Pawasa,Kaseja,Shekhan Rashid,Matola wapo

Hahahaha ulijuaje mkuu! ndio jibu lao hilo wakija hapa.....
 
Hahahaha ulijuaje mkuu! ndio jibu lao hilo wakija hapa.....
Akicheza na historia kama google bila kufanya mazoezi sio ajabu wakaingia kwenye historia ya timu iliyowahi kula mikwaju mingi zaidi Afrika.

Ila sio mbaya acha mtani naye apande mwewe walimu wasisahau kuwafundisha jinsi ya upandaji wa ndege wamekaa mnoo bila kupanda mwewe.
 
Matopeni akipita first round atakutana na timu ya Morocco au Senegal inayoitwa Mbouh Petite. Yale yake ya Libolo.
 
Ni wazi sasa kuwa Yanga na Simba wataishia hatua ya pili
 
Ni wazi sasa kuwa Yanga na Simba wataishia hatua ya pili

Ni kweli unachokisema! ila mwenye afadhali ni yule achezaye na El Merreikh kuliko Al Masry>?

Kwa El merreikh ile iliyocheza na Azam hapa ....sijui kama itawapa shida vijana wa Jangwani
 
Ni kweli unachokisema! ila mwenye afadhali ni yule achezaye na El Merreikh kuliko Al Masry>?

Kwa El merreikh ile iliyocheza na Azam hapa ....sijui kama itawapa shida vijana wa Jangwani
Wale jamaa wana mbinu chafu sana.... Yanga ikichomoka itakuwa bahati nasibu... tena tuombe tuanzie kwao
 
Wakitaka kufanya vizuri watume scouts ..mara nyingi tunafungwa hatujui timu pinzani zinavyocheza..wachezaji gani wakali wakuchungwa..tunapewaga suprise
 
Yanga pambaneni na hali zenu. Akilimali ameshasema, haiuzwi wala haikodishwi timu hapa!
 
Yaani waarabu wakae uko wawaogope Mikia ambao hata kwenye ligi wana misimu kibao hawajabeba kombe watakua wehu basi [emoji23][emoji23][emoji23]
Hao hao ambao hawajabeba makombe, Yanga iliandamana mabarabarani kusherehekea kupata nao sare
 
Hao hao ambao hawajabeba makombe, Yanga iliandamana mabarabarani kusherehekea kupata nao sare

Ile Dar Derby kama haujui hata timu moja iwe dhaifu vipi ukipata matokeo unashangilia,ila ni wehu kwa timu ambayo ina misimu 5 mfululizo haijabeba ndoo na hata kushiriki mashindano makubwa eti waarabu waiogope [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…