demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Droo ya mechi za klabu bingwa na shirikishi barani Afrika imekamilika leo huko Misri. wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa ni Dar es Salaam ambao hatua ya awali wamepangiwa na St Louis kutoka visiwa vya sheli sheli, ambapo biola shaka ataweza kufuzu na ikiwa hivyo hatua ya pili ya mtoano anakutana na meshindi kati ya Township Roller (botswana) na El Merreikh (Sudan).
Mechi safi kabisa hii kati ya Mabingwa wa TZ Young Africans na El Merreikh ya SD.
Mtanange mwingine kwenye ni kwenye michuano ya kombe la shirikisho, ambapo Bingwa wa mwaka 2012 wa TZ atacheza na klabu kutoka Djibout iitwayo Gendermerie Tnale.
Bila shaka hapa mtani anapita. Ila kimbembe kipo pale atakapo kutana na mshindi wa mechi kati ya El Masry ya Egypt vs Green Buffalo ya Zambia. Bila shaka Falao hapa atachomoka na kuja kukutana na Simba mechi ya kwanza jijini Dar es salaam.
Mtani hapa ndio kipimo kizuri cha huo uchochoro wako ambao wakina Martin na Mwashiuya waliukosakosa wiki chache zilizopita...