Droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025 | Doha, Qatar | 20.02.2025

Droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025 | Doha, Qatar | 20.02.2025

Hawa waarabu wameshindikana, katika timu 8 kuna Weusi halisia wawili (Orlando na Mamelod) kidogo na Al Hilal, wakati huko shirikisho nako kuna Weusi watatu tu (Simba, Asec na Stellenbosch).


Kwa hali ilivyo, tutaendelea kutawaliwa na Waarabu hadi pale na sisi tutakapoamua kuwekeza seriously kwenye soka kama Waarabu
 
Jioni ya leo pale Mjini Doha nchini Qatar kutafanyika droo ya robo fainali kwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa upande wa michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup) msimu wa 2024/2025 timu zilizofuzu kwa droo hii ni:

  • Simba SC kutoka Tanzania
  • USM Alger kutoka Algeria
  • Zamalek SC kutoka Misri
  • RS Berkane kutoka Morocco
  • Asec Mimosas kutoka CIV
  • Stellenbosch FC kutoka Afrika Kusini
  • CS Constantine kutoka Algeria
  • Al Masry SC kutoka Misri

Wawakilishi pekee kwa Tanzania ni Simba waliopo katika michuano ya Kombe la Shirikisho, ambapo wanaweza kukutana aidha na Stellenbosch ya Afrika Kusini, Asec Mimosas ya Ivory Coast au Al Masry ya Misri.

Katika msimu wa 2024/2025 wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), hatua ya makundi imekamilika, na timu nane zimefuzu kwa hatua ya robo fainali. Timu hizo ni:

  • Al Hilal Omdurman (Sudan) – Kwanza Kundi A
  • MC Alger (Algeria) – Pili Kundi A
  • ASFAR (Morocco) – Kwanza Kundi B
  • Mamelodi Sundowns (SA) – Pili Kundi B
  • Orlando Pirates (Afrika Kusini) – Kwanza Kundi C
  • Al Ahly (Misri) – Pili Kundi C
  • Pyramids FC (Misri) – Kwanza Kundi D
  • Espérance de Tunis (Tunisia) – Pili Kundi D
Mechi za mkondo wa kwanza zinategemewa kupigwa 1-2 mwezi April huku mechi za marudio zikitarajiwa kupigwa kati ya tarehe 8-9 April.

Droo hiyo itaanza majira ya Saa 11:00 Jioni na kurushwa live kupitia Azam Sports 1HD, Supersport, Canal na bila kusahau Caf Tv kule Youtube.

Wana JF wote tutakutana kwenye uzi huu bila kujali timu yako ipo au ilitoka mapemaView attachment 3242267

========================
Ratiba ya Robo Fainal kwa Kombe la ShirikishoView attachment 3242989

Droo ya Ligi ya Mabingwa AfrikaView attachment 3243020
Nikiiangalia miamba iliyopo hapo kwenye Champions League, nawapongeza Yanga kwa kutoka mapema!
 
Simba itajiandaa kwa nguvu zaidi kwa AL MASRY kuliko ingekuwa kwa wale wengine..huenda ikawa advsntages..
Ingawa route za simba huwa zinapita misri kila wakati but no way
 
Halafu nimekuja kushtuka Mwenyekiti wa Vilabu Africa hakuhudhuria tukio muhimu kama hili au alisusa akajificha kwenye kichaka cha harusi?
 
Back
Top Bottom