Jiji la Dar es salaam limeshapita level ya mabasi ya mwendokasi kutokana na idadi ya watu kuwa kubwa hasa pembezoni mwa mji.
Kwa sasa jiji la DSM linahitaji treni ili kuendana na kasi ya kuongezeka kwa idadi ya watu. Walau ruti nne za treni zinahitajika.
1. Gerezani- Tegeta-Bagamoyo
2. Gerezani-Mbezi-Kibaha
3. Gerezani-Mbagala-Kongowe
4. Gerezani-Pugu-Kisarawe
Utafiti wangu mdogo ni kuwa Mwendokasi Mbezi haijapunguza hata kidogo tatizo la usafiri kwa abiria. Watu wanajaa kupita kiasi na foleni ya abiria pale Mbezi kama huna uvumilivu unaweza kuondoka bila kupanda basi. Watu 200 wamesimama kwenye foleni wanasubiri basi ambalo bado halijafika na likifika linachukua watu 80-90 wengine mnaendelea na msoto.
Watu wa mipango jiji la DSM limewazidi akili kila mnachopanga inaonekana kama kimepitwa na wakati. Tuachane na mwendokasi twendeni kwenye treni. Jiji la DSM linakimbia wakati watu wa mipango wanatambaa.
Ahsante!