DStv badilisheni mtangazaji na utangazaji wa Kiswahili kwenye mechi za Kombe la Dunia

DStv badilisheni mtangazaji na utangazaji wa Kiswahili kwenye mechi za Kombe la Dunia

Huyu mtangazaji wenu anapayukapayuka na hata haieleweki anaongea nini. Kila wakati anapaza sauti na kuongea vitu visivyoeleweka wala kuhusiana na mechi iliyopo mubashara.
Mimi nimeamua ni rudi kwenye comentetor wa kiingereza hao waswahili wenzagu siwawezi kelele tupu stori kujifanya ni wachambuzi, mswahili ni mswahili siku zote hata umpeleke ulaya
 
Keep it 222 then..World cup central hapo dstv..hakuna kiswahili..huko kina Peter drury ndo commentetors
Wanafamilia walitamani kuangalia kwa kiswahili ila sasa wengine tunashindwa kuvumilia ule upayukaji usiokuwa na tija wala mwelekeo.
 
Kiukweli hawa watangazaji wa kiswahili wa DSTV wanaboa mnoo.
Mapungufu makubwa niliyoyaona.

1. Mtangazaji anakuwa nyuma ya tukio, sisi tunaona tukio kwanza (goli au kosa kosa) halafu mtangazaji ndio anaibuka kusema kwa makeke wakati tukio limepita kwa nusu sekunde. Hiyo kitu inaboa sana. Nadhani ni kwa sababu watangazaji hawako live uwanjani, wanafuatilia sambamba na sisi tunaoangalia kwa Tv, hivyo sauti zao zitachelewa kidogo.

2. Hawako katika uhalisia kabisa, hususani huu utangazaji wa Maulid Kitenge (umejaa mbwembwe zisizo na maana) au ule kina Kibwana (wa Clouds Fm) ambao umejaa blah blah za kuiga uzungu, afadhali hata ule utangazaji wa option nyingine ya kiswahili (sijui jamaa wa RTD wale) ambao umekaa kiuhalisia kiasi.

Binafsi mpaka sasa watangazaji wa kiswahili wa Azam Tv kwenye ligi ya ujerumani ndio nawaelewa vizuri. Wale jamaa nawaelewa sana.
 
Hii ya kuwa nyuma ya muda wa tukio ndio inaharibu kabisa na kufanya yale matangazo yasiwe na umuhimu wowote.
2. Hawako katika uhalisia kabisa, hususani huu utangazaji wa Maulid Kitenge (umejaa mbwembwe zisizo na maana) au ule kina Kibwana (wa Clouds Fm) ambao umejaa blah blah za kuiga uzungu, afadhali hata ule utangazaji wa option nyingine ya kiswahili (sijui jamaa wa RTD wale) ambao umekaa kiuhalisia kiasi.
Yaani ni fujo na kelele za ajabu na kujiongelesha mambo yasiyokuwa ya kitaaluma. Jamaa anapayuka kama kichaa.
Binafsi mpaka sasa watangazaji wa kiswahili wa Azam Tv kwenye ligi ya ujerumani ndio nawaelewa vizuri. Wale jamaa nawaelewa sana.
Wale angalau ni watangazaji. Hata hawa wa ligi kuu ya NBC Azam wana ahueni sana.
 
Mmejitakia unaanzaje kuwasikiliza waswahili wanaangalia kwenye TV 32"lazima wachemke na hawana uzoefu,hao wasoma vichwa vya habari vya magazeti akina jemedari
 
Kwanin uskilze mpira Kwa lugha ya kiswahili kweli uache kuskia sauti ya peter dury unakazana na lugha ya kiswahili vitu vingine ni upuzi tu
Wapo watanzania wasiojua kiingereza. Huoni muvi za kutafsiri zinavyouzika na kukodiwa sana?
 
Back
Top Bottom