Kiukweli hawa watangazaji wa kiswahili wa DSTV wanaboa mnoo.
Mapungufu makubwa niliyoyaona.
1. Mtangazaji anakuwa nyuma ya tukio, sisi tunaona tukio kwanza (goli au kosa kosa) halafu mtangazaji ndio anaibuka kusema kwa makeke wakati tukio limepita kwa nusu sekunde. Hiyo kitu inaboa sana. Nadhani ni kwa sababu watangazaji hawako live uwanjani, wanafuatilia sambamba na sisi tunaoangalia kwa Tv, hivyo sauti zao zitachelewa kidogo.
2. Hawako katika uhalisia kabisa, hususani huu utangazaji wa Maulid Kitenge (umejaa mbwembwe zisizo na maana) au ule kina Kibwana (wa Clouds Fm) ambao umejaa blah blah za kuiga uzungu, afadhali hata ule utangazaji wa option nyingine ya kiswahili (sijui jamaa wa RTD wale) ambao umekaa kiuhalisia kiasi.
Binafsi mpaka sasa watangazaji wa kiswahili wa Azam Tv kwenye ligi ya ujerumani ndio nawaelewa vizuri. Wale jamaa nawaelewa sana.