barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,378
- 29,739
Mtu Kama una akili timamu unaanzaje kumsikiliza kitenge akitangaza mpira?? Usomaji wake wa magazeti hujakupa onyo??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani nilivosikia wachambuzi wa bongo tu nkapata kichefu chefu.,uswahili mwingi....ndio maana siku zote naangalia tv yenye wazungumzaji wa kiingereza...jamaa wako vizuri...wanatema reality na facts...ukija wa bongo Sasa no fact ,utumbo mtupu...siasa za Simba na Yanga zimeharibu Sana akili za wachambuzi .Huyu mtangazaji wenu anapayukapayuka na hata haieleweki anaongea nini. Kila wakati anapaza sauti na kuongea vitu visivyoeleweka wala kuhusiana na mechi iliyopo mubashara.
HatariBajeti imebana aiseee...zamani walikuwa wanapelekwa South Africa...
Watangazaji walikuwa Radio Tanzania,na External ,idhaa ya nje,Kiukweli hawa watangazaji wa kiswahili wa DSTV wanaboa mnoo.
Mapungufu makubwa niliyoyaona.
1. Mtangazaji anakuwa nyuma ya tukio, sisi tunaona tukio kwanza (goli au kosa kosa) halafu mtangazaji ndio anaibuka kusema kwa makeke wakati tukio limepita kwa nusu sekunde. Hiyo kitu inaboa sana. Nadhani ni kwa sababu watangazaji hawako live uwanjani, wanafuatilia sambamba na sisi tunaoangalia kwa Tv, hivyo sauti zao zitachelewa kidogo.
2. Hawako katika uhalisia kabisa, hususani huu utangazaji wa Maulid Kitenge (umejaa mbwembwe zisizo na maana) au ule kina Kibwana (wa Clouds Fm) ambao umejaa blah blah za kuiga uzungu, afadhali hata ule utangazaji wa option nyingine ya kiswahili (sijui jamaa wa RTD wale) ambao umekaa kiuhalisia kiasi.
Binafsi mpaka sasa watangazaji wa kiswahili wa Azam Tv kwenye ligi ya ujerumani ndio nawaelewa vizuri. Wale jamaa nawaelewa sana.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Huyu mtangazaji wenu anapayukapayuka na hata haieleweki anaongea nini. Kila wakati anapaza sauti na kuongea vitu visivyoeleweka wala kuhusiana na mechi iliyopo mubashara.
Wa TBC1 nafikiri anaboa zaidi[emoji3]Ujaona wa TBC wew, kuna jamaa anajifanya anajua kiarabu,anaropoka hadi sio poa
Keep it 222 then..World cup central hapo dstv..hakuna kiswahili..huko kina Peter drury ndo commentetors
Hawapo live uwanjani kivipi,si nimeskia wapo qatar jamn kila mechi watakua live au[emoji848][emoji848][emoji848]Kiukweli hawa watangazaji wa kiswahili wa DSTV wanaboa mnoo.
Mapungufu makubwa niliyoyaona.
1. Mtangazaji anakuwa nyuma ya tukio, sisi tunaona tukio kwanza (goli au kosa kosa) halafu mtangazaji ndio anaibuka kusema kwa makeke wakati tukio limepita kwa nusu sekunde. Hiyo kitu inaboa sana. Nadhani ni kwa sababu watangazaji hawako live uwanjani, wanafuatilia sambamba na sisi tunaoangalia kwa Tv, hivyo sauti zao zitachelewa kidogo.
2. Hawako katika uhalisia kabisa, hususani huu utangazaji wa Maulid Kitenge (umejaa mbwembwe zisizo na maana) au ule kina Kibwana (wa Clouds Fm) ambao umejaa blah blah za kuiga uzungu, afadhali hata ule utangazaji wa option nyingine ya kiswahili (sijui jamaa wa RTD wale) ambao umekaa kiuhalisia kiasi.
Binafsi mpaka sasa watangazaji wa kiswahili wa Azam Tv kwenye ligi ya ujerumani ndio nawaelewa vizuri. Wale jamaa nawaelewa sana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mimi natune lugha ya kiarabu wanatangaza vizuri sana una enjoy, wakati mwingine natune sheng ama kichina
Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
Huyo gharib Yuko well informed yani,dogo anajianda Sana na mechi anayoenda kuitangaza...Kwa Sasa Kuna Gharib Mzinga wa azam, yule jamaa anajitahidi
Akiwa anatangaza mechi anakua na taarifa za wechezaji wote, sio kama wale WA TBC hawajui hata mchezaji anaeingia sub, shwaini zao
Hawapo live uwanjani kivipi,si nimeskia wapo qatar jamn kila mechi watakua live au[emoji848][emoji848][emoji848]
Yule mwamba wa TBC anaitwa Nazareth nadhani anajua sanaKiukweli hawa watangazaji wa kiswahili wa DSTV wanaboa mnoo.
Mapungufu makubwa niliyoyaona.
1. Mtangazaji anakuwa nyuma ya tukio, sisi tunaona tukio kwanza (goli au kosa kosa) halafu mtangazaji ndio anaibuka kusema kwa makeke wakati tukio limepita kwa nusu sekunde. Hiyo kitu inaboa sana. Nadhani ni kwa sababu watangazaji hawako live uwanjani, wanafuatilia sambamba na sisi tunaoangalia kwa Tv, hivyo sauti zao zitachelewa kidogo.
2. Hawako katika uhalisia kabisa, hususani huu utangazaji wa Maulid Kitenge (umejaa mbwembwe zisizo na maana) au ule kina Kibwana (wa Clouds Fm) ambao umejaa blah blah za kuiga uzungu, afadhali hata ule utangazaji wa option nyingine ya kiswahili (sijui jamaa wa RTD wale) ambao umekaa kiuhalisia kiasi.
Binafsi mpaka sasa watangazaji wa kiswahili wa Azam Tv kwenye ligi ya ujerumani ndio nawaelewa vizuri. Wale jamaa nawaelewa sana.
Atakuwa Juma Nkamia huyo kama siyo Denis MpagazeHuyu mtangazaji wenu anapayukapayuka na hata haieleweki anaongea nini. Kila wakati anapaza sauti na kuongea vitu visivyoeleweka wala kuhusiana na mechi iliyopo mubashara.
Wapo watangazaji wa kiswahili wanaotangaza kwa data na ufundi mkubwa mfano mzuri ni Gharib Mzinga wa Azam tvTatizo la watangazaji wa kiswahili wanafanya kazi kwa mazoea, na sio wataalamu
1. Hawana data!
ukisikiliza matangazo ya wazungu huwa wanatoa data za timu na wachezaji
unaeza pata darasa tosha la mpira
watakuambia rekodi ya timu ya mechi zilizopita
watakupa data za mchezaji mmoja mmoja mfano; idadi ya magoli, club anayocheza, historia yake nk
watakupa uchambuzi juu ya kocha na vikorombwezo vingi vingi vinavokupa burudani
mbongo utasikia tu mbungi inawekwa kati piga moja refuuu kule anapokea namba 23
naona mabaliko namba 10 anatoka anaingia namba 19....utopolo mtupu
hwafanyi research ya timu wanazoenda kutangaza, hata majina ya wachezaji hawayajui wanataja namba
2. Hawana lugha nzuri za kutangaza, zaidi ya kelele za kosakosa na mara chache hukaa kimya bila maneno!
wanajisahau sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Anadhani yuko redioni.Maulidi Kitenge anatangaza kama anatufokea,Totototo Toresiiiii [emoji16][emoji16]
😂😂😂😂 Huyo jamaa kaua.Kuna wa TBC yeye hutaja tu nchi yoyote
Utamsikia "ni free kick kuelekea Portugal.....anapiga kule unababatiza mabeki wa Brazil unakuwa ni kona...anaenda kupiga kona nambari kumi wa Croatia...anapiga kona go go gooo...la la inatoka juu ya lango...ni goal kick kuelekea Poland...wakati huo huo Wachezaji wa Ecuador wanamlalamikia Refa kwamba Kipa aliugusa mpira ule".