Kuna Day nilitembelea Mzungu nmoja Arusha ni Mwanamke wa Kimarekani ila kaolewa na Mmasai, ana watoto wanne, nilishangaa kuto kuona TV sebuleni na vile alivyo na watoto wadogo, ila sikumuuliza.
Siku nyingine nikaenda tena ila siku hio sikuingia ndani niliishia nje kuna kazi nilikuwa nafanya ikabidi nimuulize kwamba Watoto wako hawatazami TV?
Alicho niambia ni kwamba hawezi ruhusu ujinga huo kwa watoto na watoto wanapoteza ile natural cretivity yao na wanajazwa ujinga sana sana wana computa wanacheza games mbalimbali na michezo mingine.
Sasa njoo kwetu Sasa Mtoto anaijua Tamthilia ya Kituruki kuliko kitu chochote kile.
Watoto wanakuwa wajinga lakini wazazi wanaona ni kama ndo malezi Bora ya Watoto.