Dudu baya a.k.a mamba aichana chana clouds fm, amwagia sifa rubby

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
11,660
Reaction score
11,654
Msanii mkongwe na asiyesahaulika katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya dudu baya amekivua nguo kituo cha clouds fm kwa kuwaita ni wanafki wakubwa, wanyonyaji wa wasanii, na wenye kuharibia wasanii ndoto za mziki wao
Mamba alitolea mfano wasanii wanazungushwa mikoani kwenye tamasha la fiesta na kuambulia ujira mdogo, huku akisema pesa wanayopata kwenye hilo tamasha huishia hukohuko mikoani na hurudi dar wakiwa wamepayuka hawana kitu mfukoni

Dudu alisema hayo akipokuwa kwenye kipindi cha usiku cha FRIDAY NIGHT LIVE... FNL kinachorushwa na EATV

Alienda mbali zaidi kwa kumpongeza msanii mwenye kipaji anayekuja juu ruby kwa kusema ametoka kwenye minyororo ya wafu FM akawasihi na wasanii wengine wamuige ruby kwani ameonesha mfano

Akionekana mwenye afya km alivyokuwa zamani, amesema wafu fm hawajapiga nyimbo zangu kwa miaka sita sasa lakini sijatetereka naendelea na maisha yangu kama kawaida

Wakati akiendelea kuwatolea uvivu clouds fm mtangazaji wa kipindi hicho sam misago alitumia mbinu ya ziada kumtoa kwenye kile akichokuwa nacho moyoni
Hata hivyo alipongeza redio ambazo zipo chini ya IPP km East africa radio, radio one, capital fm na kusema hajawahi kuombwa pesa na mtangazaji au dj yeyote wa kituo hicho ili wimbo wake uchezwe hewan
Amevitaka vituo vingine kuiga vyombo vya ipp media

Kwa maneno ya dudu baya ni dhahiri wasanii wengi ni watumwa wa baadhi ya media house
 
kwani aliitwa ili aongelee nini ?
Kwa nini hakusema hayo siku zote ?
Kutumia eatv haonekani ana tafutia ugomvi wa media hizi ?
Dudu lea wajukuu umri unaenda wile anakutegemea usiwe mtu wa hovyo hovyo kama hao wafu fm
watu karibia wote tunajua ni wanyonyaji ila ndio wapo juu
 
Hiki kitu anacho mda mrefu nafkiri na angepewa muda zaidi angewa chana zaidi
 
Kama komando JIDE, hamna kuyumbishwa, inasikitisha wasanii wakubwa wamejazwa ndani ya coaster dar hadi mikoani kisa kuiogopa clouds mwdia.
 
Hawa jamaa kiukweli hawawasaidii wasanii wetu.ya yule bint hamkuyazingatia vinega walishindwa waunga mkono sasa wanatakabharakat za mtu mmoja mmoja
 
Bila kuongelea Clouds Media naona watu hawana pa kupatia kiki

Kama wasanii wangekuwa wanalipwa pesa mbaya si wangeenda kwingine.

Mkubali kuwa Clouds kwa jina.wamejijenga na mengi hata iweje...wakongwe wa mengi nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…