Dudubaya amjibu Mwakyembe, azidi kumshukia Ruge Mutahaba

Nyie si ndio mliolewa na waarabu hapo pwani.. Mkapigwa miti haswa mpk leo mmelegea tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona huko kanda ya usukumani hakukuwa na soko la watumwa badala yake walikuwa wanasombwa kutoka kigoma tabora kilwa huko
Nenda makumbusho uone majina ya akina ngosha walivyowengi. Nenda Bagamoyo uone mazalia ya watumwa waliookolewa na walikotokea.
 
Haha mkuu kwani washirazi ni watu wa wapi au ndo weusi kama yule Karume wa kwenye shilingi 200??
 
Haha mkuu kwani washirazi ni watu wa wapi au ndo weusi kama yule Karume wa kwenye shilingi 200??
Washirazi ni kutoka Ghuba ya Uajemi, kwa neno rahisi ni wale wenye asili ya Iran manake ndio wa kwanza kuingia East Africa enzi hizoooooo!
 
Mbona huko kanda ya usukumani hakukuwa na soko la watumwa badala yake walikuwa wanasombwa kutoka kigoma tabora kilwa huko
Pale Kilwa ni kama ilivyokuwa Bagamoyo na Unguja! Pale hakuna aliyesombwa bali pale akina Ngosha ndo mlikuwa mnapigwa mnada kama viroba vya pamba!!
 

Huzuni bado imetanda kufuatia kifo cha Ruge Mutahaba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Cloud Media Group, aliyezikwa kijijini kwao, Kiziru, nje kidogo ya manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Kwa mara nyingine, msanii aliyekosa staha na utu, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’, ameutumia msiba wa Ruge kutafuta kiki, kama ilivyokuwa kipindi cha ugonjwa wa Ruge.

Wakati Ruge akiwa Afrika Kusini akipigania maisha yake, Dudubaya alileta za kuleta na kuanza kumtuhumu kwa mambo yasiyo na msingi. Yalikuwa ni madai yasiyo na msingi kwa sababu Dudubaya ambaye kwa sasa amechuja kabisa katika mziki, anaamini eti kuanguka kwake katika sanaa, kulisababishwa na Ruge na Clouds Media Group.

Mengi yalizungumzwa, kila mmoja akaamini kwamba kwa sababu Dudubaya ana akili timamu, atakuwa amejifunza kutokana na jinsi watu walivyomshukia kwa kitendo chake hicho.

Waswahili wanasema ukishangaa ya Musa, utayaona ya firauni. Baada ya taarifa za kifo cha Ruge kuanza kutangazwa, huku Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kutoa taarifa zilizowashtua wengi kuhusu kifo cha Ruge, Dudubaya kwa mara nyingine, uso wake ukiwa hauna hata chembe ya haya, alijitokeza na kuzua jipya.

Safari hii, eti alikuwa ‘akishangilia’ kifo cha Ruge kwa kujirekodi huko uchochoroni na baadaye kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, video iliyojaa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya marehemu. Wakati taifa zima likiomboleza kifo cha Ruge, kwa Dudubaya ilikuwa ni sherehe, ‘asiyempenda’ kaondoka kwenye uso wa dunia.

Huenda akili zake ndogo zinazoweza kujaa kwenye kizibo cha soda zinamtuma kuamini kwamba yeye ataishi milele na kwa sababu mbaya wake ameondoka, sasa nyota yake ya muziki itang’aa upya, atarudi kwenye chati kama zamani na kuendelea kutesa milele!

Safari hii upuuzi wake haukuachwa upite hivihivi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe akalitaka jeshi la polisi kumkamata mara moja na kumsweka nyuma ya nondo, jambo ambalo lilifanyika haraka, akawekwa korokoroni katika Kituo cha Polisi Oysterbay. Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), nalo likatangaza kumfutia usajili kutokana na kitendo chake hicho. Kiki yake ya kutaka kumtumia marehemu ikawa imebuma!

Dudubaya ni mfano wa wasanii washamba ambao licha ya kuishi mjini kwa miaka nenda rudi, bado ‘pori’ lipo ndani ya kichwa chake. Ni mbumbumbu wa mitandao ya kijamii, anachoangalia yeye ni kuhakikisha anapata kiki tu, hajali kuhusu athari zake.

Akili yake haina tena uwezo wa kutambua baya na jema, matumizi ya pombe kali kupindukia yamefanya hata ubongo wake kusinyaa na kushindwa kuyaona mambo ambayo hata mtoto mdogo wa darasa la pili anaweza kuyaona.

Amebaki kuwa kituko kwa kila anayemfahamu, na aibu kwa familia yake. Wahenga walisema asiyefunzwa na mamaye, atafunzwa na ulimwengu, huenda kwa sasa Dudubaya anajiona kama ‘malaika’ katikati ya waovu, hayaoni kabisa maovu na kashfa nzitonzito zinazomkabili, huenda akili yake mgando inaamini kwamba ataishi milele, anaamini kwamba anaijua kesho yake.

Mengi yameshazungumzwa kumhusu yeye lakini kwa kuwa anajifanya ni sikio la kufa, tuache muda uzungumze.
 
Pale Kilwa ni kama ilivyokuwa Bagamoyo na Unguja! Pale hakuna aliyesombwa bali pale akina Ngosha ndo mlikuwa mnapigwa mnada kama magunia ya pamba!!
Sasa ndugu yangu mbona mimi hapa nchini ni wa Kuja tu kutokea kisangani zaire iweje nami nijumlishwe na kina king musukuma
 
Alikuwa direct na katika baadhi ya clip anasikika kabisa akimtaja.
kanisa limemtuma katekista.....
USILAZIMISHE WATU KUFANANA MAWAZO,
USA walisheherekea kifo cha OSAMA.....ila kuna sehemu kubwa ya ulimwengu uliumia kwa kifo cha OSAMA

mwache DUDU aishi maisha yake.....wewe ishi ya kwako
 
Darasa la saba la Usukumani Shinyanga anawezaje Kuwa sawa Na Mwenye Shahada Mbili Za Masoko toka Marekani?
 
mtu akifa roho isipokuuma waweza shikiliwa na polisi?


DUDU NGEPOTZEWA ABAKI NA ROHO YAKE YA VISASI ......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…