Podcast ni kama vipindi vya redio, ila tofauti yake ni kwamba:
- Havirushwi live, bali vinarekodiwa.
- Unaweza kusikiliza muda wowote unaotaka kupitia simu au kompyuta.
- Mara nyingi huwa na mada maalum (mfano: michezo, afya, teknolojia, hadithi, dini, n.k.).
- Vinaweza kuwa na sehemu nyingi (episodes), kama vile muendelezo wa vipindi.
Kwa ufupi Podcast = redio ya kidijitali ambayo unasikiliza unapotaka na sehemu unayotaka.
Mfano, Pastor Tonny na Salama Jabir naona Podcast zao zinafanya vema kwa Tanzania.