DUH: HUYU MAGUFULI ATAKUWA FROM HERO TO ZERO

DUH: HUYU MAGUFULI ATAKUWA FROM HERO TO ZERO

kina moha waliandika na kuwasema wote wenye rushwa mbona hawajipigwa izo risasi
Hujafuatilia Jana Maoni ya waandishi huko labda,
Waandishi walitoa Changamoto zao Kenya,
Vitisho ni vikubwa sana,
Kuna vyombo vingine imefikia hatua havipati mgao wa Serikali kwenye Matangazo kisa
Kuripoti Ufisadi unao fanywa Serikalini
 
Wewe wakati huwa unaandika kuhusu Trump kule kwenye jukwaa la kimataifa huwa unataka kuwa Mmarekani. Dunia ni kijiji, kila kiongozi anajadiliwa kwenye majukwaa yote, hutaki basi usiingie JF wala kuomba omba bundle hapo Lumumba street.

Tye tye tye kweli we kituko
 
Lakini Tanzania yetu has more press freedom than Kenya, kwenye ranking za Kidunia Kenya, Uganda &Co. wako chini kabisa na Tanzania yetu inaongoza AM!
Hata rushwa mkuu. Jana South Africa kumetoka ripoti yakwamba Kenyans wanaongoza kwa rushwa sisi hatumo
 
Yeyote anayehusika na tamko hili, NAAMINI KILA SIKU ANALETEWA MAGAZETI YOTE OFISINI BUREEEE, sasa kuna wale wanyonge wenye haki ya kupata habari, ila hawana uwezo wa kununua magazeti. Yan hta hiyo ofa ndogo tu wamenyimwa, kwa sababu naamini hata kwenye redio HUWEZI KUSOMEWA GAZETI LOTE, ni habari chache tu utasomewa. Na hata hvy, hakuna redio iliyokuwa inasoma habari yote, walikuw wanasoma kidogo tu. Nway, tunasubir tamko jingine
 
Wewe wakati huwa unaandika kuhusu Trump kule kwenye jukwaa la kimataifa huwa unataka kuwa Mmarekani. Dunia ni kijiji, kila kiongozi anajadiliwa kwenye majukwaa yote, hutaki basi usiingie JF wala kuomba omba bundle hapo Lumumba street.

WADAU HAMJAELEWA MAADA HII " UKISOMA KILA KITU NANI ATANUNUA MAGAZETI?"... WENYE MAGAZETI WATAUZA NINI?..... WATALIPA KODI VIPI KAMA WATU HAWANUNUI MAGAZETI... HATA HAPA NILIPO MBALI SANA NA NYUMBANI.." UTARATIBU NI UWOUWO...ACHENI KUONGELEA KILA JAMBO KISIASA
 
Published on May 3, 2017
May 3 2017 ni maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari ambapo kitaifa yamefanyika Mwanza na kuhudhuriwa na Wadau pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe.

Marufuku Magazeti kusomwa Redioni na TV Tanzania - Dr. Mwakyembe

Millard Ayo

Hapa sasa ni kama Kenya wakati wa Rais MOI. Nchi itaongozwa na dikteti kupita rais museveni na kagame combined!!!

Kilichokatatazwa ni kusoma habari nzima iliyoandikwa na gazeti redioni au kwenye tv, wanachotakiwa ni kusoma heading au kugusia kidogo tu! Na hili ni kwa nia njema kabisa, tena lina wafavour wenye magazeti na wamekuwa wakilalama mara kwa mara kuwa kitendo cha kusoma habari nzima kwenye redio kunazorotesha biashara maana hakuna atakayenunua habari ambayo ameshaiskia mwanzo mwisho!
 
Pale nyang'au wa Kenya anapodai kujua haya mambo kuliko wamiliki wa magazeti Tanzania.

 
Mnashindwa kujua yakwenu ya Tanzania hamyawezi,
Ripoti ilitoka ya Uhuru wa vyombo vya habari Kenya mpo nafasi ya 90+
Sasa jilinganisheni na Tanzania kisha mje na Upuuzi wenu.
Vipi bosss! inakuwaje leo unachangamkia 'stats' kihivyo. Huwa mnadai ya kuwa wakenya tunashabikia tafiti ambazo nyinyi huwa hamna imani nazo?.
 
As long as he's delivering, hakuna noma. Hero to zero in your country, ngojea uchaguzi 2020 ndio utashangaa hizo zeros zinavogeuka into millions.

....Hahaaaa eti zeros zinageuka into millions....Chezea nguvu ya free Kapelo's, Kanga & Flana....
 
Dah! Inabidi kukaa pembeni na kutazama kwa macho, itachukua muda sana mimi kumwelewa Magufuli anachojaribu kufanya au malengo yake, maana kila uchao anaibuka na jipya, hujui kesho atakuja na lipi. Halafu anathubutu chochote bila breki. Juzi ametangaza kuwafuta wote wenye vyeti feki nikamsifia, leo ameibuka na hili la kuzuia magazeti kusomwa redioni...khaa!

Labda ndani ya miaka mitano tutamwelewa, labda huyu ndiye aina ya rais Afrika inahitaji au ndiye wa kukaa mbali naye. Labda Afrika hatuhitaji uhuru wa maoni, magazeti wala demokrasia za wazungu vitu ambavyo naona Magufuli anaviminya, au labda atakua anafanya makosa makubwa sana. Tusubiri tuone experiments zake hizi kama zitafua dafu.

Akipewa kipaaza sauti na kuanza kutoa hotuba, yeye huzungumza kilicho moyoni, wala harembi au kupaka kwa mgongo wa chupa. Anasema tu liwalo na liwe, juzi kawaambia watu wa Kilimanjaro amewasamehe kwa kupigia kura upinzani, kwanza kule Kagera ndio katema cheche wakati wa janga la tetemeko la ardhi. Halafu keshasema hapangiwi na wala asijaribiwe na mtu....hehehehe!!

Haya Magufuli yetu macho mzee, labda wewe ndiye kiongozi wa kuigwa na utainyanyua Tanzania iwe kwenye level mpya kiuchumi na kimaendeleo kwa kuzuia makelele na maneno mengi ya Waswahili na kuwaburuza kwa pua ili wafanye kazi na kuacha soga au labda wewe ndiye utaipiga chini nchi kwa kutotaka ushauri wala nini.

Nafikiri kinachomfanya Magufuli awe hivi ni kwa sababu ya upinzani. Wapinzani wa Kiafrika hawajui kukosoa kwa nia njema, wao hupinga chochote kwa vyovyote na kwa nguvu zote, hawana lolote njema wala cha kusifia, hapo inabidi rais kujitoa ufahamu na kufanya yake ili atimize malengo yake.
Umehitimisha hoja kijinga sana.
 
Back
Top Bottom