Duh instagram imejaa matangazo ya waganga mara kuiba mume wa mtu, libwata na kurudisha nyota.

Duh instagram imejaa matangazo ya waganga mara kuiba mume wa mtu, libwata na kurudisha nyota.

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Ukitaka kula pesa ya mwa afrika basi uijiingize ktk huduma za kiroho na ukitaka kujua roho chafu za watu basi mnunulie pombe mganga alewe alafu akuambie mambo anayoletewa kuyafanyia kazi.

Ni mapicha unayaona tu mara mbuzi ameuliwa na amechorwa maumbo na alama tofauti.

Alafu chini ya posts zao kunakuwa kuna comments za kujirudia rudia za ushuhuda wa kufanikiwa na huduma zao.

Wengine wanaonganisha intro ya ayo tv na contents zao ili waonekane wako credibe zaidi.

Hali imekuwa ngumu ndugu zangu, angalieni msije kulizwa ndugu zangu.
 
Hayo ndio maisha yenyewe, cha msingi kuwa bize na mishe zako.

Kuna ambao ukiwaandikia tangazo usitupe takataka hapa kwayo ndio kama umewaonesha jalala la kutupa taka
 
Insta ulikuwa mtandao wa kishua lakini kwa sasa wamejaa wapuuzi na matapeli huko. Hakuna mwenye uwezo wa nyota huko ni kudanganya wenye shida na uhitaji ndio hutapeliwa. Mara mvuto wa mapenzi, mara ndagu, mara chama kubwa freemason ni utapeli mtupu
 
Hutaki tujipatie pesa mkuu😥
 
Insta wanakuletea zaidi kile unachofatilia kupitia ads zao jaribu kureport kuwa hauko interested na hio ads haitakaa uwone Tena🙏
 
Targeted ads. Wanakuletea kila unachopenda kukifuatilia. Kama unakutana na hayo matangazo basi ni wazi wamejihakikishia kuwa wewe ni mdau wao. Ukiya-report au kusema kwamba hauko interested nayo hutayaona tena!
 
Algorithm hizo kuna vipendwa unafuatilia , mimi binafsi nikiingia lazima nikute page ya kuuza nguo , ujenzi au furnitures maana ndio madili yangu .
 
Back
Top Bottom