Ukitaka kula pesa ya mwa afrika basi uijiingize ktk huduma za kiroho na ukitaka kujua roho chafu za watu basi mnunulie pombe mganga alewe alafu akuambie mambo anayoletewa kuyafanyia kazi.
Ni mapicha unayaona tu mara mbuzi ameuliwa na amechorwa maumbo na alama tofauti.
Alafu chini ya posts zao kunakuwa kuna comments za kujirudia rudia za ushuhuda wa kufanikiwa na huduma zao.
Wengine wanaonganisha intro ya ayo tv na contents zao ili waonekane wako credibe zaidi.
Hali imekuwa ngumu ndugu zangu, angalieni msije kulizwa ndugu zangu.
Insta ulikuwa mtandao wa kishua lakini kwa sasa wamejaa wapuuzi na matapeli huko. Hakuna mwenye uwezo wa nyota huko ni kudanganya wenye shida na uhitaji ndio hutapeliwa. Mara mvuto wa mapenzi, mara ndagu, mara chama kubwa freemason ni utapeli mtupu
Targeted ads. Wanakuletea kila unachopenda kukifuatilia. Kama unakutana na hayo matangazo basi ni wazi wamejihakikishia kuwa wewe ni mdau wao. Ukiya-report au kusema kwamba hauko interested nayo hutayaona tena!