Mbona mabeberu hao hao ambao wana lengo la kuchafua nchi, wametoa ripoti inayoitaja Tanzania kuongoza katika kupiga vita rushwa na matumizi mazuri ya pesa za serikali katika Africa nzima?.
Mkuu vipi wale maaskofu na mapandre waliotoa ule waraka kuhusu hali ya demokrasia nchini, baadhi yao wakatishiwa kufutiwa uraia wao, hawa nao pia wamepewa pesa na mabeberu, au hawaipendi Tanzania?.
Kule Rwanda, mtu yeyote mwenye kusema mambo yanayomsema Kagame, anapewa jina la "Genocide sympathizer", au anashirikiana na waasi kuiangusha serikali ya Kagame, tabia hiyo ndio inayomfanya Kagame kugombana na dunia nzima, je unataka Tanzania kuiga mwelekeo huo?, kwamba kila mwenye mawazo tofauti basi haipendi Tanzania au anatumiwa?