Dulla anapokea kipigo cha mbwa koko huko

Kwa taarifa yako viazi ni wanga mzuri sana na vinautia nguvu mwili
Sio vya kukaanga ,vya kuchemsha ni sawa kabisa,ila kibongobongo asilimia kubwa vinakaangwa na ndio sio vizuri kwa hilo ulisemalo
 
Cheki Twaha Kiduku anavyosikitika mwamba anavyodhalilika.
 

Attachments

  • VID-20211010-WA0004.mp4
    3.2 MB
Cheki Twaha Kiduku anavyosikitika mwamba anavyodhalilika.
Hata yeye Twaha Kiduku ana kaa kwa huyo bondia wa Kongo.
Twaha ana vingumi vyepesi sana na hajawahi kumdondosha dulla mbabe katika mapambano yake yote.
Kama anabisha amwite Katompa aje achapwe na yeye.
Tshimanga ana viwango vya kimataifa.
Na sio vya akina Mwakinyo.
 
Hata yeye Twaha Kiduku ana kaa kwa huyo bondia wa Kongo.
Twaha ana vingumi vyepesi sana na hajawahi kumdondosha dulla mbabe katika mapambano yake yote.
Kama anabisha amwite Katompa aje achapwe na yeye.
Ngumi hazipo hivyo,unaweza kushangaa akadondoshwa kiulaini tu huyo Katompa na Kiduku,naamini mapromota watamleta tena amchalenji kiduku,uzuri wa kiduku hakupi nafasi sana ya kumshambulia,shida ya dullah hana uwezo wa kujilinda kabisa,anaruhusu sana kupigwa,we fikiria ile mara ya pili alivyoangushwa yeye ndio alimbananisha huyo mkongo kwenye kamba lakini mkongo akachoropoka akamgonga ngumi iliyomwangusha mbabe,ana mapungufu mengi sana huyo mzaramo
 
Mijitu ya bara naona hilo neno la afile munu asigale munu mmelishikilia na kuliona labda lugha ya ajabu duniani,,, wakati nyie wenyewe milugha yenu mkiongea ka mzizi wa jiwe, aliyepigwa abdallah lkn naona lugha ndo inajadiliwa, acheni shobo
Hombo dikwela munyu [emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji28][emoji28]

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Halafu hawa Majaji hovyo kabisa zile point wamempa Abdalah Pazi za nini kuna mmoja katoa 94 kwa 93. Yaani hata kwenye ngumi kuna akina Mahela wa NEC.
Hapo nimeshangaa sana kudondoshwa kote bado wanyama point dulla
 
Dula amuige mwakinyo, atafute wastaafu huko aje ajipigie akijidai kuendelea kuleta walio kazini atafia uwanjani shauri yake
Mwakinyo janja sana anapigana na wanyanyua vyuma ambani mikono imepinda hawawezi kuachia jebu
 
Halafu hakuna na maandalizi wamemstukiza
 
Watanzania wote macomedian ,comment ya kwanza hadi mwisho ni full kichekesho.
Huyo sijui dula makabila akipitia hizo comment anatundika daluga siku hiyo hiyo

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Jamaa kachoka haswaaa,Sasa atulie tu tatizo hataki kutunza mwili wake ndiyo shida,na Sasa hivi tunamsubiria kwenye mapambano ya utangulizi tu Mana haya ya kukatana shoka hayawezi,Yani tutampa mapambano ya utangulizi apambane na kina Halima vunja Bei mana anatuchosha tu...
 
Game ya jana nilitaka kumwona cosmas cheka tu, huyu dulla nilijua atapigwa tu hamna kitu pale
 
Hapo nimeshangaa sana kudondoshwa kote bado wanyama point dulla
Yaani mtangazaji alipokuwa anasoma zile pointi mimi nilibaki mdomo wazi. Yaani Dula kupigwa kote kule na mkongo kuanzia raundi ya kwanza mpaka ya mwisho lakini eti jaji mmojwapo akakosa aibu kabisa akasema wamepishana point moja. Hawa majaji wawe "serious" aisee vinginevyo watauharibu mchezo wa ngumi kwani kwa sasa hapa Tanzania nadhani ngumi ndio mchezo unaofuatiliwa na watu wengi ukiacha mpira wa miguu. Mwanzoni majaji walikuwa na hii tabia ya kuwapendelea wabongo lakini baada ya kelele nyingi za wadau walijirekebisha. Lakini kwa mwelekeo wa jana naona kama vile wanataka kurudisha tabia hii mbovu.

Kwa Dula Mbabe nadhani sasa ni wakati wake wa kustaafu na kuachana na ngumi vinginevyo atakuja kufia ulingoni. Ni wakati wake sasa aende akacheze mieleka. Mchezo wa ngumi unahitaji vitu vingi sana kuachana na miguvu tu aliyonayo Dula Mbabe. Ngumi zinahiji nidhamu ya hali ya juu sana wakati wa kujilinda na kushambulia, wepesi, mazoezi magumu, pumzi, uwezo mkubwa wa kumsoma adui yako nje na ndani ya ulingo, uwezo wa kubadilika kwa haraka wakati mpambano unaendelea na baba wa vyote kipaji ambavyo vyote hivi Dula Mbabe hana kabisa. Yaani huyo Dula Mbabe anategemea tu ukutane tu bahati mbaya na gumi lake moja uzimie basi zaidi ya hapo hajui amepanda ulingoni kufanya nini kwani hata aina yake ya upiganaji haivutii kuangalia mapambano yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…