Dullah Planet(EARADIO/EATV) weka wazi WCB wamekukosea nini?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi.
Bila shaka hakuna ubishi kabisa moja ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha muziki na tasnia ya muziki wa kizazi kipya hatuwezi kivisahau vyombo kama EATV na EARADIO na wala si vya kubezwa...

Pamoja na hivi vyombo kuwa na matatizo na wasanii ambayo kimsingi yanaweza kutokea kwakuwa wanaofanya kazi wote ni binadamu na hawajakamilika kabisa.....lakini tusisahau kuwa vyombo hivi vingi au karibu vyote vina sifa ya kupenda kuabudiwa lakini mara zote matatizo yao na wasanii humalizwa kwa kuongea hasa kwa hawa EARADIO/EATV.

Ni wazi kabisa EARADIO/EATV ndio lilikuwa kimbilio la wasanii wengi maana walijiweka mbali sana na migogoro na wasanii na kwakweli kipindi cha nyuma walijizolea umaarufu mkubwa sana kwa sababu ya utaratibu mzuri wa kutatua migogoro yao na wasanii.......

Hivi karibuni EATV/EARADIO wamekuwa wakilalamikiwa sana tena sana kuwa hawachezi nyimbo za Diamond na wamekwenda mbele zaidi hawachezi nyimbo zote za WCB.... katika ya watu waliokuwa wana watetea hawa EARADIO/EATV mimi nilikuwa mmoja wao kwani niliamini hawana kosa lolotea na wanayo hoja na kuna kipindi walikuwa wanapinga nyimbo za WCB.

Lakini baada ya kufanya utafiti nimejiridhisha kabisa EARADIO/EATV ni chombo kilicho jaa wanafiki waliotukuka kwa sababu pamoja na kuwa na chuki na msanii fulani hawataki kuweka wazi kama wenzao clouds ambao ni wazi kuwa kila mtu anajua kuna wasanii hawapatani nao...

Kibaya zaidi EATV/EARADIO sasa wamekuwa wakiongozwa na fikra na chuki za Abdallah Hamisi Ambua ambaye yeye na kundi lake pale EATV/EA RADIO huokoteza vihabari kwenye mitandao ambavyo vina lengo la kumchonganisha Diamond na watu

Na wao huvifanya topic ili Diamond na wale wanaomzunguka waonekane wabaya na pamoja na watu wa karibu wa Diamond kujaribu kutatua migogoro hiyo lakini Dullah yeye huwa ndio kama mmiliki wa vituo hivyo....

Kwa sasa hawachezi nyimbo za WCB kabisa na hii ni kutokana na chuki za Dullah kwa Diamond...

Dullah anatakiwa kujua kuwa kwa sasa vyombo vya habari ni vingi hata wasipo cheza nyimbo za Diamond na WCB bado zita hit kwani ni ukweli ulio wazi EA RADIO kwa sasa haina nguvu kuzidi Clouds fm na E-fm pamoja ina frequency mbili....na uongozi wa Earadio na EATV wasipo angalia Dullah na timu yake watawaharibia biashara kwaajili ya chuki zao binafsi...

Dullah anatakiwa kujua kuwa hata yeye alipo hapo alisaidiwa sana tena kupitia Salama Jabir anatakiwa kujua kama yeye alisaidiwa atumie nafasi yake kusaidia wengine.

Kama ni hoja ya kutoshiriki tunzo zao wanatakiwa kutwambia kama ni WCB peke yao ndio hawakushiriki au lah...lakini bado si hoja ya kumchukia msanii wakati tunzo ilikuwa si lazima au wajitazame upya....

Naamini EATV/EARADIO wanaweza tafuta njia nzuri ya kutatua matatizo yao na wasanii hawa kwa njia nzuri tuu na sio kwa chuki hizi za wazi wazi kwani hazimsaidii yeyote yule na wote wana chakupoteza kwenye hili....Hakuna watu wanaofurahia migogoro bali wengi wanapenda amani.

Wasalaam
 
Huyo Dullah anaelalamikiwa ni mtangazaji wa kawaida tu. Je yeye ndo ana mamlaka ya kuchagua nyimbo gani zipigwe na zipi zisipigwe? Je yeye ndo anatangaza vipindi vyote? Mimi nadhani lawama zinapelekwa kwa mtu ambae hausiki maana sisi tunawajua watangazaji tu lakini kuna other staff members ambao wao ndo wanafanya decisions.

Otherwise labda useme kama Dullah ana cheo kingine hapo apart from utangazaji.
 
Ukifanya utafiti kama mimi utagundua kuwa Dullah pamoja kuwa ni mtangazaji wa kawaida lakini anao ushawishi mkubwa pale Earadio
 

pia tujiulize, Je WCB wameshawahi kulalamika kuwa nyimbo zao hazichezwi EATV and Radio??
 
Sasa kama awachezi nyimbo za WCB na umeishasema hata wasipozicheza kuna vituo kibao vya Redio vinacheza nyimbo za WCB sasa hapa unalalamika nini msiwapangie watu mziki wa kupiga kwenye vituo vyao vya Redio Mbona Magufuri alisema tusimpagie na wenyewe East Africa Radio msiwapangie
 
Hili la EATV/RADIO kutokucheza nyimbo za WCB sikuwa nalitambua au tuseme sikuwahi kulifikiria.. Itabdi nifanye kautafiti kasiko rasmi..
Safi sana mkuu. Kwa mtu msomi huwa hachangii hoja pasi kujiridhisha kama hoja ni ya kweli au laa. Wewe utakuwa ni msomi wa kweli
 
Hata mimi namshangaa mtoa mada maana anasema dullah hapigi nyimbo za wcd kwenye kipindi cha planet bongo sasa sijafaham kama vipindi vingine wanapiga nyimbo za wcd
 
Hata mimi namshangaa mtoa mada maana anasema dullah hapigi nyimbo za wcd kwenye kipindi cha planet bongo sasa sijafaham kama vipindi vingine wanapiga nyimbo za wcd
Hawapigi kabisa
 
Hili la EATV/RADIO kutokucheza nyimbo za WCB sikuwa nalitambua au tuseme sikuwahi kulifikiria.. Itabdi nifanye kautafiti kasiko rasmi..
fanya utafiti hata mimi nilikuwa napinga nalo na nilikuwa na watetea sana hapa jamvini lakini nimejiridhisha kabisa hawapigi nyimbo za WCB hasa Diamond
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…