Dullah Planet(EARADIO/EATV) weka wazi WCB wamekukosea nini?

Dullah Planet(EARADIO/EATV) weka wazi WCB wamekukosea nini?

acha ujinga dula sio dj na kwanza dj hajipangii playlist

We kwa nn usiwaulize hao wasafi kwa nn nyimbo zao hazichezwi kabla ya kuja ku blame radio nzima na tv nzima myb wcb watakua na jibu?

kama una nia njema na wasanii kwa nn usianze na jide na rubi ambao nyimbo zao Zina miaka hazichezwi na kituo B?

punguza unafki wewe
iv mtu unaanzaje ku blame kitu uschokijua hapo m ndo nachokaga na ushabiki mandazi
af umen'gan'gana na dula as if yeye ndio mtangazaji pekee kwe radio
some tyms naeza nkaamini wasafi wanawalipa mchafue watu
anyway so what?
 
bro sikubaliani nawewe diamond hakushiriki tuzo za Eatv coz alikua Na contract Na voda Na ni balozi WA voda kiutaratibu hakupaswa yeye wala timu yake ya Wasafi kiashiriki Ni utaratibu WA kawaida huo.NI Kama coca wakiwa Na bahati nasib zao wanakuambia kabisa wafanyakazi Na familia zao hawapaswi kushiriki,hii Ni kwa uelewa wangu mdogo.Bifu laweza kua Na sabanu nyingi ambazo sisi watazamaji hatuzifaham.
tuzzo zilkua znaitwaje?
wavoendaga mtv wanakua na contract ya makampuni wadhamini wa huko?
Ujinga na kuto jitambua tuu sjaona maali tuzo znaitwa Coca-Cola au vodacom!!!! Tuzo zinaitwa eatv awards
 
Yaan kila MTU anatumia jina LA mond kuweka vibifu ujinga,wanapoteza mda WCB upige nyimbo usipige utajua mwenyewe na kwa diamond utampiga tu maake yupo kwenye matangazo km cocacola sasa ukijidai unachuki na mond lazima ujampe,ukifikq nyumbn kwako watt wako wanacheza ngororo,mama anaimba Salome,aunt ana Chibu perfume,wadogo zako wanakula diamond karanga
 
Wasalaam wana jamvi.
Bila shaka hakuna ubishi kabisa moja ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha muziki na tasnia ya muziki wa kizazi kipya hatuwezi kivisahau vyombo kama EATV na EARADIO na wala si vya kubezwa...

Pamoja na hivi vyombo kuwa na matatizo na wasanii ambayo kimsingi yanaweza kutokea kwakuwa wanaofanya kazi wote ni binadamu na hawajakamilika kabisa.....lakini tusisahau kuwa vyombo hivi vingi au karibu vyote vina sifa ya kupenda kuabudiwa lakini mara zote matatizo yao na wasanii humalizwa kwa kuongea hasa kwa hawa EARADIO/EATV.

Ni wazi kabisa EARADIO/EATV ndio lilikuwa kimbilio la wasanii wengi maana walijiweka mbali sana na migogoro na wasanii na kwakweli kipindi cha nyuma walijizolea umaarufu mkubwa sana kwa sababu ya utaratibu mzuri wa kutatua migogoro yao na wasanii.......
Hivi karibuni EATV/EARADIO wamekuwa wakilalamikiwa sana tena sana kuwa hawachezi nyimbo za Diamond na wamekwenda mbele zaidi hawachezi nyimbo zote za WCB.... katika ya watu waliokuwa wana watetea hawa EARADIO/EATV mimi nilikuwa mmoja wao kwani niliamini hawana kosa lolotea na wanayo hoja na kuna kipindi walikuwa wanapinga nyimbo za WCB.
Lakini baada ya kufanya utafiti nimejiridhisha kabisa EARADIO/EATV ni chombo kilicho jaa wanafiki waliotukuka kwa sababu pamoja na kuwa na chuki na msanii fulani hawataki kuweka wazi kama wenzao clouds ambao ni wazi kuwa kila mtu anajua kuna wasanii hawapatani nao...

Kibaya zaidi EATV/EARADIO sasa wamekuwa wakiongozwa na fikra na chuki za Abdallah Hamisi Ambua ambaye yeye na kundi lake pale EATV/EARADIO huokoteza vihabari kwenye mitandao ambavyo vinalengo la kumchonganisha Diamond na watu na wao huvifanya topic ili Diamond na wale wanaomzunguka waonekane wabaya na pamoja na watu wa karibu wa Diamond kujaribu kutatua migogoro hiyo lakini Dullah yeye huwa ndio kama mmiliki wa vituo hivyo....
Kwa sasa hawachezi nyimbo za WCB kabisa na hii ni kutokana na chuki za Dullah kwa Diamond...

Dullah anatakiwa kujua kuwa kwa sasa vyombo vya habari ni vingi hata wasipo cheza nyimbo za Diamond na WCB bado zita hit kwani ni ukweli ulio wazi EARADIO kwa sasa haina nguvu kuzidi Clouds fm na E-fm pamoja ina frequency mbili....na uongozi wa Earadio na EATV wasipo angalia Dullah na timu yake watawaharibia biashara kwaajili ya chuki zao binafsi...
Dullah anatakiwa kujua kuwa hata yeye alipo hapo alisaidiwa sana tena kupitia Salama Jabir anatakiwa kujua kama yeye alisaidiwa atumie nafasi yake kusaidia wengine.

Kama ni hoja ya kutoshiriki tunzo zao wanatakiwa kutwambia kama ni WCB peke yao ndio hawakushiriki au lah...lakini bado si hoja ya kumchukia msanii wakati tunzo ilikuwa si lazima au wajitazame upya....

Naamini EATV/EARADIO wanaweza tafuta njia nzuri ya kutatua matatizo yao na wasanii hawa kwa njia nzuri tuu na sio kwa chuki hizi za wazi wazi kwani hazimsaidii yeyote yule na wote wana chakupoteza kwenye hili....Hakuna watu wanaofurahia migogoro bali wengi wanapenda amani.

Wasalaam
Maelezo meengi kama umetumwa, jambo la msingi kama wamedharauliana kwe masuala ya mpunga ili awapawambe je? Najua mleta mada unatumika kama toilet paper tu wakipatana huna dili wakishindwana unadili mmbea.
 
Ushasema kuna tv na radio stations nyingi na umeenda mbali kwa kutuaminisha kua EATV na EA Radio kwa sasa hawana nguvu kama E-fm sasa kwa nini unalalama unataka wapige ngoma za WCB wakati hawana nguvu ingekua Majogoo fm ya Njombe au Mashujaa fm ya Lindi mngelalama ivi,inawezekana hata unaemtetea na yeye aliropoka kama wewe kua hawana nguvu ya kumpandisha au kumshusha mnatakiwa muwe na adabu na media house zote maana wasanii wanavimba ila wakivimbiwa mbio kujiliza na kutafuta huruma naona hadi Wambua anawatoa kamasi.
Msingi wa ubora wa msanii unaanzia home ukisema wewe unawaza Mtv,Soundcity na BET na unataka uwapangie watu aya ndio matokeo yake najua mashabiki wa kweli wa Diamond wanajua nini kipo nyuma ya balaa hili wote wamekosea nyambafu zao.
 
Kwan kushiriki izo tunzo ilikuwa lazima maana kwanza zilikuwa za kujipendekeza.,..au ww maana ya neno kujipendekeza hulijui mkuu

Kushiriki haikua lazima,na wao kupiga nyimbo za WCB sio lazima pia mbona mnawapangia wakati WCB hawakutaka kupangiwa acheni double standard basi.
 
wapige wasipige diamond bado mkubwa kuliko EATV.
Unamaanisha Diamond mkubwa kuliko Mengi? Mengi anauwezo wa kumfanya Diamond houseboy wake na akamlipa pesa ndefu kuliko anayopata kwenye mziki
 
Huyo Domo nyimbo zake zilikuwa hazipigwi hapo kitambo lakini bado anatisha.. Hao wasanii wanaochezwa nyimbo zao huko wamefika wapi kimafanikio ya kimuziki? (harmorapa, baraka da prince n.k)

Ukweli utabaki palepale, kituo chenye nguvu ni clouds pekee maana wale watu msaada wao hauishii kwenye kupiga nyimbo pekee hadi shows, na deals mbalimbali (Mf. Perfume za Chibu limepigwa collable Kusaga na Domo, Usiku wa kuamkia leo Domo kapiga show Rwanda huko iliyoandaliwa na Clouds)

Hao walalanjaa Eatv ni kama kitumbua kikikosekana unakula sambusa ila Clouds ni Chumvi na ndio alikojishkiza huyo Domo, hajatetereka na hawezi kutetereka kisa Eatv..
 
Huyo Domo nyimbo zake zilikuwa hazipigwi hapo kitambo lakini bado anatisha.. Hao wasanii wanaochezwa nyimbo zao huko wamefika wapi kimafanikio ya kimuziki? (harmorapa, baraka da prince n.k)

Ukweli utabaki palepale, kituo chenye nguvu ni clouds pekee maana wale watu msaada wao hauishii kwenye kupiga nyimbo pekee hadi shows, na deals mbalimbali (Mf. Perfume za Chibu limepigwa collable Kusaga na Domo, Usiku wa kuamkia leo Domo kapiga show Rwanda huko iliyoandaliwa na Clouds)

Hao walalanjaa Eatv ni kama kitumbua kikikosekana unakula sambusa ila Clouds ni Chumvi na ndio alikojishkiza huyo Domo, hajatetereka na hawezi kutetereka kisa Eatv..

Na ndivyo Management ya Mondi inavyofikiria namna hii. Wrong!

Pamoja na ukweli kuwa Clouds inaushawishi zaidi, ila ni busara kwa msanii kuheshimu vyombo vyote vya habari hata kama vingine ni vichanga namna gani, sembuse EATV/RADIO!

Haohao Clouds, wanaweza kumgeuka jamaa na akakosa pa kukimbilia. Unakumbuka fiesta ya mwaka jana walimchunia kimtindo kupiga nyimbo zake kwa sababu alikataa kushiriki shughuli zao? Wanaweza kumfanya mtumwa vilevile, wakamlazimisha akubali matakwa yao wakijua kuwa hawezi kukataa kwani hana mawasiliano mazuri na vituo vingine.

Kama ni mjanja, atafute suluhu sasa. Maandiko matakatifu yanasema "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote,,,," na "Ajidhaniaye kuwa amesimama na aangalie asianguke,,,"
 
Msiwalaumu sana hao dabiliusibii na huyo Abdallah wote ni watoto wanakua
 
Eatv/radio ni vyombo vikubwa na vikongwe sana hapa nyumban, mond inabid atumie busara kutatua matatizo aliyonayo na hiyo media sabab yeye hatawika miaka yote, ila eatv itaendelea kuwepo, 2kumbuke hapo nyuma kulikua na wasanii wakubwa 2 mr. Nice, ferouz, mb dogy, matonya ......nk na nyimbo zao zilikua zinapigwasaa hapo, ila saiv wako wap? Inabid ajue kua kuna kusiz akiwa vizur na media kubwa kama hiyo watafanya kumrespect miaka ijayo kama ilivyo kua juz kwenye heshima ya bongo fleva, wasanii kama dudubaya, juma nature, zanton.... Nk walipaform
 
Unakumbuka fiesta ya mwaka jana walimchunia kimtindo kupiga nyimbo zake kwa sababu alikataa kushiriki shughuli zao?
Sababu ya kutoshiriki Fiesta ilikuwa kampuni ya Tigo ndio ilikuwa inadhamini show na yeye ana mkataba na Voda.

Kwa kifupi hapa TZ hawezi kuhudhuria shughuli yeyote kama imeandaliwa na kampuni ya simu tofauti na Voda.
 
Back
Top Bottom