Dullah Planet(EARADIO/EATV) weka wazi WCB wamekukosea nini?

Dullah Planet(EARADIO/EATV) weka wazi WCB wamekukosea nini?

Iyo ndo ilichochea zaid mkuu..sabb eatv walitaka kumaliza ubishi au.kushindanisha zile tuzo kati ally kiba na diamond pia wasafi walitoa maneno sio mazur kwa.uongozi wa eatv ple.walipoombwa kushiriki uchukuaji form
Maneno gani hayo?
Mbona kabla ya hizo tuzo diamond na rayvanny waliitwa FNL na walisifia kuhusu hizo tuzo na wakawa wanawasisitiza wasanii wakachukue form.
 
Hapa sasa ndyo nimeelewa vzur sana,nakumbuka tuzo hzo niliziangalia nikiwa chuo na 'Salama J' ndye aliyekuwa mc,kiukweli Wcb walipaswa kuona kuwa wamekosea na kuuomba uongoz was eatv/ea- radio msamaha ili maisha yaendelee
Walikosea nini? Basi wasingesema wasanii wajipendekeze wangewashindanisha tu.
Sasa walisema wajipendekeze mtu hajipendekezi unakasirika ukizingatia moja ya kanuni yao ilikuwa kwamba msanii awe kajisajili basata, ila wasafi itakuwa wengi hawajajisali si uliona juzi basata walisema hawakumuandalia rayvanny mapokezi kwakuwa hajajisajiri kwao.
Na siyo wcb peke yao ambao hawakuchukua tuzo unless labda zile tuzo ziliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwashindanisha wcb labda na watu wengine otherwise sioni sababu ya wao kununa
 
inaweza kuwa au si kweli ila ile tuzo ya van unapewa nje ya ukumbi yani hata kwenye live perfomance ya watu wa tuzo ile bet hawajawaweka it means bet wao ile ni tuzo isiyo na mashiko
Lakini kuishinda hiyo tuzo ya nje ya ukumbi ukitokea east africa kwa wenzako huku kwa mtogore siyo mchezo...
Hata akina wizykid bado wanashindania hizo hizo tuzo za nje ya ukumbi japo wamepiga collabo na akina drake, chrisbrown et el
 
Siku ya birthday ya dullah alichagua wimbo wa diamond wakaupiga, pia kumbukeni huyo diamond mwenyewe alishasema hategemei nguvu ya vyombo vya habari unategemea watampa airtime hata mimi siwezi, pia kupigwa kwa wimbo kunategemeana na djs, producer wa kipindi na idara ya muziki kama DJ Kim na wengine sidhani kama ni haki kumlaumu dullah
Tatizo watu mna miss-interprete alichokisema diamond.
Mnazunguka tu ukweli ni kuwa hawapigi nyimbo zake sababu halisi wao kama EATV hawajasema ni nini...
Lakini siyo mara ya kwanza waliwahi kuwa na tatizo na diamond mwaka jana nadhani wakayamaliza hadi akafanyiwa exclusive ya planet bongo kipindo kizima alihojiwa diamond tu na host alikiwa bell 9, bado diamond na rayvanny wakafanyiwa mahojiano FNL kipindi hicho ndipo walikuwa wameanza toa form za tuzo.
Diamond kwenye FNL akaulizwa kuhusu tuzo akasifia na akasisitiza wasanii wachukue form na akasifia utaratibu wa kujipendekeza ila wao baada ua hapo hawakuchukua hizo form.
Sasa kama sababu ndiyo hiyo basi EATV wanazingua waondoe kipengere cha kujipendekeze wawe wanawapendekeza wao maana huwezi nipa uhuru wa kujipendekeza halafu nisipochukua form unune.
 
Huyo Dullah anaelalamikiwa ni mtangazaji wa kawaida tu. Je yeye ndo ana mamlaka ya kuchagua nyimbo gani zipigwe na zipi zisipigwe? Je yeye ndo anatangaza vipindi vyote? Mimi nadhani lawama zinapelekwa kwa mtu ambae hausiki maana sisi tunawajua watangazaji tu lakini kuna other staff members ambao wao ndo wanafanya decisions.

Otherwise labda useme kama Dullah ana cheo kingine hapo apart from utangazaji.
Wabongo ni mabingwa wa Umbea na Uchonganishi.....
 
Someni hiki na muelewe...

Eatv walianzisha Tuzo za Watu .. Neno lao lilikuwa Jipendekeze.. (Maana ake jipendelee wewe maana wao wakichagua itaonekana wamepanga) wasanii wengi walijitokeza kwenda kuchukua form wakajipendejeza kwenye vipengele walivoona vinafaa.. Hao wauza karanga wakajiona wao watabembelezwa .. Walipigiwa simu mara nyingi tu kwa ajili ya uwepo wao.. Mameneja nao wakajifanya ni mameneja pesa .. Mwisho wake tuzo zikafika wao hawakuchukua form ikaonekana wana dharau kile kinachoanzishwa kwa ajili ya wasanii sababu wao wanajiita intaneshino.. Wakapigwa Ban izo ni taratibu tu za chombo cha habari ukijifanya wewe mjuaji wao wanajua sana.. Dula hasilaumiwe yuko kazini..

Ova
Ni wasanii tu wa wcb ambao hawakujipendekeza kwny izo tunzo...
Mbona darasa hakujipendekeza na wasanii kibao tu mbona hawakushiriki au kulikuwa na maada nje ya pazia tofauti na kujipendekeza kwny tunzo zao.....ebu tufafanulie zaidi
 
Iyo ndo ilichochea zaid mkuu..sabb eatv walitaka kumaliza ubishi au.kushindanisha zile tuzo kati ally kiba na diamond pia wasafi walitoa maneno sio mazur kwa.uongozi wa eatv ple.walipoombwa kushiriki uchukuaji form
Kwan kushiriki izo tunzo ilikuwa lazima maana kwanza zilikuwa za kujipendekeza.,..au ww maana ya neno kujipendekeza hulijui mkuu
 
Mimi najua ile ngoma ya WATAISOMA NAMBA EEEH haipigwi na media zote Tanzania zaidi ya kwenye mikutano, na wenye ngoma yao wala hawalalamiki!
 
Tunajua kwnn clouds hawakupiga nyimbo kwa kipind hicho chote.. lkn hatujua kwann eatv na radio yake hawpigi nyimbo za diamond na wcb.. upo?
Hawapigi kwasababu diamond aliwaambia yeye ni mkubwa kuliko hiyo media, na wcb huwa hawapeleki nyimbo zao huko.....upo?
 
Hili suala mm pia linaniboa sana . naichukia EATv na radio kwasasa. Hata siwafuatilii tena
 
Hili povu lote lnamuangukia
Dullah au
 
Hili suala mm pia linaniboa sana . naichukia EATv na radio kwasasa. Hata siwafuatilii tena
Maisha yako yako hatarn
Kuvunjika kawaambie
Hao mafala wcb wakutibu
 
afuu kunaa yulee jamaaa Graysongedion jamaaa mnafikii sanaa anaonesha chuki za waziii waziii kabisaaaa kwa Mond na maneno yake ya a taarabu. ..
 
Someni hiki na muelewe...

Eatv walianzisha Tuzo za Watu .. Neno lao lilikuwa Jipendekeze.. (Maana ake jipendelee wewe maana wao wakichagua itaonekana wamepanga) wasanii wengi walijitokeza kwenda kuchukua form wakajipendejeza kwenye vipengele walivoona vinafaa.. Hao wauza karanga wakajiona wao watabembelezwa .. Walipigiwa simu mara nyingi tu kwa ajili ya uwepo wao.. Mameneja nao wakajifanya ni mameneja pesa .. Mwisho wake tuzo zikafika wao hawakuchukua form ikaonekana wana dharau kile kinachoanzishwa kwa ajili ya wasanii sababu wao wanajiita intaneshino.. Wakapigwa Ban izo ni taratibu tu za chombo cha habari ukijifanya wewe mjuaji wao wanajua sana.. Dula hasilaumiwe yuko kazini..

Ova
Eatv kuanzisha tuzo za hiari na Mtu kutoshiriki hapo dhambi iwapi?

WCB wana haki ya kuchagua cha kufanya na EATV/RADIO wana haki ya kuwaadhibu wanavyoona inafaa...na sidhani kama hilo ni tatizo kuuubwa, na ndo maana WCB sijawasikika kulalamika...ndio kwanza leo mimi nasoma hapa sasa hivi.

Nadhani tatizo ni hapo Mleta uzi alipoandika 'huokoteza vihabari vya mitandaoni ambavyo vina lengo la kumchonganisha Diamond na Watu, na wao kuvifanya topic'.

Sasa je hii nayo ni sehemu ya taratibu za chombo hicho cha habari? na je huwa wanazisema pia zile nzuri kuhusu hao WCB?

Tofauti iliyopo kati ya Clouds na Jide...sijawahi kuwasikia clouds wakimuongelea Jide kwa lolote linalojitokeza mitandaoni liwe baya au zuri.

So point hapa ni EATV/RADIO wapotezee tu, waachane mazima na habari za WCB na kila kitu kitakuwa sawa.

Na kuhusu 'Wauza karanga' mama...hata Bakhresa mulimuita sana 'Muuza ice cream' leo hii bila yeye Zanzibar mngeeenda na zile Panton za Ferry.
 
inaweza kuwa au si kweli ila ile tuzo ya van unapewa nje ya ukumbi yani hata kwenye live perfomance ya watu wa tuzo ile bet hawajawaweka it means bet wao ile ni tuzo isiyo na mashiko
Eti bana, unapewa tuzo ya nje ya ukumbi unaviiimba...wakati kuna Wasanii kibao bongo wana Matuzo ya ukumbini, Wasanii kama.............kama................, hebu nikumbushe majina ya waliowahi kupata tuzo za ndani BET nimalizie komenti yangu.
 
Wasalaam wana jamvi.
Bila shaka hakuna ubishi kabisa moja ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha muziki na tasnia ya muziki wa kizazi kipya hatuwezi kivisahau vyombo kama EATV na EARADIO na wala si vya kubezwa...

Pamoja na hivi vyombo kuwa na matatizo na wasanii ambayo kimsingi yanaweza kutokea kwakuwa wanaofanya kazi wote ni binadamu na hawajakamilika kabisa.....lakini tusisahau kuwa vyombo hivi vingi au karibu vyote vina sifa ya kupenda kuabudiwa lakini mara zote matatizo yao na wasanii humalizwa kwa kuongea hasa kwa hawa EARADIO/EATV.

Ni wazi kabisa EARADIO/EATV ndio lilikuwa kimbilio la wasanii wengi maana walijiweka mbali sana na migogoro na wasanii na kwakweli kipindi cha nyuma walijizolea umaarufu mkubwa sana kwa sababu ya utaratibu mzuri wa kutatua migogoro yao na wasanii.......
Hivi karibuni EATV/EARADIO wamekuwa wakilalamikiwa sana tena sana kuwa hawachezi nyimbo za Diamond na wamekwenda mbele zaidi hawachezi nyimbo zote za WCB.... katika ya watu waliokuwa wana watetea hawa EARADIO/EATV mimi nilikuwa mmoja wao kwani niliamini hawana kosa lolotea na wanayo hoja na kuna kipindi walikuwa wanapinga nyimbo za WCB.
Lakini baada ya kufanya utafiti nimejiridhisha kabisa EARADIO/EATV ni chombo kilicho jaa wanafiki waliotukuka kwa sababu pamoja na kuwa na chuki na msanii fulani hawataki kuweka wazi kama wenzao clouds ambao ni wazi kuwa kila mtu anajua kuna wasanii hawapatani nao...

Kibaya zaidi EATV/EARADIO sasa wamekuwa wakiongozwa na fikra na chuki za Abdallah Hamisi Ambua ambaye yeye na kundi lake pale EATV/EARADIO huokoteza vihabari kwenye mitandao ambavyo vinalengo la kumchonganisha Diamond na watu na wao huvifanya topic ili Diamond na wale wanaomzunguka waonekane wabaya na pamoja na watu wa karibu wa Diamond kujaribu kutatua migogoro hiyo lakini Dullah yeye huwa ndio kama mmiliki wa vituo hivyo....
Kwa sasa hawachezi nyimbo za WCB kabisa na hii ni kutokana na chuki za Dullah kwa Diamond...

Dullah anatakiwa kujua kuwa kwa sasa vyombo vya habari ni vingi hata wasipo cheza nyimbo za Diamond na WCB bado zita hit kwani ni ukweli ulio wazi EARADIO kwa sasa haina nguvu kuzidi Clouds fm na E-fm pamoja ina frequency mbili....na uongozi wa Earadio na EATV wasipo angalia Dullah na timu yake watawaharibia biashara kwaajili ya chuki zao binafsi...
Dullah anatakiwa kujua kuwa hata yeye alipo hapo alisaidiwa sana tena kupitia Salama Jabir anatakiwa kujua kama yeye alisaidiwa atumie nafasi yake kusaidia wengine.

Kama ni hoja ya kutoshiriki tunzo zao wanatakiwa kutwambia kama ni WCB peke yao ndio hawakushiriki au lah...lakini bado si hoja ya kumchukia msanii wakati tunzo ilikuwa si lazima au wajitazame upya....

Naamini EATV/EARADIO wanaweza tafuta njia nzuri ya kutatua matatizo yao na wasanii hawa kwa njia nzuri tuu na sio kwa chuki hizi za wazi wazi kwani hazimsaidii yeyote yule na wote wana chakupoteza kwenye hili....Hakuna watu wanaofurahia migogoro bali wengi wanapenda amani.

Wasalaam
bado hujabainisha dulla Planet kafanya nn au ndio ufisiemu umekukaa kichwani ??
 
Walikosea nini? Basi wasingesema wasanii wajipendekeze wangewashindanisha tu.
Sasa walisema wajipendekeze mtu hajipendekezi unakasirika ukizingatia moja ya kanuni yao ilikuwa kwamba msanii awe kajisajili basata, ila wasafi itakuwa wengi hawajajisali si uliona juzi basata walisema hawakumuandalia rayvanny mapokezi kwakuwa hajajisajiri kwao.
Na siyo wcb peke yao ambao hawakuchukua tuzo unless labda zile tuzo ziliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwashindanisha wcb labda na watu wengine otherwise sioni sababu ya wao kununa
Mi nashangaa walikosea nini ikiwa NI WENGI TUU hawakushiriki?
 
Back
Top Bottom