Dully Sykes ana mchango mkubwa wa Harmonize kujitoa Wasafi

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
10,805
Reaction score
14,181
Kimsingi Dullysykes ni nyoka mbaya sana kucheza naye ,ni mtu ambaye amesurvive mwanzo kwa ubora wa kazi zake kama julieta ,nyambizi na hi,baada ya hapo akajua kucheza na nyakati.

Alianza na chokochoko na TID ambapo alikuwa kinara by then mashabiki wa TID hawakuwa na time nae ila haters wa TID walitengeneza yeye kama ngao hajapata imba nyimbo kali kama zeze ,nyota yako,etc hili nalolikapita .

Ikaja zama ya Mr nice na dudu baya kama kawaida yake akaside na dudubaya maana hakuweza kutoboa kwa mr nice sangoma zilikutana.

Zikaja zama za Mr blue na Joseline ,Jamaa aligundua macho yote yako kwa hawa wawili basi alipambana mpaka ikafanyika colabo ''dhahabu'' yeye akanufaika kurudi ila joseline nasikia anauza kibanda cha chipsi uswahilini.

Sasa mastermind wa survival akajaribu kushine enzi za ufalme huu wa diamond na king kiba akatengeneza ileile mbinu ya colabo safari hii hakutoboa inasemekana mondi aligundua mkakati akafuta verse ya alikiba na huo ndo ulikuwa mwanzo wa bifu maana hata dully akagoma kutoa huo wimbo ,ila hapo mondi alikuwa anazikwa hai maana nyota yake iilikuwa anauziwa jamaa.

Mnyama huyu mkali alipoona hajatoboa na option pekee ni kuwa karibu na wasafi akaanza mbinu za kujisogeza kwa harmonise mara ooh mdogo wangu sijui atafika mbali ,mara anaheshima ,dogo akajaa misifa balaa taratibu akafanikiwa kupata collabo ambazo hata yeye anakiri dogo kampa kampani ,za ufytele jamaa ni moja ya wanaompa kichwa dogo kuwa anaweza na ananyonywa
muda hujibu,hesabu hazikosei .

Mondi ukisema afanye kolabo na alikiba anaekataa ni alikiba maana anawashauri wazuri wanamwambia utapotea mazima ,furahia hii siasa ya nani zaidi bila mashindano,hata mange aliposikia tetesi alikiba amealikwa wasafi festival pamoja na kuigiza kinafiki kuwa ali yuko juu ya mondi kwa mara ya kwanza ali act the truth alimwambia ukithubutu umeliwa .

Mondi pia katili sana alijua kinachompa kiki dogo harmo ni ushauri na influence yake asee kampotezea kila support overnight page ya mondi ikitolewa nyimbo ya harmoniser alikuwa anaipost balaa kumbuka ana followers almost 7 mil ,rayvan 3 mil ,mboso 2.3 mil,ravalava 1.5 hawa wote wameusiwa wamteme ,nampa moyo akiimba vizuri ataheat ila akileta huuupuuzi wa kujifanya anainua wakina qchief na dullysykes hata kaa aamini wenzake wako busy na kukuwa sio kushukuru shukuru watu amabao hata hawajakusaidia .

wenu mtiifu

The only
 
Umeandika kikubwa sana uko vyema
 
Harmonise ashapotea

Tumsahau huyu jamaa

Kiki yake ya mwisho itakua uchaguzi wa mwakani na hiki kinyimbo chake uchwara kinachomsifu dikitesa

After that itakua kama toilet paper imetumika then over

Anyway ngoja apambane na ujinga wake
 
Harmonise ashapotea

Tumsahau huyu jamaa

Kiki yake ya mwisho itakua uchaguzi wa mwakani na hiki kinyimbo chake uchwara kinachomsifu dikitesa

After that itakua kama toilet paper imetumika then over

Anyway ngoja apambane na ujinga wake
Hhahahaha mziki wake unauzika kwa vijana ,mimi ukinikutanisha na magu ntampamba hadi atafurahi ,ila siwezi fungua bar niseme azindue ,ukiwa mnafiki kuwa na mipaka na mjanja ,dogo hajui wenzie huwa wanafanya kwa uchaguzi tuu ingia akaunt za ondi ,alikiba hukuti siasa wanajitenga na negativity
 
hapo kwa duly no comment mana sioni na sijui how anahusika na hayo, ila namuhurumia harmonize am sure tena very sure haya ya sijui kualikwa na viongozi wa siasa wanapata hadi lunch sijui kuwaimbia sijui leo yako na nani mwenye jina mjini yana muda mfupi sana tena sana, soon the reality will kick in hapo sasa haaapo sasa, mmh tupo hapa, i wish him well kiukweli sitaki kumuhukumu kwasababu siyajui yaliyopo behind the curtain but am sure hakukurupuka kujitoa kwa mtu ambae alimshika mkono when he was totally nothing hata pa kulala tu hakuwa napo diamond kamchukua kaishi nae madale baada ya hapo dai aliponunua ile nyumba kunduchi akamuhamishia kule akaishi mwenyewe kama kwake halipi hata 100, so nataka kuamini haikuwa rahisi kwake kutoka wcb ila may be kuna yasiyobebeka nyuma ya pazia ambayo ameona heri lawama kuliko fedhea
 
Haka kajamaa bhana

Anyway ngoja nisiongee sana muda utaongea

Subirini
 
kaka hivi leo chris brown akimwambia diamond tupige collabo mapato asilimia 95 ya chris unadhani atakataa ,atawaza watz next after hiyo diamond hajawahi kuwa hata na viewers mil 70 tangu aanze mziki chris brown hata akipost anaimba bafuni viewers hawapungui mil mia ,sisemi kuondoka kubaya ila hakuwa matured enough ,kumbuka dogo anajenga villa kwao ,anamjengo kunduchi uza madale tatu huununui na haujaisha ,amenunulia mama na babake gari mbili second hand mil 60 cash hivi mpaka uwanunulie wazazi milion 60 magari kawapa rafiki zake magari ya milion 7-10 si chini ya watatu ina maana dogo kifedha hawezi pungua bil 2+ ,unadhani anakipaji kuliko mr blue? rich mavoko ? anamuweza ben paul? waza aliwazidia nini sasa kimeondoka
 
yani hata sijakuelewa, alafu mimi sio kaka, uko upande wa diamond au harmonize?
 
Swala muda msije baadaye mkaanza kutafuta wachawi ,uzuri jamii forum ipo hapa siku zote,siku muda ukifika tutakukumbusha ulichokiandika ktk thread yako.
 
Swala muda msije baadaye mkaanza kutafuta wachawi ,uzuri jamii forum ipo hapa siku zote,siku muda ukifika tutakukumbusha ulichokiandika ktk thread yako.
WATCH AND LEARN
 
Sioni cha ku learn,ila muda ukigika tutakukumbusha yote uliyo andika,uzuri JF hawafuti thread.
WATCH (TIZAMA KILA HATUA ZAKE TANGU SASA) LEARN (JIFUNZE ,HAIMAANISHI MIMI NTAKUWA SAHIHI ILA UTAJIFUNZA AFTER WATCHNG ),NO HARD FEELINGS BUDDY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…