Dumu la mafuta ya kupikia lita 20 ni 82000 na cement ni 24000, hakuna wa kuongea tena!

Hakuna aliyelaumu zaidi ya majungu yenu,wavivu ndiyo mnalalamika watu wanapiga kazi hawana muda wa kuloloma ati.

Maisha yamewashinda na bado aisee mtakimbia wote nchi kenge nyie
Dah😁😁 mm sisiemu lakini cha moto nakiona huyu jamaa atafaa tena kweli?
 
Punguza kodi
 
Hakuna mchezo niserikalli kuweka tozo nyingi huku Gharama za uzalishaji zikiwa juu.hakuna mfanyabiashara anaetaka kufanya kazi ya hasara.
Karibu na meli ya cement inafika au imeshafika
 
Mkulima kujikomboa kutoka unyonyaji wa watu wa mjini! Hii ni dhihaka; mjini ndiko kuna soko kubwa la mazao ya mkulima, kama mtu wa mjini hana hela, hataweza kununua kwa bei ya juu mazao ya mkulima, Mwishowe maumivu yote yanarudi kwa mkulima, maana mkulima hana uwezo wa kukaa na mazao yake kwa muda mrefu Kumbuka suala la centre - periphery relationship (kama unalijua)
 
Makusanyo ya kodi yamefikia trilion 2!
 
Mtu anapandisha bei za bidhaa muhimu (basic needs) kwa sababu anataka kuongeza pato la serikali. Wajinga wanadanganywa kwamba meli inaleta mzigo. Ilianza sukari, cement na sasa ni mafuta.
 
Mpaka tusubiri meli kweli?
Tulia hivyo hivyo mzigo ukishashushwa kutoka kwenye meli mtakula mema ya nchi. Serikali haiwaachi wananchi mupate shida inashugulikia kelele ndio zinakera. Wewe mtu ukiamuka kelele eti mafuta leo bei hii , kesho hivyo hivyo unafikiri ndio yatashuka ukiposti mitandaoni ?
 
Hapo mjini Kawe, jana jamaa yangu mtaani kaenda akakuta yana 84000 yakamshinda akaacha kununua.
Wapi huko jamani? Mbeya sasa lita 6000! Ina maana hiyo ni lita 20 ni 120000!
 
Mfumuko wa bei ni mkubwa, kutafuta unashushwa na kushuka bei kea vyakula hasa mahindi na mchele. Huku mikoani korie na aina zake ni sh 98000 kwa lita 20, sabuni ctn ndogo ya miche 10 imetoka sh 8000 miezi 2 iliopita, sasa ni 10,000. Kifupi gharama ya maisha imepanda sana.
 
Mh Rais anapitia wakati mgumu sana kuna watu hawapend kweli apeleke maendeleo hakika binadam wana roho mbaya.
Apeleke maendeleo wapi? Upendeleo ktk kusambaza maendeleo nchini umeshika kasi ktk awamu hii. Nyerere Amekufa bila uwanja wa ndege wa maana Musoma. Hospitali ya Kwangwa sina uhakika kama imesha kamilika.
 
Waovu tu mnasherekea kutangaza mabaya. changamoto zinazojitokezea ni kawaida, sio kwamba serikali haioni na imelala, inashughulikia meli ya mafuta inakuja na bei itarejea kikawaida.
Mkuu iyo meli mbona haifiki? Ngano nayo kwa sasa imefikia 1500 kwa kilo kutoka 1200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…