Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Ukiangalia historia ya maisha ya watu wengine waliotangulia utabaini kwamba maisha ya mwanaume siku zote huwa magumu sana.Mwanaume anaweza kuonewa huruma nyakati nne ,moja akiwa mgonjwa sana,mbili akiwa mzee,tatu akiwa mlemavu,nne akiwa majeruhi /akiwa na majeraha.
Kinyume na hapo mwanaume huwa anawajibika kubeba majukumu yake na matatizo yake mikononi mwake yeye mwenyewe.
Miongoni mwa mambo ambayo husababisha Watu wengi kulia sana na kujuta sana ni kuishi kwa ile dhana ya "wema hauozi,ukitenda wema leo ,siku yoyote ile ule wema wako utakurudia katika njia ambazo hauna matarajio yoyote"
ukweli mchungu ni kwamba maisha hayo yapo kwenye movies na tamthilia lakini ukija kwenye ulimwengu halisi hamna kitu kama hicho.
angalia mifano hapa chini
-Umewahi kumfanyia mpango wa kazi rafiki yako wa karibu kisha alikwenda kujenga ukaribu uliopitiliza na mwajiri wako kisha akazusha uongo juu yako kisha wewe ukafukuzwa kazi akabaki yeye kwenye kazi ambayo wewe ndiyo umemfanyia mpango ?
-Umewahi kumsaidia rafiki yako/ndugu yako ambaye alikuwa anapitia manyanyaso kutoka kwa mwenza wake kisha baada ya kumpatia hifadhi nyumbani kwako , rafiki yako wa karibu anajenga mahusiano ya kimapenzi na Mwenza wako kisha akakugombanisha na mwenza wako mkaachana akabaki yeye na mwenza wako?
-Umewahi kumsaidia mwenza wako ambaye alikuwa hajasoma lakini ulimsomesha,alikuwa hana kazi ulimtafutia kazi,alikuwa hana biashara ukamtafutia mtaji,alikuwa hana ndugu wala marafiki lakini ukamkaribisha kwa ndugu zako na marafiki zako kisha alifanya kazi ya kukufitinisha na ndugu zako,pamoja na marafiki zako mpaka mnagombana na kuvunja mahusiano baina yenu?
-Je umewahi kumpokea rafiki yako ambaye alikuwa ni mgonjwa sana,ambaye hana kazi wala biashara yoyote kisha baada ya kumsaidia sana akakuwekea sumu kwenye chakula ili ufe abaki na mali zako ?
-Je umewahi kumsaidia mtu ambaye hana pa kuishi kwa kumpa hifadhi kisha baada ya kupazoea mahali unapoishi akaiba fedha zako zote na kutokomea kusikojulikana?
-Je umewahi kumuamini sana Mwenza wako au rafiki yako kiasi cha kumuacha huru kujua nyaraka za mali zako zote ,kisha alikwenda kubadilisha majina ya hati miliki ya mali zako zote kisha akakubambikia kesi na kutokomea kusikojulikana?
- je umewahi kumuamini sana rafiki yako wa karibu lakini ghafla akamtongoza mwenza wako ghafla ukaibuka ugomvi baina yako na Mwenza wako kisha mkaachana yeye akamchukua Mwenza wako?
kama haujawahi kupitia hali kama hizo ni rahisi sana kuamini kwamba ukiwa mwema sana kwenye jamii inakuwa tiketi ya kuishi kwa amani utulivu na furaha ukiwa na kila mtu.
MAMBO YA KUZINGATIA
-Mwizi ataiba bila kujali wewe ni mwema kwake kiasi gani
-Msaliti atakusaliti bila kujali utakuwa muaminifu kwake saa 24 miaka yote ya uhai wako
-Mtu mwenye sifa ya kudhulumu atakudhulumu bila kujali utakuwa mwema sana kwake
-Tapeli atakutapeli bila kujali utakuwa mwema sana kwenye jamii
-Mtu mwenye tabia ya dharau, majivuno, kiburi,na ujuaji ataonyesha tabia hizo kwako bila kujali utakuwa mwema sana kwake miaka yote.
MAMBO YA KUEPUKA
Epuka kujenga mahusiano ya kimapenzi na Mwanamke au mwanaume ambaye anakuja kwako akiwa na matatizo labda ni Mwanamke mwenye huzuni, simanzi, majonzi, upweke uliopitiliza, hasira kupindukia, analia muda wote wakati huohuo anapitia kipindi kigumu sana kifedha, ametelekezwa na ujauzito au watoto.
ukifanya kosa la kujenga naye mahusiano kwa kutarajia kwamba atakupenda sana kwa kukulipa fadhila za wema ambao umeufanya kwake ,utalia sana siku sio nyingi.
Mwenza ambaye kwako anakuja kama tatizo atakubali kuwa na wewe kwa sababu anapitia matatizo,anapitia kipindi kigumu sana kifedha,anapitia upweke,anapitia huzuni, simanzi na majonzi kwa wakati huo haujui tabia zake.
Utajua tabia zake halisi pale ambapo utakuwa umempa fedha nyingi sana kwa ajili ya kumhudumia, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama, kumjengea, kusaidia sana ndugu zake,kujenga nyumbani kwao, kumsomesha mtoto ambaye ametelekezwa naye.
mkono mtupu haurambwi.Ukiona wewe pekee ndiyo unatumia fedha nyingi sana,nguvu nyingi sana kubadilisha maisha ya mwenza wako wakati yeye havuji jasho lolote kwa niaba yako lazima tu atakaposimama vizuri kiuchumi, kielimu,akiwa na kazi au cheo atakugeuka na atakudhalilisha sana wakati anakuacha .
Lakini atarudi tena kwako pale ambapo anataka kukutumia kama tambara la deki ili apate MSAADA wa kifedha na faraja yako.
Mtu ambaye anakuona sio wa HADHI yake akiwa na furaha na mafanikio hafai kuwa mwenza wako pale ambapo atakuwa anapitia kipindi kigumu sana kifedha au kiafya kwa sababu punde tu hali yake ya kiafya na kifedha ikiwa nzuri atakuona takataka, atakuona bwege, atakuona hauna hadhi ya kuwa na yeye.
Ukiona upo na fedha nyingi sana wakati huo mwenza wako hana kitu chochote ambacho anafanya chenye manufaa kwako ujue anakutumia kama tambara la deki ili akiwa vizuri aondoke kwenda kwa watu wa hadhi yake.
-Ukiwa mwanamke,endapo utakuwa katika mahusiano na mwanaume ambaye hana kazi,wala biashara yoyote,hataki kazi,hajishughulishi kwa chochote ili aweze kubeba majukumu yake ipasavyo ni wazi kwamba anakutumia kama tambara la deki,siku akiwa vizuri kiuchumi anakuacha ghafla bila kujali jasho lako kwake.
MAHUSIANO KUVUNJIKA AU KUDUMU HAYATEGEMEI JUHUDI ZAKO TU
Baada ya mahusiano kuvunjika ndipo utagundua kwamba kujiweka hatarini, kujinyima chakula ili mwenza wako ale, kuhatarisha uhai wako ili kumfurahisha mwenza wako, kumsomesha, kumjengea, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama mwenza wako sio GUARANTEE ya kupendwa wala kudumu na mwenza wako.
unaweza kujitoa mhanga kumfariji, kumliwaza, kumtetea, kumpa ushauri, kumbembeleza sana mwenza wako lakini siku chache baadaye unamfumania akiwa na mtu mwengine kwenye kitanda ambacho unalala wewe.
unaweza kuacha kazi kwa ajili ya kumfurahisha mwenza wako kisha yeye anakuacha ghafla bila sababu zozote za msingi
unaweza kumtoa mwenza wako kwenye hali ya kudhalilishwa hadharani kwenye jamii mpaka kubadilisha maisha yake akawa mtu mwenye kuheshimika sana kwenye jamii kisha akakuacha ghafla kwenda kwa mtu mwingine ambaye hajavuja jasho lolote kwa mwenza wako.
MAISHA HALISI SIO MOVIES NA TAMTHILIA
"Niliwafanyia 1,2,3 wapo pia wanatakiwa kunifanyia 1,2,3 ,nikiwa katika hali kama ya kwao"
Huu sio utaratibu halisi kwenye maisha.
Maisha hayaendeshwi kwa tit for tat kwamba "Nimefanya 1,2,3 na wewe fanya 1,2,3 kama nilivyofanya kwako".
maisha halisi hayaendeshwi kwa misingi ya kujitoa mhanga kumfurahisha mtu mwengine bali kwa misingi ya kuheshimiana na kufanya uadilifu.
Pima faida na hasara za maamuzi yako sio kutarajia kwamba wema wako kwa jamii yako itakuwa kinga dhidi ya kuumizwa, kuibiwa, kudhulumiwa, kutapeliwa, kupokonywa mali, kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho,kubambikiwa kesi, kufilisiwa,na kusalitiwa.
-Kuwa mwema lakini sio kujilinda dhidi ya ubaya wa Watu kwa kutenda wema
-Jali Watu wengine lakini kujali watu wengine sio kinga ya kupuuzwa , kuachwa mpweke ukiwa na matatizo
-Sema watu wengine kwa mazuri lakini sio kinga ya kuzushiwa kashfa za uongo
-Kuwa mwaminifu kwa watu lakini uaminifu sio kinga dhidi ya kusalitiwa na Watu wengine
-Kuwa mpole kwa Watu wengine lakini upole sio kinga dhidi ya ubabe wa Watu wengine.
-Kuwa na huruma kwa Watu wengine lakini huruma sio kinga dhidi ya ukatili, udikteta, utemi, dharau,na ujeuri wa Watu wengine.