Dunia haiko fair, leo mtoto wa Nyerere analalamika watu Serikali hawapokei simu za familia ya Nyerere

Mwanaume yeyote anayekuwa busy sana kutimiza lengo fulani anatakiwa kuwa na mke shupavu atakayekaba majukumu ya kifamilia. Malezi ya watoto wa Nyerere yalipaswa kufanywa zaidi na mke wake ambaye alikuwa na muda na anashinda nao zaidi. Hii ni failure ya Mama Maria zaidi kuliko Mwalimu mwenyewe.
 
Ndio wajifunze kwamba kuna wengine wanateseka zaidi ya hapo, Bora yeye viongozi hawapokei simu lkn wanahudumiwa vzr tuu yamkini kuna akina sisi pangu pakavu tia mchuzi..

Ila mwanasiasa ni mtu wa dhulma sana, hebu fikiria kiongoz wa serikali kama waziri ama Raisi anagharamiwa maisha yake kwa pesa za serikali na bado analipwa mshahara mnono na kupewa huduma Bora ya afya, lakini kuna mkulima huko kijijini ambaye kula yke tu ni ya shida akiumwa inabidi alipe gharama za matibabu ..

Hivi inaingia akilini kwel?? Yule ambaye analipwa mshahara mnono anagharamiwa matibabu, lkn maskini ambaye ana kipato duni ajigharamie hii imekaaje??..
 
Ile taasisi ya Mwl Nyerere nani anaiendesha na faida yake ikoje
 
Balaa Sanaa

Nukuu ya baba wa taifa.
""UTII UKIZIDI SANAA HUZAA UOGA, UOGA UKIZIDI SANA HUZAA UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA NA MWISHO WAKE NI MAUTI""
 
Kwani makongoro Nyerere sio mtoto wa Nyerere?
 
Hivi nyie mnaifahamu familia ya Nyerere au mpo hapa kuchangamsha genge? Familia ya Nyerere haina shida na kamwe haitakuja kuwa na shida. Hao watoto wanapiga kelele kwa shida moja tu ya kutaka kusikilizwa na sio shida ya njaa ya hela. Mwanao unaweza kumpa kila kitu lakini akikuita 'baba! Baba!" alafu ukampotezea utakuwa umemuumiza sana na kumnyanyasa kisaikolojia. Watoto wa Nyerere wanataka kila wakikohoa watetemekewe kitu ambacho hakiwezekani. Kuhusu kufanikiwa, Nyerere amefanikiwa sana na ataendelea kufanikiwa na kuenziwa vizazi hadi vizazi pindi nchi idumupo! Legacy yake inaishi katika nyanja zote kisiasa, kielimu, kiuchumi, kiungozi, kiuzalendo, nk. Hakutatokea mtu nchi hii akashika dola hasipotembelea nyota ya Nyerere!
 
Nilitaka nishangae kwamba hiyo familia isipewe royalty. Ina maana hao watakula matunda mpaka kizazi chao kitapofutika ila nina wasiwasi mama Nyerere asipokuwepo wanaweza kupotezewa kabisa kuliko ilivyo sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…