Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Kwa miaka mingi tumekuwa tukifundishwa kwamba mafanikio yana formula moja tu. Soma kwa bidii, pata kazi, kuwa na nidhamu, vumilia kwa miaka mingi, halafu siku moja utafanikiwa. Ukweli ni kwamba njia hii bado ipo na bado inafanya kazi.
Lakini dunia ya leo imebadilika kwa kasi ambayo wengi hawajaitambua. Ujio wa internet, social media na teknolojia umefungua milango mipya ya mafanikio ambayo zamani haikuwepo. Leo unaweza kuanzia na simu mkononi na ndani ya muda mfupi ukajenga jina, biashara au kipato kikubwa.
Ukisikiliza watu wengi waliofanikiwa kwa njia za zamani, watakupa principles ambazo hazina ubishi. Discipline, consistency, commitment na patience. Hizo ndizo msingi wa mafanikio na hazitapoteza thamani yake.
Tatizo ni kwamba watu wengi wanafikiri hizo ndizo njia pekee za kutoboa. Wanasahau kwamba dunia imebadilika, na fursa zimebadilika pia.
Leo attention imekuwa bidhaa yenye thamani kubwa kuliko ilivyokuwa zamani. Ukiweza kuwafanya watu wakutazame, wakusikilize au wakukumbuke, tayari umefungua mlango wa opportunities ambazo zamani zilihitaji miaka mingi kuzifikia.
Hebu angalia mifano michache.
- Khaby Lame alipoteza kazi kipindi cha COVID-19. Akaanza kutengeneza video fupi bila hata kuongea. Leo ni mmoja wa content creators wanaolipwa zaidi duniani.
- Kili Paul, kijana wa Kimasai kutoka Tanzania, alianza kwa kuimba na ku-lip sync nyimbo za Kihindi akiwa kijijini. Leo anatambulika duniani, amekutana na mastaa wakubwa na amejenga brand kupitia simu yake.
- IShowSpeed alianza kwa livestream ambazo watu wengi waliziona kama kelele za kawaida. Leo ana mamilioni ya followers, deals kubwa na ushawishi mkubwa duniani.
- MrBeast alianza YouTube akiwa mtoto. Wakati wengine walikuwa wanamwona anapoteza muda, yeye alikuwa anajifunza internet. Leo ni mmoja wa creators wakubwa na wafanyabiashara wenye ushawishi mkubwa duniani.
Ukifuatilia hawa wote, utaona kitu kimoja kinachofanana. Hawakufuata njia ambazo kila mtu alikuwa anafuata. Walijaribu kitu tofauti, wakaendelea kukiboresha mpaka dunia ikawapa nafasi.
Point yangu si kwamba watu waache discipline au waache kufanya kazi kwa bidii. Hapana. Ninachosema ni kwamba watu waache kuamini kuna njia moja tu ya mafanikio.
Jipe nafasi ya kujaribu vitu mbalimbali. Unaweza kuanza biashara mtandaoni, kutengeneza content, kujifunza skill mpya, kuanzisha podcast, YouTube, TikTok au hata kujenga personal brand yako LinkedIn. Huenda mlango wako upo sehemu ambayo hujawahi kuthubutu kuingia.
Kingine kinachowaua watu wengi ni aibu. Tunahangaika sana kuwaza, "Jamii itanichukuliaje?" Wakati huo huo wale waliotucheka jana ndiyo wanaokuja kuomba connection baada ya kuona umefanikiwa.
Kama jambo unalofanya halivunji sheria, halikiuki maadili na halina madhara kwa mtu mwingine, usiogope kulijaribu. Mara nyingi watu hucheka kile ambacho hawajakielewa, lakini wakiona kimezaa matunda wanataka kujua ulianzaje.
Na mwisho, usiwe bize kutafuta mafanikio mpaka usisahau kuishi. Tenga muda wa kufurahi na familia yako, tengeneza moments za kukumbukwa, rekodi video, pigeni picha, hata mkifanya TikTok challenge pamoja si dhambi. Siyo kila content inalenga kuwa viral, nyingine zinatunza kumbukumbu ambazo pesa haziwezi kununua.
Dunia imebadilika. Swali siyo kama mabadiliko yapo, swali ni kama wewe umebadilika pamoja nayo.