Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Usipojitambua mwenyewe wanaojitambua watatafuta namna ya kukutambulisha na wewe kukubali utambulisho huo kuwa ni wewe.
Dunia umejawa na upekee kwa ajili ya kila mtu wapekee kama wewe na siyo mwingine na hii inatokana na ukweli kuwa upekee ndiyo ladha ya maisha "varieties is the spice of life"
Tafuta nafasi yako na fanya kilicho chako,haipo sababu yoyote ile ya msingi inayotutaka tuishi maisha yetu katika namna ileile.
Leo ushindani ni mkubwa kutokana na kuigaiga badala ya kuibua upekee wetu Duniani.Siyo sawa kabisa kwa binadamu kufanya kitu kilekile na kwa namna ileile.
Usikubaliane na mafundisho yoyote yanayopingana na ukweli kuwa wewe ni wa pekee na una kitu chako cha pekee unachopaswa kujifanyia ili Dunia ionje ladha ya upekee wako.
Katika kujitambua unaweza kufanya mambo mengi sana ili kutambua nafasi yako na ukishajitambua fanya kilicho chako.
Dunia inasubiri na inatoa mianya mingi na tofautitofauti kwa kila mtu na katika mazingira yote.Angalia kwa makini ili kuona mwanya wako.
Kuamini katika upekee na kufanikiwa siyo miujiza ila ni matokeo ya binadamu kujitambua kusudi la uwepo wake.
Kutambua kusudi la uwepo wako Duniani ni wajibu wa kila aliyeumbwa na Mungu katika kutekeleza kusudi la uwepo wake na kutekeleza kusudi lako kunakupa nafasi ya kuona thamani yako.
Hayupo aliyekuja Duniani bila kusudi la kuwepo kwake,ninaamini kuwa linatangulia kusudi ndipo anafuata mtekelezaji wa kusudi hilo.
Kutekeleza makusudi ya uwepo wetu Duniani ndiyo siri ya utajirisho wa mwili nafsi na roho za binadamu Duniani.
Hakuna furaha kubwa kama tuishi maisha yaliyopo chini ya kusudi la uwepo wako,na ninahisi maisha hayo ndiyo haswaa tunayopaswa kuyachuchumilia.
Jiulize "nimekuja kufanya nini katika Dunia hii?"..ukianzia hapo unaweza kuendelea kujitafuta ulipo na kuona nafasi yako.