1. Wamba Dia Wamba
2. Laurent Nkunda
3. Bosco Ntaganda
4. Mamadou Ndala
(Wakishaanza kuzungumziwa tu hawa jamaa huwezi kusikia majina ya miji kama Kinshasa au sijui Lubumbashi, Mzee humu utasikia tu RCD Goma, RCD Kisangani, Mbuji Mayi, Kananga)
5. Slobodan Milošević (Mwanamama Oumilkheir anaunguruma saa 7 mchana DW Radio, unasikia tu vita va kugombea Jimbo la Kosovo kati ya Waserbia na Wakurdi)
6. Hujatulia kidogo unasikia kuna Kanali Bakari kashakorofisha huko Comoro.
7. Mara unakutana na ugomvi wa Bi Angela Merkel na Gerhard Schröde, unasikia mara sijui mrengo wa kijani, huelewi kitu Mzee 😅😅.
8 Huko Afghanistan kwenye milima ya Tora Bora kuna muhuni anaitwa Mullah Mohammed Omar nae kakiwasha.
9. Twende mashariki ya kati sasa: Huku utasikia ukanda wa Gaza, magharibi ya mto Jordan. Humu hayawezi kukosekana majina kama Benjamin Netanyahu, Mahmoud Abbas, Shimon Peres na Baba wa taifa la Palestine toka chama cha ukombozi PLO, hapa namzungumzia Yaser Arafat.
10. Huwezi kukosa taarifa ya India na Pakistan kugombania Jimbo la Kashmir, hapa humkosi muhuni Perves Musharraf.
11. Hujakaa sawa unasikia Muamar Ghadafi na Hosni Mubarak wana kikao sijui wanajadili amani kati ya Israel na Palestine.
12. Sudani napo kuna habari za John Garang anagombania ukombozi wa Sudan kusini toka kwa Omar El Bashir
Ilikua ni kama unaangalia movie vile. Kuna muda unajiuliza hawa jamaa wako serious ama wanaigiza, maana matukio ni episode after episode. Unajaribu kujenga picha huko kwenye hizo nchi watu wanaishije?! Aiseeh kumbe nishakua Mzee sasa, maisha yanaenda kasi sana. Nimechoka kutype. 😅