Dunia imesimama na Rais Samia Suluhu Hassan hoja ya Teenage Mothers

Mimba za watoto wa shule na umaskini ni pacha. Kupunguza hili tatizo lazima na umaskini upungue
 
Kama wameruhusu ningependa na wale wanaowapa mimba wapewe adhabu ndogo ili kulinda ustawi wa mtoto asiye na hatia...
Baba gerezani na mama yuko shule, huyo mtoto ataanza kufunzwa na ulimwengu mapema sana.
 
Nadhani hii ndio hoja ya msingi zaidi.

Kwanza ziwekwe seria kali za kulinda hawa mabinti zetu na watoto wetu wa kike na kiume waliopo shule wapewe elimu ya uzazi mapema sana.

Tatizo la msingi nadhani linaanzia kwenye familia zetu, Je sisi kama wazazi tunaongea na binti zetu au watoto wetu wa kiume kuhusu elimu ya uzazi?

Pia sheria zetu zingejikita kwenye kushawishi na kufanya ngono na mtoto under 18 liwe ni kosa la jinai kabisa na mtu akikutwa aadhibiwe kama waingereza wanavyofanya.

So far ni vizuri kurudisha watoto waliopata ujauzito shuleni ila sheria zetu bado haziwalindi hawa mabinti wetu.
 
Hebu toa sababu kwanini mliwazuia wasirejee shuleni baada ya kuzaa
1.hawakuzuiwa wasirejee shuleni waliruhusiwa kusoma kwenye shule za private za ufundi na mambo mengine ya kijamii
2.funzo kwa wanafunzi wengine kutopata ujauzito wakiwah shuleni.
3. Kuwapa mda wa kulea na kuwatunza watoto wao vizuri
4. Kuwapunguzia mzigo wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na kuepusha mzigo kwa wanafamilia
 
Umeongea ya muhimu sana mkuu
 
Kwahiyo mlijigeuza watetezi wao,

Wapi walisema hawayawezi hayo?
 
Safi sana! Una Big Vision sana wewe!
 
Unaweza kutukumbusha mwaka gani nchi hii watoto wa kike waliopata ujauzito wakirejea mashuleni?
Zile harakati za kupima mimba mashuleni zilikuwa kwaajili gani? Zilianza lini na zilikoma lini?
Kikwete aliwahi kusema watoto wa kike kubeba mimba ni kiherehere Chao
Magufuli akamalizia kabisa kusema hasomeshi wazazi shule za umma.
Wazazi wanaojitambua hawakumuacha mtoto wao aliezaa abaki nyumbani Bali walikuendeleza lakini sio shule za umma na hakukuwa na zuio hata Mara moja.
Kufanikiwa kuacha siasa za watu na kuyajadili maslahi mapana ya taifa hili itakuwa hatua kubwa sana kwa nchi yetu.
 
Zanzibar imo nchini Tanzania na inatumia mfumo wa elimu ya Tanzania lakini wasichana waliopata mimba huruhusiwa kuendelea na masomo wakijifungua! Mapacha wangu Kulwa ni wa kichina na Doto wa kisomali!
Zanzibar sio Tanzania
 
Juhudi zimefanyika na nikubwa sana, Ukitaka kujua wewe mpe Mwanafunzi mimba ndio utaziona juhudi za Serikali,
Juhudi za kusubiria tatzo ndio mchukue hatua? Hizi sio hatua effective inatakiwa serikali na jamii ije na hatua mbadara za kuzuia mimba kabla haijatokea sio kusubiria tatzo litokee Ndio mchukue hatua tena hatua zenyewe zinaweza leta chuki kwa mzazi mtoto.
 
Toa way forwards
 
Umeandika vizuri ila hausomeki mkuu wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…