Dunia imetawaliwa na low thinkers


Kwahiyo ukweli ni kwamba nguvu zipo ndani yetu na si kama wasemavyo wanadini kuwa mungu ndio humfanikisha mtu.
 
Wengine wanaenda kuombewa wapate magari....

Kuomba hakuhitaji dini yo yote. Wewe ukitaka cho chote unapata. mfano. "Ninataka kuwa daktari". iwapo utaiweka hii kwenye subconsious mind yako sawa sawa mwisho wa siku utakuwa daktari na sio dereva wa malori. Sasa hapo dini ni ipi?
 

Kwahiyo unataka unataka kusema hata hapa Tanzania hatuendelei na ni masikini kwa sababu ya dini??
 
Kuomba hakuhitaji dini yo yote. Wewe ukitaka cho chote unapata. mfano. "Ninataka kuwa daktari". iwapo utaiweka hii kwenye subconsious mind yako sawa sawa mwisho wa siku utakuwa daktari na sio dereva wa malori. Sasa hapo dini ni ipi?

Kwahiyo hata Lowassa angeweka subconsious mind yake sawasawa angekuwa rais??
 

Mie mkuu bado sijapata ufafanuzi zaidi ni vp dini na siasa zinazuia watu kufikiri??
 
Nimeingia mkuku-mkuku hapa nikidhani kuna kitu nitajifunza kutokana na kichwa cha habari ambacho kwa kiasi fulani kinaakisi tawala nyingi za ulimwengu wetu.

Mtoa mada hujatuonesha "HOW" umefikia hilo hitimisho/conclusion, umekua mchoyo wa maarifa, tafadhali funguka Mkuu, naamini kuna mambo mengi sana ya kujifunza kutokana na kichwa cha habari cha uzi wako.

Na jambo jingine ningeomba wanabodi kupunguza kutupiana vijembe hasa kwenye masuala ya imani, na ikitokea mchangiaji utaongea kitu kitakasogusa imani/dini, hebu jaribu kujenga hoja bila dhihaka kwa imani/dini husika kwa kukumbuka hapa ni jukwaa la intelegensia, siyo uwanja wa imani/dini, tulitendee haki jukwaa na tusiharibu 'nyuzi' kwa vijembe, ubishi na ushabiki wa kidini/imani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…