Dunia imetawaliwa na low thinkers

Dunia imetawaliwa na low thinkers

Wale ambao hawana dini wanaamini juu ya kila ambacho wanakifanya. Nadhan unajua kabisa kuwa ukijenga iman juu ya kila unachokifanya mara nyingi unafanikiwa na hiyo inatokana na physic power ambayo kila mtu anayo. Kinachotakiwa ni kuweka na kuamini juu ya kile unachokifanya ANY THING IS POSSIBLE.

Kwahiyo ukweli ni kwamba nguvu zipo ndani yetu na si kama wasemavyo wanadini kuwa mungu ndio humfanikisha mtu.
 
Wengine wanaenda kuombewa wapate magari....

Kuomba hakuhitaji dini yo yote. Wewe ukitaka cho chote unapata. mfano. "Ninataka kuwa daktari". iwapo utaiweka hii kwenye subconsious mind yako sawa sawa mwisho wa siku utakuwa daktari na sio dereva wa malori. Sasa hapo dini ni ipi?
 
Nakubaliana na wewe kwamba dini ndio zinawafanya watu wasifikiri kabisa. Ukiangalia nchi maskini utagundua ndio wanapambana na dini kuliko zilizoendelea. Dini zinawafanya watu watumwa wa fikra wasiweze kufikiri zaidi ya kuamini wasichokijua.

Binadamu hajaweza kutumia uwezo wake wa kufikiri kwa sababu mbali mbali ikiwemo dini. Itambulike kwamba fikra ndio kila kitu. Kila kitu duniani kimetokana na fikra au wazo. Dini zitakuambia kuwa kila kitu kimeumbwa na Mungu. Huu sio ukweli. Mungu aliumba mara ya kwanza tena vitu vichache tu, lakini binadamu ndiye amekuwa akiumba vingine hadi leo. Mtoto akizaliwa ni matokeo ya uhai uliwekwa ndani mwanaume ukiunganishwa na mazingira ya uumbaji kwenye tumbo la uzazi la mwanamke na baadae kutokea au kumanifest kama binadamu. Hapa sii Mungu bali binadam wameendeleza uumbaji. Leo hii Mungu haumbi tena. Hii ndio procreation. Ila tukisema Mungu aliumba binadam tuko sahihi.

BTW Mbegu ya mwanume ndiyo yenye uhai tuu. Bahati mbaya hata yai la mwanamke halina uhai.

Najua wengine mtapiga mawe lakini ni kwa sababu ya dini zao.

Kwahiyo unataka unataka kusema hata hapa Tanzania hatuendelei na ni masikini kwa sababu ya dini??
 
Kuomba hakuhitaji dini yo yote. Wewe ukitaka cho chote unapata. mfano. "Ninataka kuwa daktari". iwapo utaiweka hii kwenye subconsious mind yako sawa sawa mwisho wa siku utakuwa daktari na sio dereva wa malori. Sasa hapo dini ni ipi?

Kwahiyo hata Lowassa angeweka subconsious mind yake sawasawa angekuwa rais??
 
Katika mkusanyiko wa sayari nyingi na nyota mbalimbali kunauwezekano mkubwa kwenye sayari zingine mamilioni kukawa na viumbe hai.

Kwakutumia formula za kimahesabu uwezekano wa kuwepo viumbe kwenye sayari zingine ni asilimia mia.

Lakini kwa utawala wa sasa wa dunia ni mbovu kiasi cha kufanya watu wasifikiri sana. Dunia imetawaliwa na siasa na dini. Watu wanajificha kwenye mgogo wa dini au siasa na kuacha kabisa kutumia akili zao inavyotakiwa.

Viongozi wa dini wamewapumbaza watu kiasi cha kushindwa kuwaza zaidi ya vitu wajuavyo.

Ningependa sisi GT tujaribu kutoa mawazo yetu na kuruhusu kujifunza zaidi.

Hebu fikiria watu wanauana kwa kigezo cha dini au siasa. Hivi inaingia akilini kweli?

Mie mkuu bado sijapata ufafanuzi zaidi ni vp dini na siasa zinazuia watu kufikiri??
 
Nimeingia mkuku-mkuku hapa nikidhani kuna kitu nitajifunza kutokana na kichwa cha habari ambacho kwa kiasi fulani kinaakisi tawala nyingi za ulimwengu wetu.

Mtoa mada hujatuonesha "HOW" umefikia hilo hitimisho/conclusion, umekua mchoyo wa maarifa, tafadhali funguka Mkuu, naamini kuna mambo mengi sana ya kujifunza kutokana na kichwa cha habari cha uzi wako.

Na jambo jingine ningeomba wanabodi kupunguza kutupiana vijembe hasa kwenye masuala ya imani, na ikitokea mchangiaji utaongea kitu kitakasogusa imani/dini, hebu jaribu kujenga hoja bila dhihaka kwa imani/dini husika kwa kukumbuka hapa ni jukwaa la intelegensia, siyo uwanja wa imani/dini, tulitendee haki jukwaa na tusiharibu 'nyuzi' kwa vijembe, ubishi na ushabiki wa kidini/imani
 
Back
Top Bottom