Dunia ina mambo, ukiwa na pesa unaweza kufanya chochote

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327

Wahenga wenzangu wa zamani nadhani mtakua mnamkumbuka dada kama si mama ambaye alipata kuimba kua dunia ina mambo...ooh mwanangu dunia ina mambo ..dunia hii mama lukumba lukumba dunia ina mambo mwendo wa ngamia..

Katika pitapita zangu kwenye mitandao nikakutana na habari ambayo imenishangaza kama si kunistaajabisha, huyu kijana wa miaka 33 kutoka nchi fulani ya west afrika tajiri wa kutisha na mwenye vibweka kama si vya kutisha na kushangaza, amefanya jambo ambalo liliwafanya watu wabaki mdomo wazi..

Kuwachukua na kutembea na wanawake saba na kuwapa ujauzito wote kwa wakati mmoja, na wote habari njema wamejifungua, nikimanisha mimba zilipotimia miezi tisa wote walijifungua japo kila mwanamke kwa wakati tofauti

Huyu jamaa pesa zinanchanganya kiasi kwamba alishawahi kununua mdoli wa kike mwanzoni na akataka kufunga nako ndoa na sherehe kubwa sana, sababu ni kua alidai wanawake wana "stress" sina uhakika na hili mana si wanawake wote ni pasua kichwa, anyway jambo hilo likashindikana..

Huyu kijana akienda mahali anapanda farasi, anatembea na wadada wa kumwagia maua kila anapopita, mara nyingine wanambeba, mara nyingine anaingia mahali na mbilikimo ambao wamebeba matunguli, aisee..

By the way afya za mama na watoto saba zinaendelea vizuri.

Pesa!
 
Na wewe tafuta za kwakoule bata kidogo kabla Allah hajachukuwa pumzi yake broo acha kulia lia kama Demu aliyeumizwa.
 
Ila pesa yako haiwezi kuzuia wachinba kaburi lako huku wewe ukiwa kwenye jeneza
 
Ila pesa yako haiwezi kuzuia wachinba kaburi lako huku wewe ukiwa kwenye jeneza
Kwaio mkuu ndivyo ambavyo kutokua na pesa ama kutotafuta pesa tunafarijiana ya kwamba tutakufa na hata zikiwepo nyingi za kutosha haiwez wazuia wachimba kaburi? Kwani usipokua na pesa hautakufa au wachimba kaburi kuchimba kaburi lako?
 
Kuna rafiki yangu alipataga hela ya urithi anachokumbuka ni kulala na wanawake watatu kwa mpigo anadai ni yeye na Iddi Amini Dada ndio waliofanya huo uhuni basi.Tuko naye maskani sasa tunabangaiza .Hela tamu jamani.
 
Kaka nahisi ni hadith ya kufikirika.Habari haina picha,haina nchi iliyotokea wala haina jina la muhusika.Hili litakuwa ni changa la macho
 
Huenda anatimiza masharti aliyopewa ili kulinda huo utajiri..
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…