BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,327
Wahenga wenzangu wa zamani nadhani mtakua mnamkumbuka dada kama si mama ambaye alipata kuimba kua dunia ina mambo...ooh mwanangu dunia ina mambo ..dunia hii mama lukumba lukumba dunia ina mambo mwendo wa ngamia..
Katika pitapita zangu kwenye mitandao nikakutana na habari ambayo imenishangaza kama si kunistaajabisha, huyu kijana wa miaka 33 kutoka nchi fulani ya west afrika tajiri wa kutisha na mwenye vibweka kama si vya kutisha na kushangaza, amefanya jambo ambalo liliwafanya watu wabaki mdomo wazi..
Kuwachukua na kutembea na wanawake saba na kuwapa ujauzito wote kwa wakati mmoja, na wote habari njema wamejifungua, nikimanisha mimba zilipotimia miezi tisa wote walijifungua japo kila mwanamke kwa wakati tofauti
Huyu jamaa pesa zinanchanganya kiasi kwamba alishawahi kununua mdoli wa kike mwanzoni na akataka kufunga nako ndoa na sherehe kubwa sana, sababu ni kua alidai wanawake wana "stress" sina uhakika na hili mana si wanawake wote ni pasua kichwa, anyway jambo hilo likashindikana..
Huyu kijana akienda mahali anapanda farasi, anatembea na wadada wa kumwagia maua kila anapopita, mara nyingine wanambeba, mara nyingine anaingia mahali na mbilikimo ambao wamebeba matunguli, aisee..
By the way afya za mama na watoto saba zinaendelea vizuri.
Pesa!