Dunia ina Umri gani?

Dunia ina Umri gani?

Nadhani inategemea na namna tu unavyotazama MAENDELEO.

Ukitazama maendeleo kama mchakato unaoathiriwa na mambo kadhaa kama Mila na Mazingira (CULTURE & ENVIRONMENT), basi utaona utabadili mtazamo huu wa kuwa 'sisi wa sasa' tunaakili au tumeendelea kwa kasi kuliko wa 'zamani'.

Licha ya dunia kuwa na umri zaidi ya miaka Bilioni 13, mwanadamu (huyu wa sasa) amekuwepo takribani miaka 200,000 tu iliyopita. Hadi alipoanza kulima na kufuga na kuacha maisha ya kulandalanda miaka 30,000 KK ndipo Kasi kubwa ya maendeleo alianza kuipiga hapa—TAWALA ZA KISIASA mf Mesopotamia, MILA NA DESTURI, SERIKALI, ZANA ZA KAZI NA VITA NA UBUNIFU NDIO ULIOANZA HAPA. Bila kuanza kilimo, wabunifu wasingekuwepo kwani hawakuwa na hofu tena ya njaa wasipotafuta chakula.

Toka miaka 30,000 KK kuja mbele, mwanadamu amekuwa akifanya bunifu mbalimbali ambazo ndio hadi sasa zimewezesha kasi hii unayoisema sasa.

Mfano 1. Gunpowder ilivumbuliwa kwanza miaka ya 140BK na kuja kuwa sawia mwaka 900 BK bunduki yake ikaja tengenezwa mwaka 1000BK. Risasi ya kwanza yenye kufanana na 'usasa' ilitengenezwa mwaka 1400.

Mfano 2. Kompyuta ilianza vumbuliwa miaka ya 1880, semiconductor ilivumbuliwa 1870. Lakini ni toka mwaka 1820 ndipo semiconductor as a concept ilianza kuappear kwa kina Thomas Seebeck. Ambao nao kuna kazi ilifanywa na watu awali ya kuchaganya Potassium n.k ili kuitengeneza. Navyo vilihitaji umeme ambao ulivumbuliwa miaka ya 1700. So, unaweza jiuliza ilitokea nini toka mwaka 1700 ndio Kompyuta ipatikane 1880!?

Mfano 3. Rejea historia ya Locomotive.

Hoja yangu ni kuwa, maendeleo ni mchakato ambao unarithishwa kizazi hadi kizazi, ambapo ili upate teknolojia fulani—ambayo ndio nguzo ya maendeleo ya mwanadamu—ni muunganiko wa vumbuzi mbalimbali za nyuma ambazo zimepitia vipindi virefu vya 'Trials and Errors'.

Kasi ya maendeleo inaathiriwa pia sana na Masuala ya mazingira na tamaduni. Mfano, ni ukweli kuwa toka 1500, ndio maendeleo yalishika kasi sana sababu ya kupitia ZAMA ZA MUANGAZA. Ambazo zilibilisha sana Ulaya. Kwa vipi? FIKRA HURU NJE YA DINI NA TAFITI NDIO ZILIANZA ONGOZA MAISHA YAO.

Matibabu yalianza chunguza hasa nini kinatokea kwenye mwili wa wanadamu badala ya kuhusianisha magonjwa na imani za kimungu—MAENDELEO MAKUBWA YA FANI YA AFYA NA UTABIBU.

Uongozi ukaanza kutazamwa kwa UWEZO(MERITOCRACY) na si KUZALIWA—UFALME UKAFA, na kuanza kwa demokrasia, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora—INCLUSIVE SOCIETIES. So, kama Enlightenment ideas zingeanza mwaka 1000BK, pengine Kompyuta zingevumbuliwa 1500. 😄
But agriculture seems to be the most successful scam in humankind history according to historian Miss Yuval Noah harrari
 
Wanajamvi Salam.
Leo nataka kujua zaid kuhusu mada fikirishi ya umri wa dunia. Kupitia hadithi mbalimbali za historia na vitabu vya dini, zinatuambia Kwamba Dunia ilianza takriban miaka million kadhaa huko nyuma. Pia watu walioishi miaka hiyo ya nyuma sana inasimuliwa na kuaminika kwamba walikua ni watu wenye maumbile makubwa sana kimwili, wenye nguvu sana, wenye akili sana, majasiri, wenye uthubutu, na sifa nyinginezo kedekede.
Swali langu la msingi ni kwamba, kwa huu umri wa Dunia unaosimuliwa na aina ya watu waliokwepo zamani, kwanini Civilization na technological advancement zimechelewa sana? Kwanini maisha ya zamani yalikua magumu sana, (only strongest survived) Kwanini maisha yamekua some how simplified kuanzia karne ya angalau ya 15 hapo?
Does it mean hao watu wa zamani walikua vilaza sana tofauti na historia zinavowapamba? Kama sio, kwanini hawakuwa na hiyo akili na uvumbuzi wa teknolijia ambayo ingepunguza ugumu wa maisha tokea miaka hiyo??

Kwa wale Watu wazima waliozaliwa miaka kati ya 1930 hadi 1970 ambao wako hai hadi leo, wanasema wameishi katika ulimwengu wa zaid ya aina 3 hapahapa duniani. Kwanini wanasema hivyo? Angalia gap la mabadiriko ya dunia kuanzia 2010 hadi sasa, Rudi nyuma Kidogo angalia mabadiriko ya dunia ya 2000 hadi 2010, kisha endelea kurudi nyuma kwa kuangalia dunia ya miaka chini ya 2000. Nadhani hapo utakua umepata picha kidogo ya swali langu. Dunia ya 2000 ni tofauti kabisa na dunia ya 2023.

Hiyo dunia ya zamani na watu wake wenye uwezo mkubwa walishindwa hata kutengeneza simu ili wawasiliane? Computer zimekuja mwishoni mwa karne ya 20 (miaka ya 1940-1950) kama sikosei, Simu pia zilianza miaka ya 1980s, magari na vyombo vingi vya moto vilianza kuanzia angalau karne ya 15 hapo. Unaambiwa watu walikua wanasafiri hata miezi kadhaa wako tu njiani. Sasa hizo akili na uwezo wao mkubwa ulikua wap?

Mwisho, mi naamini hii dunia ni ya Juzijuzi tu hapo. Naombeni mje na hoja za kusema hii dunia ina hiyo miaka mamilioni.
Bhaa
 
Kulingana na hesabu ya vizazi na miaka yao waliyoishi katika biblia, inakadiriwa tangu Edeni mpaka wakati wa Gharika, ni miaka elfu 2, na tangu wakati wa gharika mpaka kuzaliwa kwa Bwana Yesu ilipita miaka elfu 2 hivi, na tangu kipindi cha Bwana wetu Yesu hata leo nacho pia ni kipindi cha miaka elfu 2 kimepita. Kwahiyo jumla yake tangu Edeni mpaka sasa ni miaka kama elfu 6
Kisayansi?
 
nadhani wewe unataka kujua modern humans wametokea lini hapa duniani....ni miaka michache iliyopita sidhani kama inazidi miaka 150,000 tu

Ni juzi kabisa

Dunia ina miaka Bilioni 4 kama landmass...mwanadamu tena modern human katokea juzi tu by accident
Na binadamu ndio waharibifu wakubwa wa dunia
 
Fanya research mwaka wa kwanza wadunia jumlisha hadi sasa ×360days halafu utapata jibu
 
Mr dewij
I'll like to answer you in the manner that outrageous brave man will take a grasp of the concept.

Imagine me and you we are mechanizing a car , let's say it takes us 20 years to modernise it and later on future, it turns out that after all the car isn't working anyhow.

But comes a strange guy who tell us we got everything on point except that we needed an engine to get it started, you see here a guy design an engine and off it go the car is finely working and the guy take all the credit,

It's not fair isn't it, after all it took us two decades

Here is what I mean everything, modern or new which is regarded as hyper technology, advanced one ofcourse it's a series of old sweat of these brave minds who devotedly ventured their souls into creating and innovating

While some of them their work was unfortunately left unfinished, it didn't remain that way , some of their works are being accomplished each and everyday that's what makes us look like we outsmart them but in reality it's their bravely that brought us all here and we should forever be grateful to these gentle, hard working, great thinkers and unknown souls who didn't descend in history for their hard working spirit and devotion which makes this world today beautiful as we see it


It was series of pain and sweat to fight ignorance so that you and I today we can be so brave enough to understand the work of these beautiful souls.

Auf wiedersehen.
FlyingDutchman
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Back
Top Bottom