Ave Kitomary
New Member
- May 7, 2024
- 2
- 1
Matumizi ya mitandao ya kijamii sasa yanaongezeka kwa kasi Duniani na kufanya kila mtu kuwa rahisi kuwasilina na kujua vitu vinavyoendelea Duniani.
Takwimu zinaonesha kuwa watu bilioni 4.7 kote ulimwenguni wanatumia mitandao ya kijamii ambapo ni sawa na asilimia 59 ya watumiaji.
Kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 29.169 kwa kipindi cha Juni 2022 hadi milioni 31.122 kwa Septemba 2022 sawa na ongezeko la asilimia 6.7.
Hivyo ongezeko la watumiaji wa intaneti linaonesha kwamba kulikuwa na ukuaji wa takriban asilimia 17 kila mwaka katika kipindi cha miaka 5 ambapo mwaka 2017, kulikuwa na watumiaji Milioni 16,106,636 na mwishoni mwa mwaka 2021 waliongezeka kufikia Milioni 29,103,482.
Matumizi ya intaneti yameongezeka kutoka wastani wa MB 6,037, kwa mtumiaji Machi 2022 hadi MB 6,626 kwa mtumiaji Septemba 2022 na kuenea kulikuwa asilimia 78 mwaka 2017, asilimia 81 mwaka 2018, asilimia 88 mwaka 2020 na asilimia 91 mwaka 2021.
Takwimu za TCRA zinabainisha kuwa mitandao mitano ya kijamii inayotumiwa zaidi ni FaceBook uliongoza kwa kurekodi GB Bilioni 2.59, ukifuatiwa na YouTube wenye GB Bilioni 1.91, kisha WhatsApp uliokuwa na Bilioni 1.58, na TikTok ukiwa na GB Milioni 999 ikifuatiwa na mitandao mingine.
Mitandao hiyo ya kijamii iliyofikiwa zaidi kupitia kifaa kimojakimoja cha mtumiaji kama vile simu, kompyuta mpakato, kiskwambi, kompyuta ya mezani) ambapo Facebook ilikuwa na vifaa Milioni 3,487,393, WhatsApp vifaa Milioni 3,415,917, YouTube vifaa Milioni 2,846,839, Instagram vifaa Milioni 2610,509 na TikTok vifaa Milioni 1,601,392.
Matarajio makubwa ni kuwa bado kutakuwa na ongezeko la watumiaji wa simu kwa kadiri miaka inavyokwenda kwani sayansi na teknolojia zinakua na pia watu wanatamani kwenda na wakati.
Wakati matumizi hayo yakiongezeka na kila mtanzania kutamani kuwa katika mitandao lakini bado kuna madhaifu makubwa kuhusu suala na usalama mitandaoni .
Mara nyingi kupitia vyombo vya habari na mitandao tumeona watu wengi wakitapeliwa na wengine kufanyiwa udhalilishaji bila wahusika kutoelewa ni wapi sehemu sahihi ya kupata msaada wa changamoto zilizowakumba.
Wapo watu ambao wanapitia utapeli na kuamua kujidhuru na hata kufikia hatua ya kujiua baada ya kutuma fedha kimakosa kwa kutumiwa taarifa za uongo.
Pia wapo watu ambao wamepitia changamoto ya kudhalilishwa na kushindwa kujiamini tena katika uwanja huo na wengine kuacha kabisa matumizi ya mitandao huku wengine wakikubwa na msongo wa mawazo ambao mpaka sasa haujatibika .
Hatua hizi zimeleta athari kwa jamii licha ya serikali kutangaza kusajili laini kwa kutumia kitambulisho cha Taifa ili kudhibiti uhalifu mitandaoni lakini bado idadi ya matukio inaongezeka hivyo haikuwa suluhu ya tatizo hilo.
Watumiaji wengi wa mitandao hawana elimu ya kutosha kuhusu namna ya kuripoti matukio ya utapeli na udalilishaji wanaofanyiwa huku wengi wao wakiwa hawajui haki zao ya matumizi ya mitandao.
Hapa nchini matumizi ya mawasiliano ikihusisha mitandao ya kijamii yanasimamiwa na TCRA hasa katika suala la kupata mtandao wa wahalifu .
Lakini likija suala la kufuatilia wahalifu wa mitandaoni jeshi la polisi kitengo cha uhalifu mitandao ndilo linalohusika kufuatilia na kuwakamata wahalifu hao japo sio kesi zote uhalifu wa mitandaoni kama udalilishaji.
Kutokana na hili matarajio ya kupambana na kuzia uhalifu mitandao bado hayajafikiwa kwani hakuna mamlaka inayosimamia moja kwa moja uhalifu za mitandaoni hasa pale mtu anapotapeliwa au kudhalilishwa.
Hali hii inawafanya hata watu wanapokutana na mikasa ya uhalifu mitandao hawajui pa kwenda kuripoti na hata wakienda polisi masuala haya kutokuchukuliwa kwa uzito.
Nini Kinatakiwa kifanyike
Matarajio ya kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ni suala lisilopingika .
Na pia ukuaji wa teknolojia ikiwemo matumizi ya akili mnembe katika mitandao ya kijamii itaongezeka kulingana na mabadiliko ya kidunia na Tanzania haliwezi kuepuka wala kulikimbia hilo.
Hivyo miaka ijayo dunia kwa kiasi kikubwa itakuwa ikiendeshwa kidigitali kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo mawasiliano ya kibiashara ,kikazi na mawasiliano mengine.
Napendekeza nchi kuunda mamlaka au taasisi itayajihusisha moja kwa moja na kupambana na kudhibiti uhalifu mitandaoni kama ilivyo kwa taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU).
Majukumu ya Taasisi au mamlaka hiyo ya kuzuia na kupambana na uhalifu mitandaoni itakuwa na majuku yafuatayo
Kwanza kutoa elimu kwa jamii matumizi sahihi ya mitandao hasa ya kijamii na jinsi dunia sasa inavyoelekea katika matumizi ya akili mnembe ,sheria zinazosimamia mitandao na hatua anazopaswa kuchukua mtumiaji anapokutana na matukio ya uhalifu mitandaoni.
Pili taasisi au mamlaka hizo ifuatilie kwa ukaribu hali ya matumizi ya mitandao na kushughulikia malalamiko yote yanayohusu mitandao kuanzia kwa mtu mmoja mmoja au hata matukio ya uhalifu yanayohusishwa na mitandao ya kijamii ikiwemo uvunjifu wa maadili kama kusambazwa kwa picha na video za uchi.
Kufuatilia biashara za mitandaoni na taarifa zingine ambazo zinalenga kutapeli watu wengine .
Matokeo
Kwa kufanya hivi itasaidia kuwakamata haraka watu wanaofanya uhalifu mtandaoni na kesi zao zitachukua muda mfupi hivyo kurahisisha hatua muhimu ya kupambana na uhalifu mitandaoni .
Elimu itafanya watumiaji kuwa na uelewa mpana hivyo kuepuka kudhalilisha wengine na utapeli na pia watakaodhalilishwa watapata urahisi wa kutoa taarifa haraka ili kupata haki zao.
Kupitia matumizi ya akili mnembe utapeli hasa wa kibishara utaweza kudhibitiwa mitandaoni kwasababu kuna mamlaka ambayo imeweka nguvu kubwa katika kufuatilia mitandao.
Mwishooo…

Upvote
3