Dunia inazalisha Chakula cha Kutosha, Lakini Afrika bado njaa ni Kubwa

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Mapambano ya Njaa duniani na harakati za kufikia lengo la pili (Zero hunger) kati ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 17 zinaonekana kuzaa mtunda, Takwimu zinaonesha Njaa imepungua kwa mwaka wa tatu mfululizo, lakini kwa mara ya kwanza, Afrika ina idadi kubwa ya watu wenye njaa kuliko Asia.
Hapa Tanzania, swali la msingi siyo “kuna chakula au hakuna?” bali ni “je, familia zina uwezo wa kumudu mlo kamili na bora?”

Group.jpg

​
Kidunia, maendeleo Yapo, Lakini ni ya Polepole Sana.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 645 (sawa na 7.8%) walikabiliwa na njaa mwaka 2025, ikiwa ni wamepungua kutoka kilele cha watu milioni 709 waliorekodiwa mwaka 2022.
Pamoja na hayo, watu bilioni 2.69 bado hawawezi kumudu lishe bora, jambo linalofanya lengo la 2030 la "Njaa Sifuri" (Zero hunger) kuwa gumu kufikiwa.

Screenshot_16-10-2026_15623_claude.ai.jpeg
Screenshot_16-10-2026_15634_claude.ai.jpeg

Africa tuna historia Mpya: Afrika sasa kwa mala ya kwanza Inaongoza kwa Njaa Kuliko Asia
Takriban Waafrika milioni 309 walikuwa na utapiamlo mwaka 2025, ikilinganishwa na milioni 292 barani Asia. Asilimia ya watu wenye njaa imeshuka kidogo (kutoka 20.3% hadi 20.0%), lakini kasi ya ongezeko la idadi ya watu inafanya jumla ya wanaoathirika kuongezeka. Sasa Afrika inabeba takriban 48% ya watu wote wenye njaa duniani, na kufikia mwaka 2030 huenda ikafika 56%.

Screenshot_16-10-2026_15821_claude.ai.jpeg

Screenshot_16-10-2026_15837_claude.ai.jpeg

*Watu wawili kati ya watatu barani Afrika (66.6%) hawawezi kumudu lishe bora, kiwango ambacho ni zaidi ya mara mbili ya kile cha Asia au Amerika ya Kusini.

Changamoto kubwa Afrika ni kupanda kwa Gharama ya chakula:
Kwa mujibu wa shirika la chakula duniani (FAO), Wastani wa gharama ya kupata lishe bora barani Afrika ulipanda kutoka Dola za Kimarekani TSh 7,309 hadi TSh 11,530 kwa mtu mmoja kwa siku, kati ya mwaka 2019 na 2024 ( sawa na ongezeko la 37%).

Hii inaonyesha kuwa kwasasa njaa ni tatizo la bei, siyo suala la ukosefu wa mazao mashambani pekee.

Hapa kwetu ni wazi Maghala yamejaa, Lakini Sahani bado zipo Tupu!
Kwa mujibu wa Takwimu za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kulikuwa na takriban tani 560,000 za nafaka kufikia mwishoni mwa Februari 2026. Hata hivyo, ripoti ya SOFI 2026 inakadiria kuwa asilimia 73 ya Watanzania, sawa na watu milioni 51.5, hawakuweza kumudu mlo bora kufikia mwaka 2025.

Screenshot_16-10-2026_151625_claude.ai.png

Taarifa nzuri ni kwamba: FAO inaiorodhesha Tanzania kati ya nchi 14 za Afrika zilizofanikiwa kupunguza asilimia ya watu waliokuwa hawawezi kumudu lishe bora kati ya mwaka 2019 na 2024.

Lakini bado kuna Njaa iliyojificha: Kulingana na utafiti wa afya na idadi ya watu wa mwaka 2022 (TDHS), takriban asilimia 58 ya watoto chini ya miaka mitano na asilimia 45 ya wanawake wa umri wa kuzaa walikuwa na upungufu wa damu (anemia), wakati uzito na unene uliopindukia uliathiri asilimia 36 ya wanawake.
*Hii inaweza kuashiria upatikanaji mdogo wa mlo sahihi au utamiaji uliopitiliza wa mlo usio sahihi.

Nini kifanyike?
Bila ya shaka uvumbuzi na ubunifu ndio muarobaini wa Tatizo letu,
Ripoti ya SOFI 2026 inaonyesha kuwa minyororo ya thamani ya mazao ya kilimo ndiyo inayochochea bei za chakula bora, na inapendekeza kuwepo kwa mfumo wa karibu wa kufuatilia gharama na uwezo wa wananchi ili viongozi waweze kuona mabadiliko ya bei mapema kabla hayajaleta madhara.

Mavuno mazuri ni hatua ya kwanza tu. Uhifadhi mzuri, usafirishaji, masoko na bei rafiki ndizo zitakazoamua nani anayekula vizuri na nani anayebaki na njaa au Lishe isiyo bora.

Wakuu leo ni Oktoba 16, 2026, siku ya chakula duniani na hapo juu ndio hali halisi.
Suala la kuwa na chakula cha kutosha kama nchi sio tatizo tena, kwasasa tatizo ni bei ya chakula.

Wakuu nawaacha na maswajili mawili;

  1. Kipi hasa kama nchi tunapaswa kukifanya ili kupunguza changamoto ya bei za vyakula nchini na kuhakikisha kila mtu anaweza kumudu lishe bora?
  2. Unadhani utitili wa madalali kwenye mnyororo wa mazao ya kilimo inaweza kuwa sababu ya Bei za vyakula kuwa juu?
  3. Au Tatizo sio bei ya vyakula bali ni umasikini na nguvu ndohgo ya manunuzi (Purchasing power) ya Watanzania
Sources
SOFI_2026
FAO_Global hunger statistics and trends
TDHS-MIS 2022_Ministry of Health Tanzania
NBS Microdata_hemoglobin variable
Utafiti wa 2026 kuhusu upungufu wa damu Tanzania unaotumia TDHS 2022
 
Attachments

  • Screenshot_16-10-2026_151225_claude.ai.png
    Screenshot_16-10-2026_151225_claude.ai.png
    212.2 KB · Views: 8
Sisi ni mijitu ya hovyo, hatujali utu, hatupendani. Na hili ni tatizo la jamii nzima. Yaani unaweza ukawa unalaumu viongozi lakini usisahau hao viongozi sio wameshushwa kutoka mbinguni, ni wajomba zetu, shangazi zetu, baba zetu, mama zetu n.k. Matatizo ya waafrica yamejengwa na waafrica wenyewe kutojitambua wanataka nini.
 
Tatizo la afrika ni kuongozwa viongozi wabinafsi, wenye roho mbaya

Fikiria hizo b700 za eli nino zingeelekezwa kwenye kilimo cha kisasa chini ya usimizi mzuri
 
Pale USA kuna watu hawana makazi wala chakula, kuna maisha lakin huwezi kuyaona hadi ufike pale,
Ni africa ndio tunaongoza kujiaibisha, Wenzetu hawana huo mda😀,
 
Sisi ni mijitu ya hovyo, hatujali utu, hatupendani. Na hili ni tatizo la jamii nzima. Yaani unaweza ukawa unalaumu viongozi lakini usisahau hao viongozi sio wameshushwa kutoka mbinguni, ni wajomba zetu, shangazi zetu, baba zetu, mama zetu n.k. Matatizo ya waafrica yamejengwa na waafrica wenyewe kutojitambua wanataka nini.
Sisi ni manyani. Tunataka tuwe na mikia. Ngozi hii ya rangi ya TAKO tuna shida sana.
 
Ngoja nile nishibe nipate cha kukoment..
Maana inafikirisha san
 
CCM mjifunze , Nchi haindeshwi Kwa political science, Economy measures
 
Si rahisi kwa watu wajinga kuishinda njaa.

Kuishinda njaa tunahitaji
1. Miradi mikubwa ya umwagiliaji. Mungu katujalia maji mengi ya kutosha.
2. Viwanda vya mbolea. Bahati nzuri gesi na phosphates kwa ajili ya mbolea tunavyo. Tutahitaji kuagiza potash tu.
3. Viwanda vya zana kama matrekta nk. Hapa nchi inahitaji kwanza kuweza kuzalisha chuma kwa ajili ya hizo zana.

Tukituliza akili na kuacha mapepe ya kilimo kwanza na Big Results Now na tukaweka nia tutaweza jilisha na kuuza sana misosi.
 
Well said
 
GDP per Capita inabidi iongezeke ili kuendana na bei za sasa. Watu waongeze vipato vyao tufike angalau USD 4500
 
Mradi wa umwagiliaji kwenye mashamba yetu wanasubiri mpaka aje mzungu kufunga mabomba. Sasa hawa wasomi wetu walifuata nini huko vyuo.
Nchi ya kifala sana hii vikuu
 
Mapambano ya Njaa duniani na harakati za kufikia lengo la pili (Zero hunger) kati ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 17 zinaonekana kuzaa mtunda, Takwimu zinaonesha Njaa imepungua kwa mwaka wa tatu mfululizo, lakini kwa mara ya kwanza, Afrika ina idadi kubwa ya watu wenye njaa kuliko Asia.
Hapa Tanzania, swali la msingi siyo “kuna chakula au hakuna?” bali ni “je, familia zina uwezo wa kumudu mlo kamili na bora?”

Kidunia, maendeleo Yapo, Lakini ni ya Polepole Sana.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 645 (sawa na 7.8%) walikabiliwa na njaa mwaka 2025, ikiwa ni wamepungua kutoka kilele cha watu milioni 709 waliorekodiwa mwaka 2022.
Pamoja na hayo, watu bilioni 2.69 bado hawawezi kumudu lishe bora, jambo linalofanya lengo la 2030 la "Njaa Sifuri" (Zero hunger) kuwa gumu kufikiwa.

Africa tuna historia Mpya: Afrika sasa kwa mala ya kwanza Inaongoza kwa Njaa Kuliko Asia
Takriban Waafrika milioni 309 walikuwa na utapiamlo mwaka 2025, ikilinganishwa na milioni 292 barani Asia. Asilimia ya watu wenye njaa imeshuka kidogo (kutoka 20.3% hadi 20.0%), lakini kasi ya ongezeko la idadi ya watu inafanya jumla ya wanaoathirika kuongezeka. Sasa Afrika inabeba takriban 48% ya watu wote wenye njaa duniani, na kufikia mwaka 2030 huenda ikafika 56%.

*Watu wawili kati ya watatu barani Afrika (66.6%) hawawezi kumudu lishe bora, kiwango ambacho ni zaidi ya mara mbili ya kile cha Asia au Amerika ya Kusini.

Changamoto kubwa Afrika ni kupanda kwa Gharama ya chakula:
Kwa mujibu wa shirika la chakula duniani (FAO), Wastani wa gharama ya kupata lishe bora barani Afrika ulipanda kutoka Dola za Kimarekani TSh 7,309 hadi TSh 11,530 kwa mtu mmoja kwa siku, kati ya mwaka 2019 na 2024 ( sawa na ongezeko la 37%).

Hapa kwetu ni wazi Maghala yamejaa, Lakini Sahani bado zipo Tupu!
Kwa mujibu wa Takwimu za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kulikuwa na takriban tani 560,000 za nafaka kufikia mwishoni mwa Februari 2026. Hata hivyo, ripoti ya SOFI 2026 inakadiria kuwa asilimia 73 ya Watanzania, sawa na watu milioni 51.5, hawakuweza kumudu mlo bora kufikia mwaka 2025.

View attachment 3691850

Taarifa nzuri ni kwamba: FAO inaiorodhesha Tanzania kati ya nchi 14 za Afrika zilizofanikiwa kupunguza asilimia ya watu waliokuwa hawawezi kumudu lishe bora kati ya mwaka 2019 na 2024.

Lakini bado kuna Njaa iliyojificha: Kulingana na utafiti wa afya na idadi ya watu wa mwaka 2022 (TDHS), takriban asilimia 58 ya watoto chini ya miaka mitano na asilimia 45 ya wanawake wa umri wa kuzaa walikuwa na upungufu wa damu (anemia), wakati uzito na unene uliopindukia uliathiri asilimia 36 ya wanawake.
*Hii inaweza kuashiria upatikanaji mdogo wa mlo sahihi au utamiaji uliopitiliza wa mlo usio sahihi.

Nini kifanyike?
Bila ya shaka uvumbuzi na ubunifu ndio muarobaini wa Tatizo letu,
Ripoti ya SOFI 2026 inaonyesha kuwa minyororo ya thamani ya mazao ya kilimo ndiyo inayochochea bei za chakula bora, na inapendekeza kuwepo kwa mfumo wa karibu wa kufuatilia gharama na uwezo wa wananchi ili viongozi waweze kuona mabadiliko ya bei mapema kabla hayajaleta madhara.

Mavuno mazuri ni hatua ya kwanza tu. Uhifadhi mzuri, usafirishaji, masoko na bei rafiki ndizo zitakazoamua nani anayekula vizuri na nani anayebaki na njaa au Lishe isiyo bora.

Wakuu leo ni Oktoba 16, 2026, siku ya chakula duniani na hapo juu ndio hali halisi.
Suala la kuwa na chakula cha kutosha kama nchi sio tatizo tena, kwasasa tatizo ni bei ya chakula.

Wakuu nawaacha na maswajili mawili;

Sources
SOFI_2026
FAO_Global hunger statistics and trends
TDHS-MIS 2022_Ministry of Health Tanzania
NBS Microdata_hemoglobin variable
Utafiti wa 2026 kuhusu upungufu wa damu Tanzania unaotumia TDHS 2022
Afrika au Tanzania kuna maeneo mengi watu wana saza chakula. Kwanini mtu anachagua kuishi mahali ambapo atakuwa hana uhakika wa kula?
 
Back
Top Bottom