Dunia isingekuwa na changamoto yeyote binadamu asingeweza kumkumbuka Mungu.

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari kwa wote!
Imani yangu wote ni wazima.

Kabla ya yote naomba tufanye assumptions chache ili mada iwe nyepesi na tuzungumze vyema.
Assumptions hizo kama ifuatavyo:-
  1. Dunia ni ideal. Ideal nikiwa na maana ya hakuna changamoto/matatizo kwa binadamu.
  2. Binadamu anaweza kufanya kitu/jambo lolote bila kushindwa(chochote kile anafanikiwa).
Haya twende kwenye mada huku nikizielezea hizo assumptions mbili kwa kina zaidi.

Dunia sababu ni non-ideal kwa maana ya imejaa changamoto nyingi kwa binadamu toka anazaliwa mpaka anakufa. Hapa atakutana na njaa,utafutaji wa mavazi,malazi,magonjwa,mapenzi,n.k.

Vyote hivi ni baadhi ila vinafanya binadamu kukosa amani.

Sasa kumbe sababu kuna changamoto za hapa na pale binadamu uanza kukosa hope na kutafuta wapi ataweza kupata hayo matumaini.
Mfano mzuri angalia sasa Covid-19 watu walikuwa wanaishi baadhi ya watu walikuwa hawakumbuki kabisa kama kuna Mungu.​
Kuona hadi sasa naandik uzi huu hakuna dawa rasmi iliyothibitika ya huu ugonjwa hapo sasa watu wakakumbuka kama kuna Mungu.​
Tuzungumze kidogo je,binadamu angekuwa na uwezo wa kufanya chochote duniani na kufanikiwa angeweza kumkumbuka Mungu?
Nawasilisha.

Kichwa Kichafu.
 
Mimi ni muislamu,
Katika Qur-an Mungu kasema
''Lau kama tungeli mpa kila mtu utajiri na mali,basi binadamu angelifanya kiburi na majivuno mno katika ardhi''
Lakini kwa makusudi Mungu kakadiria kwa kuwapa wachache na kuwanyima wengine ili maisha ya kutegemeana yawepo na wengine wajaribiwe kwa wengine.
Naunga mkono hoja, Bila ya Mfumo huu binadamu asingeliweza mkumbuka Mungu Ng'o.
 
Wengi wanaoamini Mungu ni kwa kutumainia mema waliyoahidiwa, maombi mengi ni ya wenye shida na yamejikita kuomba utatuzi wa changamoto.... waliofanikiwa wengi hata kushukuru hujisahau.

Kila apataye husifu akili yake.
 
Kuna watu wakipata changamoto wanakata tamaa na kuona hakuna maisha tena.
Mimi ni muislamu,
Katika Qur-an Mungu kasema
''Lau kama tungeli mpa kila mtu utajiri na mali,basi binadamu angelifanya kiburi na majivuno mno katika ardhi''
Lakini kwa makusudi Mungu kakadiria kwa kuwapa wachache na kuwanyima wengine ili maisha ya kutegemeana yawepo na wengine wajaribiwe kwa wengine.
Naunga mkono hoja, Bila ya Mfumo huu binadamu asingeliweza mkumbuka Mungu Ng'o.
 
Kiukweli tunatakiwa kumkumbuka Mungu wakati wote, iwe furaha ama changamoto, ila kiubinadamu huwa tunazidisha maombi wakati wa matatizo na kurelax baada ya shida zetu kuisha.

Nakumbuka kuna changamoto nilikua naipitia kipindi fulani aisee niliona kabisa bila msaada wa Mungu siwezi,basi nikasali baadaye shida ikaisha nikarudi normal ,aisee nikaanza kujiona kama ni mimi tu nimepambana shida imeisha ,nishasahau ni Mungu🙄🙄
 
Bila changamoto wengi wanasahau kama kuna maisha hayo!
Kiukweli tunatakiwa kumkumbuka Mungu wakati wote, iwe furaha ama changamoto, ila kiubinadamu huwa tunazidisha maombi wakati wa matatizo na kurelax baada ya shida zetu kuisha.

Nakumbuka kuna changamoto nilikua naipitia kipindi fulani aisee niliona kabisa bila msaada wa Mungu siwezi,basi nikasali baadaye shida ikaisha nikarudi normal ,aisee nikaanza kujiona kama ni mimi tu nimepambana shida imeisha ,nishasahau ni Mungu[emoji849][emoji849]
 
Back
Top Bottom