Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Kabla ya mdahalo wa urais wa leo Donald Trump alikuwa ameamuacha Joe Biden kwenye kura za maoni. Lakini mdahalo wa huu umefunga kabisa maneno. Ni wazi kuwa Trump sasa njia ya ikulu ni nyeupe kabisa. Biden alikuwa na hoja nzuri na aliandaliwa vyema ila afya yake na uelewa wake sababu ya uzee vimemuangusha. Si mtu fit kushika madaraka ya urais. Sasa tujiandae na dunia ya Rais Trump, itakuwaje?
1. Hoja kubwa ya Trump ambayo aliikazia na kuilazimisha ni juu ya wahamiaji haramu. Bila shaka atakomaa sana na hii ishu, sijui itakuwaje?
2. Trump ana bifu kali la kibiashara na China, ataongeza kodi na vikwazo vya kibiashara kwa China. China atajibuje? Itakuaje kwa dunia?
3. Vita ya Russia na Ukraine. Trump atawezaje kuizima. Alipoulizwa alikazana tu kuwa angekuwa Rais vita isingetokea, lakini hakusema ataizimaje. Atapunguza misaada ya kijeshi kwa Ukraine?
4. Sema wote Biden na Trump wanaiogopa mno Israel.
5. Jamaa anaweza kukuza uchumi wa Marekani na kushusha Inflation?
Naiona Dunia chini ya Trump kama Rais wa Marekani kama Dunia hatari sana