Dunia itakuwaje Trump atakapoapishwa kama Rais wa Marekani hapo mwakani?

Jidanganye, usidhani kule mtu anaongiza nchi kwa matakwa yake. Tuliwahi kusema Boris akiondoka ktk ofisi ya PM UK basi UK itaacha kusapoti Ukraine, akaja mmama fulani na sasa hivi ni huyu Mhindi ila moto uko palepale.
Dunia ni salama sana hawa viongozi wawili wakitawala kwa wakati mmoja, jumlisha Kiduku na Kiawa (sucess-driven man) wa China ndiyo kabisaa!
 
Sio kwa Trump, Trump ni muoga na mlamba miguu wa Putin.

Ikitokea ameshika power atachofanya ni kuikabidhisha rasmi Ukraine kwa Urusi.
 
4. Umeongea kama mtu usie elewa Geopolitics

Hawaiogopi Israel ila hawawezi jinasua kutoka kwa sponsor wao wa kampen na Israel ilishawai ua rais wa marekan
 
Sio kwa Trump, Trump ni muoga na mlamba miguu wa Putin.

Ikitokea ameshika power atachofanya ni kuikabidhisha rasmi Ukraine kwa Urusi.
Wala si uoga bali ni akili. Haikuwepo sababu ya msingi ya Marekani kujilazimisha pale jirani na Urusi.

Hata yeye mwenyewe hapendi adui kumpumulia kisogoni. Kwa nini afanye uchonganishi kwa Ukreni?
 
Israel imeandikwa katika siri ya AMERICA yeyote atakayeingia lazima Aitambue
 
Wala si uoga bali ni akili. Haikuwepo sababu ya msingi ya Marekani kujilazimisha pale jirani na Urusi.

Hata yeye mwenyewe hapendi adui kumpumulia kisogoni. Kwa nini afanye uchonganishi kwa Ukreni?
Mjadala wa Ukraine na Urusi haujawahi kuwa na ukomo

Kinachojadiliwa hapo ni maslahi ya taifa la Marekani kuanzia nguzo kuu ya kiusalama.

Tangu kitambo inafahamika Marekani ni adui wa Urusi lakini kinachokuja kushangaza ni pale unapoona Putin anamkubali Trump na kutamani Trump ashinde uraisi.
 
Ikitokea, nasema ikitokea, Trump akachaguliwa urais, lazima Putin ahudhurie uapisho wake pale kwenye mnara wa Washington.

Hawa jamaa wawili huenda ni watoto wa baba mmoja. Ni maswahiba hadi Marekani yenyewe inaogopa.
Vita inaisha chap, jamaa ni classmates wale πŸ˜‚
 
Ikitokea, nasema ikitokea, Trump akachaguliwa urais, lazima Putin ahudhurie uapisho wake pale kwenye mnara wa Washington.

Hawa jamaa wawili huenda ni watoto wa baba mmoja. Ni maswahiba hadi Marekani yenyewe inaogopa.
Akipita Trump ,tunaomba na Boris arudi pale uingereza...as long tuna Putin ,dunia itakua salama Sana.
 
Akipita Trump ,tunaomba na Boris arudi pale uingereza...as long tuna Putin ,dunia itakua salama Sana.
Kilichomponza Boris Johnson ni kule kufokafoka na kujifanya ana uwezo wa kumdhibiti Russia kwa kidole gumba.

Angetumia busara zaidi kuliko mihemko na kuwasikiliza wapenda-damu wenzie, leo angekuwa angali utawalani na akisifika sana miongoni mwa viongozi wakuu duniani.

Maelfu ya maisha ya watu wasiokuwa na hatia yangenusurika kifo. BJ angekuwa ndiye shujaa hasa kwenye usuluhishi wa mgogoro huo.

Hakika alikuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kuunda timu imara za wafalme katika pembe kuu 4 za dunia, kama alivyotarajiwa tangu utoto wake.

Nani asiyejua kwamba pamoja na Putin kuchukiwa sana na mrengo wa kushoto wa ushirika wa NATO na wengineo, lakini nyuma ya pazia anavutia mioyoni mwao?

Wengi wao wanatamani sana hiyo nafasi aliyo nayo huyo jahani na jahabu (legend & restorer) wa Mosko iwe ndiyo yao. Nadhani wanaona wivu juu ya mafanikio yake.

Si ajabu wanajaribu kila ngenga za kumchokonoa na kumchokoza afanye kosa moja tu la kimkakati ili wapitie humo. So far Putin has outsmarted them all.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…