Dunia itakuwaje Trump atakapoapishwa kama Rais wa Marekani hapo mwakani?

Sawa tu. Trump ashinde tuone upepo unageukaje duniani
 
Trump Alishasema Africa inabidi itawaliwe tena nimemnukuu
 
Akili mnembo hii yani hauamini kichwa chako?
 
Uzuri wa Marekani Katiba yao iko vizuri na wabunge wana macho na akiharibu tu anaondoka kwa impeachment. Angalau wenzetu wako vizuri kuliko sisi.
Na HAKUNA Rais wa Marekani aliyewahi kuondolewa madarakani kwa impeachment.
 
Jidanganye, usidhani kule mtu anaongiza nchi kwa matakwa yake. Tuliwahi kusema Boris akiondoka ktk ofisi ya PM UK basi UK itaacha kusapoti Ukraine, akaja mmama fulani na sasa hivi ni huyu Mhindi ila moto uko palepale.
Trump alisha wahi kusema ataiondoa Marekan NATO na shirika la afya duniani WHO
 
Hivi Trump akishinda anaweza akagombea tena muhula wa mwingine baada ya huu wa Novemba 2024
 
Who cares? Wote hao ni mashetani na wanyonyaji wakubwa.
 
Mwisho wa Marekani ndio umefika.Akiwa Trump ndiye raisi na hata akiendelea Biden hamna kitu tena.
 
Mwamba akipita wanaoenda kusaga meno ni China na Iran

Wakati huo huo Russia anaenda kukabidhiwa rasmi Ukraine na hapo hapo North Korea atapunguza vitisho zaidi kwa majirani zake

Wakati hayo yakitokea washirika wa Marekani (Ulaya) wanaenda kupigwa na butwaa juu ya maamuzi ya Ukraine kutelekezwa rasmi .Watabaki kuvimba na kufura juu ya bwana mkubwa (Marekani) na hawatakuwa na la kumfanya chochote kile zaidi ya hasira kali na rasilimali walizopoteza + muda waliopoteza
 
Ahsante kwa maelezo mazuri. Kwa maelezo yako inaelekea Trump akawa rais mzuri kwa wamarekani na kwa dunia pia.
 
Hamna hatari hata...awali alipokuwa Rais hiyo hatari haikuwepo.
Miaka minne aliyokaa nje dunia imebadilika sana. Ulaya kuna vita kubwa, BRICS imepamba moto, inflation nchini kwake ipo juu, nchi yake imetingwa na wahamiaji, China amekaba biashara, Saudis wanataka kuachana na petrodollar, kuna vita Gaza, Iran anazidi kuwapa nguvu washirika wake nk nk. Dunia ya kabla ya Covid ni dunia nyingine kabisa.
 
Naona LGBT wakianza kupumulia mashine... Trump na hawa mashoga ni vitu tofauti sana. Trump ni Mzee wa Sanctions lakini chini ya Sanctions zake dhidi ya Iran ndo Iran ilipojiongeza kinguvu zaidi! PM Benjamin Netanyahu anaomba Trump ashinde maana nchini Kwake Israel amekalia kuti kavu na wananchi hawamtaki ivo Akiingia Trump huenda mission ya Israel kujitanua ikafanikiwa maana Vita ya Israel Mmarekani yupo... JB alianza kunyima Netanyahu Silaha na hadi sasa aamini km Vita ya kikundi cha Wanamgambo bado haijaisha.. Na sasa anataka kupambana na Kundi kubwa na lenye Nguvu zaidi Hezbollah... Ikimbukwe Israel anajitahid sana dhid ya hilo kundi ili Waislael maelfu waliyokimbia makazi yao jirani na Lebanon warudi.. huenda Vita ikawa ya muda mrefu na US nae akachoka maana misaada anayotoa inawagharimu taxpayers wa US... Iran imefanikiwa kwa kuyapa technolgy makundi km Hezbollah la Labanon na Houth la Yemen.. .Leo hii US haamini nguvu aliyonayo wanamgambo wa Houth na jinsi wanavyoendelea kuzamisha meli za biashara licha ya US/UK kuishambulia Yemen lakin bado Houth ndo kwanza wanaendeleza campin zao... Trump ni mtu wa Biashara kwa trend inavoendelea sasa lazima hatataka vita kwasasa maana Iran ni mbishi ka shipa la ngiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…