Dunia itasimama kwa muda usiku wa jumamosi hii.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Hakika dunia itasimama kwa muda kushuhudia mpambano wa kukata na shoka kati ya Saul Arvarez (Canelo) na Daniel Jacobs "Miracle Man".

Canelo mpaka sasa amecheza jumla ya mapambano 54 ,ameshinda 51 ametoa sare 2 na amepigwa mara moja tu na bondia asiyepigika Floyd Sinclair Joy Maywether Junior.

Kwa upande wa Daniel Jacobs amecheza mapambano 37 ameshinda mapambano 35 amepigwa mara mbili , hajawahi kutoa sare. Katika mapambano hayo mawili aliyopoteza, mojawapo alipoteza kwa Gennady Gennadyevich Golovkin (GGG) kwa unanimous decision.

Ikumbukwe pia Canelo ameshacheza mara mbili na GGG ambapo pambano la kwanza walitoka sare ya Split draw ,pambano la pili Canelo alishinda kwa Majority Decisions japo kulizuka maneno makubwa kwamba Canelo alibebwa wengine walidai kuwa ushindi ulikuwa wa halali kabisa,

Hivyo basi baada ya pambano hili dhidi ya Daniel Jacobs ,Canelo atapanda ulingoni kwa mara ya tatu dhidi ya hasimu wake mkubwa GGG.


 
Canelo karuhusiwa kurudi ulingoni!??

Maana alikuwa na issue za kutumia madawa ya kuongeza nguvu..

Anyway thanks kwa info.
 
Juzi lile limbea lipuuzi ulilipa vidonge vyakeqr hadi nkafurahl , la Hovyoooo sana lile
 
Canelo karuhusiwa kurudi ulingoni!??

Maana alikuwa na issue za kutumia madawa ya kuongeza nguvu..

Anyway thanks kwa info.
Ile ishu ya madawa ilikuwa kabla ya rematch na GGG ,baadaye ikajulikana kwamba walimsingizia hivyo wakati wa rematch Canelo alikuwa na hasira sana na GGG kwa sababu alimchafua sana na kumdhihaki.
 


Hilo siyo pambano la kusimamisha dunia, kwani Danny Jacobs ni underdog, kwanza umri wake ni mkubwa kulinganisha na Canelo, pili Canelo mwepesi na ame improve sana katika defence na hii ni baada ya kupigana na kupoteza kutoka kwa Mayweather, tatu Canelo foot work yake ni nzuri kuliko Jacobs, kwa upande wa Jacobs, yeye nategemea zaidi power yake na uzoefu zaidi, juu ya yote Canelo anayo nafasi kubwa ya kushinda uninimous au KO.

Dunia itasimama wakipambana hawa; Terence crowford vs Vasyl lomachenko, Terence crowford vs Errol Spencer, Jarmell charlo vs Canelo Alvarez, Gervonta Davis vs Vasyl lomachenko,Jarmell charlo vs Genard Golovkin.
 
Shukran mtoa maada, hope nitaona marudio ya pambano
Ila mbona hujaweka mitindo wanayotumia ili tuwajue zaidi mfano orthodox au southpaw
 
Canelo naye sometimes anabebwaga tuu...lile pambano na Alvarez nilionaga hawa jamaa kama wana na syndicate flan hivi cha kupeana CV nzuri
 
Canelo naye sometimes anabebwaga tuu...lile pambano na Alvarez nilionaga hawa jamaa kama wana na syndicate flan hivi cha kupeana CV nzuri
Unamaanisha la GGG labda ama Erislandy Lara. Binafsi naona pambano alilobebwa ni hilo la Lara
 
Canelo atashinda japo mechi haitakuwa rahisi, either KO Round kuanzia ya 9 ama UD, Jacobs ni bondia mgumu sana, nilimkubali kwenye mechi yake na GGG japo alipoteza
 
Canelo atashinda japo mechi haitakuwa rahisi, either KO Round kuanzia ya 9 ama UD, Jacobs ni bondia mgumu sana, nilimkubali kwenye mechi yake na GGG japo alipoteza View attachment 1087743
Canelo kashinda kwa UD, kama nilivyosema Jacobs ni bondia tough sana, ilikuwa close fight
 
Huyu jamaa Saul Arvarez a.k.a Canelo hatari sana, ukiondoa Manny Pacqiao huyu ndo bondia kwangu anaefuatia kwa ubora

Na moja ya mapambano ambalo nahisi Money Mayweather alibebwa ni pambano alilokutana na huyu jamaa..
 
Huyu jamaa Saul Arvarez a.k.a Canelo hatari sana, ukiondoa Manny Pacqiao huyu ndo bondia kwangu anaefuatia kwa ubora

Na moja ya mapambano ambalo nahisi Money Mayweather alibebwa ni pambano alilokutana na huyu jamaa..
Usiongee hivyo mbele za watu ,watakucheka.

Katika mapambano yalikuwa rahisi zaidi kwa Floyd, basi hili la Floyd na Canelo linaongoza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…