Dunia kusimama kuelekea mpambano wa kukata na shoka kati ya Anthony Joshua na Wladimir Klitschko

Dunia kusimama kuelekea mpambano wa kukata na shoka kati ya Anthony Joshua na Wladimir Klitschko

jamani itakua muda gani wakuu na labda channel gani itarusha mubashara mpambano huo.nijuzeni tafadhali.
 
Achana na lile pambano lililobatizwa jina la "Pambano la karne" kati ya mwanamasumbwi machachali ambaye hana historia ya kupigwa wala kutoa sare tangu aanze ngumi za kulipwa, ajulikanaye kama Floyd Mayweather anayecheza stance ya Orthodox na Manny Pacquao anayecheza staili ya Southpaw


Sasa basi pambano lingine la kukata na shoka linawajia ni kati ya bondia Anthony Joshua na bondia Wladimir Klitschko


Wote hawa wanacheza stance moja ambayo ni Orthodox ,na wote rekodi zao si haba


Anthony Joshua amecheza jumla ya mapambano 18 na yote ameshinda kwa K.O na Wladmir Klitschko amecheza jumla ya mapambano 68 ,53 kashinda kwa K.O na amepoteza mapambano 4 na hajawahi kutoa sare


Anthony Joshua ni Muingereza mwenye asili ya Afrika kutoka nchi ya Nigeria ,wakati Klitschko ni Mu Ukraine


Kadri siku zinavyozidi kwenda homa juu ya pambano lao linazidi kupanda,macho na maskio yote kwa mashabiki wa masumbwi yameleekezwa kwenye pambano lao litakalo pigwa 29 April 2017 Wembley Stadium


View attachment 482466


View attachment 482467


View attachment 482469


Kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya hawa mabondia wawili upande mmoja ukidai kuwa Anthony Joshua hana experience ya kutosha ya kucheza na Klitshko lakini wakati huo huo upande mwingine unapinga vikali suala hilo kutokana na rekodi nzuri anayozidi kuionesha AJ kwa kushinda mapambano yake yote kwa knockouts


Mashabiki wa AJ walienda mbali zaidi kwa kudai kuwa baada ya kumsambaratisha Klitschko watataka pambano na Tyson Furry mbabe wa Klitschko ili na yeye wamsambaratishe


Sasa je AJ ataendeleza record yake ya unbeaten au Wladmir atalinda heshima yake ya kutopigwa na mtoto?

Majibu yote haya tunayangojea kwa hamu 29 April
Pambano litakuwa saa ngapi kwa saa za EA?
 
Pambano litaanza saa 10.10 usiku kwa saa za Uingereza,na litapiganwa uwanja wa soka wa Wembley.

Kazi kwenu kukokotoa kwa saa za EAT.
 
Pambano litaanza saa 10.10 usiku kwa saa za Uingereza,na litapiganwa uwanja wa soka wa Wembley.

Kazi kwenu kukokotoa kwa saa za EAT.
Pia wanasema muda huo utategemea na mapambano ya utangulizi.
Mageti yatakuwa wazi kuanzia saa 11 na nusu jioni, kwa saa za huko,na pambano la kwanza la utangulizi litaanza saa 12 na nusu.

Wanaongeza kwa kusema Wembley huwa panafungwa saa 4 na dakika 50 usiku,na kuhusu mpambano huu mkubwa,hakuna taarifa za kuongezwa kwa muda.
 
sio shabiki sana wa boxing ila mmenifanya nikacheki mapambabo ya uyo A J youtube jamaa ninoma akishinda naanza kufatilia akishindwa ntakuwa kama zamani
 
Back
Top Bottom