Dunia ni ngumu jitahidi kufurahi kila uwezapo

Ninachoweza kusema katika hii dunia, weka misingi mizuri ya kupata hela ili kufurahia maisha; ikiwezekana tafuta marafiki wazuri nje ya nchi wenye connection
Mungu akikubariki hata na kidogo usiache kuwakumbuka wasio na hata hicho kidogo.
 
Kwa kweli
 
Ama kwa hakika inatia faraja umpendae akupende pia.
 
Wengine tunaishi tu bora liende, Nadhani Mungu angeanza kutu-Consult kwanza kabla ya kutuleta duniani.


Hata Wewe ni wa kuongea jambo hilo??--- unamkosoa Mungu aliyekupa hadhi ya kuwa binadamu??!!, je kama angekuumba kunguni, panya au funza wa chooni, inzi nk, ili usijitambue na usimlaumu ingekuwa vizuri??-- lazima uelewe maksudi ya Mungu kukuumba wewe na heshima hii akiyokupa ya wewe kuwa binadamu/mtu, yakupasa umtolee shukrani kwani kuna maisha ya milele zaidi ya hayo maisha mafupi ya hapa duniani, wanyama hawatakuwa na maisha ya milele kama wewe, shida za dunia ni trials and tribulations katika maisha yetu, hizo trials baadhi ndio tickets za kuingia kirahisi peponi na pia ni kipimo cha wewe kumshukuru Mungu na kumkumbuka, never give up my friend the hereafter is better.

Think deeper my friend.
 
The purpose of life is to live not to exist
Afya njema ni mtaji wa kupata mengine. Kuna wanaobahatika kuzaliwa kwenye koo zenye pesa na wanatithi. Wengi tunajitafutia wenyewe.
 

umenigusa sana mkuu..
2019, 2020 , 2021 katika kila mwaka nimepoteza mtu muhimu katika maisha yangu. Jumla watatu, mmoja ndugu na wawili ni marafiki wa karibu ambao niliwapambania kiasi flani lakini haikuwa ridhki.
Huyu wa mwisho ni moja ya watu wachache ambao ningeweza kuongea nao chochote na kwa masaa bila kujihisi tofauti

nikikumbuka yupo kitandani anaumwa lakini bado ananipigia simu kunijulia hali na kunitia moyo sababu ya vitu flani, nazidi kumkumbuka. Ni mtu ambaye hakujali ukubwa wa matatizo yake ila alikuwa ana tabasamu kila mara na kutafuta furaha hata katika vitu vidogo ambavyo tunavipuuza..

Nitamkumbuka daima japo sometimes najikuta naingia whattsap kucheki previous chats na kusikiliza zile voice notes.. Forever in my heart and Rest In Peace Friend 😊
 

mkuu huwezi kujua ni vita ngapi amepigana au anapigana nazo hadi akaamua kusema hivyo, Dunia ina mitihani hii
 
Haya mambo yanasikitisha sana mkuu, yasikie tu kwa mwenzio
 
mkuu huwezi kujua ni vita ngapi amepigana au anapigana nazo hadi akaamua kusema hivyo, Dunia ina mitihani hii


Sasa inapaswa amuelekee huyo huyo Mungu kumuomba msaada, yeye si ndiye alituumba, au sio??!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…