Dunia ni uwanja wa vita za hatima

SEHEMU YA TANO.

Wakati unaenda kwa mganga au unaenda kuombewa au kupigwa dua kanisani au msikitini, kinachoombewa si hatima ila kinachoombewa ni nyota.

Nyota iko ndani ya nguvu zako za asili, kwahiyo hizi dua au maombi huwa zinanyanyua mitetemo hasi au chanya ya nguvu za asili ambazo ziko ndani yako.

Kwakufanya hivi ni kwamba ulinzi unaongezeka kwako ila sasa ule uwezo wako wa kipato unaweza usiongezeke au ukaongezeka sana na hii hutegemeana na wewe kama umeanza kuifuata ile njia ya hatima yako au bado, kama umeanza kuifuata basi baada ya hayo maombi au dua mambo yako yatakwenda vizuri sana kwa maana ile mitetemo ya mfumo nyota kutoka ulimwengu wa juu inakua iko juu sana na hapa ndio huwa watu wanasema nyota inang'aa. (Nadhani huwa mnawaskiaga watu wakisema ngoja nikasafishe nyota kidogo kwa maana mambo yangu kama yamesimama hivi) ila kama haujaanza kuielekea ile njia ya hatima yako basi kuwa na uhakika watakuombea na kukupiga dua sana ila hautakua na yale mafanikio ambayo wewe unayatarajia.

Sasa kwanini hatima huwa haiombewi au kupigwa dua ni kwamba hatima ni jambo la kiroho ambalo linamuunganiko na dunia hii ya damu na nyama ila nguvu za asili ni jambo la kiroho ambalo linamuunganiko na ulimwengu wa juu, chukulia huu mfano, mwanajeshi aliyevitani akitaka backup kutoka katika nchi yake yaani makao makuu huwa anatumia redio call kuwasiliana na watu wa makao makuu basi na wewe unapotaka backup kutoka kwa malaika walio katika mfumo nyota wako basi utatumia hayo maombi au dua au matambiko au chochote kile ambacho kimefanikiwa kunyanyua nguvu zako za asili na mara tu unavyofanya hivi basi majibu huwa yanarudi kutoka katika huo ulimwengu wa juu hadi upande wako wa kiroho na kutoka upande wako wa kiroho hadi kwenye dunia hii ya damu na nyama kupitia kiunganishi cha umiliki wa fedha na mali ambacho ni hatima, kwahiyo maombi yote ya kiroho huwa yanaishia kwenye ulimwengu wa kiroho na kutokea pale ndio kiunganishi cha kutokea rohoni hadi ulimwenguni hapa cha mahitaji ya hayo maombi kinapokea, kwahiyo mahitaji ya yale maombi ya umiliki wa mali na fadha kiunganishi chake ndio hatima.

Na hapa ndio nilikuambia sasa kwamba unapoomba maombi ya fedha majibu yake huwa yanarudi moja kwa moja kwenye hatima yako na hapa haijarishi wewe upo huko au haupo huko ila yenyewe yanaenda tu moja kwa moja kama vile mtu aliyeagiza bidhaa mtandaoni na akatoa address yake full basi mtu wa delivery atakachofanya ni kuleta mzigo kwenye address husika bila kujali wewe upo au haupo.

Pia naomba niseme hili jambo hapa, kwamba njia ya kusafisha nyota na kuichafua pia inaweza kufanywa na tendo la ndoa.

Tendo la ndoa ni tendo ambalo hufanyika kwa njia ya mwili wa damu na nyama ila liko na muunganiko wa moja kwa moja na upande wako wa kiroho.

Kila nguvu huwa inamiiko na nguvu hii ya asili miiko yake ni moja na tendo la ndoa, naomba nieleweke hapa kwanza, simaanishi kwamba tendo la ndoa ni jambo baya ila namaanisha si kila mtu afaa kukutana na wewe kimwili yaani kufanya tendo hilo la ndoa.

Kiasili mwanamke aliumbwa kuja kuongeza utimilifu kwa mwanaume hapa duniani, na moja kati ya kitu ambacho mwanamke anaweza kuongeza kwa mwanaume ni mitetemo ya mfumo nyota.

Na si tu mwanamke ndio mwenye uwezo huo wa kuongeza hiyo mitetemo ya mfumo nyota bali hata mwanaume anaouwezo wa kumuongezea mwanamke hiyo mitetemo lakini kiasili kwakua mwanaume ndio mtafutaji na ndio provider basi haifai mwanaume amuongezee mwanamke mitetemo ya mfumo nyota bali yafaa mwanamke ndio afanye hivyo kwa mumewe ili azidi kuifanya nyota ya mumewe iwake zaidi.

Sasa kwakua watu tumeundwa kwa mifumo nyota tofauti tofauti basi pia kaa ukijua kuna watu ambao wanazaliwa wakiwa na utimilifu katika mitetemo ya mifumo nyota yao na hawa huwa tunawaita wachangiaji yaani donors au powerbank.

Lakini pia kuna watu wanazaliwa huku mifumo nyota yao ikiwa si mitimilifu na hawa ndio huwa tunawaita wapokeaji yaani receivers au simu, na watu hawa pia huku kukosa utimilifu baina ya mtu na mtu huwa kunatofautiana kwahiyo huyu anaweza akawa na kasoro hii na huyu akawa na kasoro hii.

Na ninaposema utimilifu na kutokua na utimilifu namaanisha kwamba watu ambao wako timilifu kwenye mfumo nyota wao pindi wanapounganisha mitetemo inakua ya hali ya juu hadi kupelekea nyota kung'aa sana kama umeme ambao ulikata halafu ukarudi kwa wingi na wale ambao hawako na utimilifu huwa nyota zao hazing'ai sana ni kama umeme ulikata halafu ukarudi mdogo sana.

Kitu cha ajabu ni kwamba nilikwambia mwanzo kwamba wale timilifu ndio madonor ila pia kuna nyakati hata watu ambao hawako timilifu huwa wanakua madonor hasa wanapokutana na watu ambao si watimilifu pia.

Sasa angalia hapo yaani wewe umenyanyua nyota yako ikawa inang'aa japo kwa kufifia fifia halafu katika huo huo mfifio anakuja mtu anazidi kukunyonya ili nyota yako izidi kufifia zaidi.

Anyway turudi kwenye mada, kwamba kwakua watu ambao sio watimilifu huwa wanakuja na kasoro za aina tofauti tofauti basi pia hata wale watu wakuwapa huo utimilifu huwa wanakuja wakiwa wa aina tofauti tofauti.

Kwahiyo provider mwenzangu nakuasa hapa kwamba kutokana na jambo hilo ni kwamba si kila mwanamke hapa duniani amekuja kwaajiri ya kukupa utimilifu wewe kwahiyo unatakiwa kuwa makini sana na mwanamke ambae unashiriki nae tendo (hii nitailetea kipande chake cha ziada kwa maana nikiiweka hapa kwa upana itafanya hili andiko liwe refu sana na litakuchosha ila nimeweka hapa kwa uchache ili uelewe kwamba tendo la ndoa laweza kuwa njia mbadala ya kusafisha nyota).

Ila kwa sasa niseme tu kwamba...

Mifumo nyota huwa inatofautiana baina ya mtu na mtu hasa kulingana na nguvu ya asili iliyopo ndani mwake, kwahiyo basi hii inamaanisha kwamba hata njia za kufanikiwa kwenye kuzinyanyua hizi nguvu ili nyota ing'ae huwa hazifanani, sasa how? Soma hapo chini.

KWANINI MTU MWENYE NGUVU CHANYA AKIFUATA NJIA ZA MTU MWENYE NGUVU HASI HAWEZI KUFANIKIWA NA KINYUME CHAKE.​


Chukulia mfano wewe unataka kupika ugali, ukaenda kununua unga robo na wakati huo huo jikoni umebandika sufuria ya kilo kumi niambie hapa ugali utapatikana? Jibu ni hapana na inawezekana hata uji usipatikane pia, basi hivyo ndivyo ilivyo hata kwenye hizi nguvu, nilikuambia nguvu chanya inawakilisha nuru na nguvu hasi inawakilisha giza. Sasa ikitokea mtu wa nuru akaenda kutafuta mafanikio kwenye giza kinachotokea ni kwamba kama nuru itakua na nguvu kuliko giza basi nuru italifunika giza na yenyewe itaangaza na kama giza litakua na nguvu kuliko nuru basi giza litafunika nuru na lenyewe litatawala na endapo giza na nuru vyote vitakua na nguvu sawa, basi vitaweka hali ya kufifia fulani, yaani giza sio giza wala mwanga sio mwanga.

Na wakati huo huo, ili uweze kufanikiwa unatakiwa kunyanyua nguvu iliyopo ndani ya roho yako ili iweze kutoa mitetemo ya juu sana ambayo itapelekea uweze kuwasiliana moja kwa moja na huo ulimwengu wa kiroho pamoja na kufuata ile njia ielekeayo kwenye hatima yako, sasa ukiuchukua mwanga ukauongezea giza unachokifanya ni kufanya mwanga uendelee kufifia na si kuufanya uendelee kunyanyuka na ukichukua giza ukalipeleka kwa mwanga utakachokifanya ni kulifanya lififie na si kuliongezea mitetemo hasi na hii ndio hufanya watu hawa waweze kudidimia badala ya kunyanyuka pindi wanapofuata njia ambazo si ziwapasazo kupita.

Lakini mtu mwenye nguvu zenye uwiano katika usawa kwenye upande giza na nuru ukimpeleka kwenye njia za giza lile giza litaenda kufifiisha nuru na kuliongezea nguvu giza liliopo na kumfanya mtu huyu afanikiwe na ukimchukua ukampeleka kwenye nuru basi nuru itaenda kulidhoofisha giza na kuongeza nuru kwa nuru iliyopo na hapa pia utaona anafanikiwa kwa nguvu.

Najua unatamani uwe kwenye hii sifa ya kuwa na nguvu sawa ya nuru na giza lakini ukijiangalia si unaona unavyoteseka kiuchumi, sasa wenzio watu wenye hizo sifa hawateseki kiuchumi labda uwe haujawahi kwenda kwenye nyumba za ibada kabisa pamoja na kwa waganga ila kama unazosifa zote za watu wenye sifa hizi basi umasikini wako unatokana na uvivu wako wakutokutaka kutafuta ufumbuzi wa hali yako ya kiuchumi, au ni kwasababu hujajengewa misingi ya aina yoyote hapo awali, na hata sasa hujafanikiwa kunyanyua nguvu yoyote iliyopo ndani yako yaani kati ya hiyo nguvu hasi na nguvu chanya kwahiyo jitahidi unyanyue moja ila nakushauri sana unyanyue nguvu chanya ili uweze kuishi kwa kufuata sheria za ulimwengu kwani utafanikiwa zaidi.

Watu wenye nguvu hasi kwa wingi na nguvu chanya kidogo na hawa wenye nguvu hasi zilizobalance kiusawa na zile nguvu chanya huwa ndio wanaongoza kufanikiwa, kwasababu huwa kufungua siri za nguvu kwenye ulimwengu wa giza zipo moja kwa moja sana kuliko jinsi ya kufungua siri katika upande chanya yaani ulimwengu wa nuru. Elimu ya kiroho inayojihusisha na mambo ya upande wa giza, siri zake ziko wazi sana na ndio maana iko na wataalam wengi wanaoijua kwahiyo hii imefanya iwe rahisi kwa watu wa upande huo kuweza kupata msaada wa haraka pale wanapohitaji.

Pia hata masharti yake mengi sio yale ya kiroho ila ni yale yanayoonekana katika ulimwengu huu wa damu na nyama kwahiyo hii inafanya watu wengi wa upande huo wayafuate kwa uhakika kwa maana wanakua wanajua kwamba nikifanya hivi ni dhambi na nikifanya hivi si dhambi, wakati upande wa nuru masharti yake mengi ni yale ya rohoni kwahiyo unaweza ukafanya jambo usiwe na uhakika kama umevunja miiko au haujavunja, na ndio maana wengi huwa inawawia vigumu kujua kama wamejinajisi au laa. Na endapo utajua umejinajisi basi tiba yake inaenda kiroho pia, kwahiyo nayo huwa ni ngumu kujua kama umeshafunguliwa au bado, wakati wale wa gizani huwa wakijinajisi tiba zao nyingi ni zile zinazoonekana, kwamba waweza ukaambiwa tiba ya unajisi huu yafaa ulete damu ya kondoo au mnyama yoyote na ukishapeleka basi unafanyiwa dawa na unatoka ukiwa na uhakika wa kusafishika kwenye unajisi ule uliokua nao.

Ukitaka kufungua siri za upande wa nuru unaenda kwa shekhe au mchungaji au padre, na wote hawa watakupa njia tofauti tofauti lakini kubwa ya maombi, na kama tujuavyo ufunguzi wa mambo ya kiroho hautokei kama mtu anaetaka kufunguliwa akiwa hajaiweka roho yake katika hali ya utayari wa kupokea huo ufunguzi wenyewe, na utayari huu mara nyingi huwa unadhihirika kupitia imani, sasa ikitokea ukakosa imani basi mambo yote yatakayo kuwa yanatendeka itakua ni kazi bure, ila ikitokea ukawa na imani kubwa juu ya mambo haya ya kiroho na kuamini mafanikio kwanjia hiyo yanawezekana, basi ukifanikiwa kwa njia hiyo utaenda kuwa na ulinzi wa kutosha utokao kwenye ulimwengu huo wa kiroho. Au kuna wakati huwa inatokea kwamba, wewe ukawa na imani iliyo tukuka, ila ukakutana na watumishi wa Mungu ambao ni walaghai wale ambao hawana kipawa kinachoelekea kwenye hiyo hatima, ila kwakua wako na nguvu hasi zilizo katika uwiano sawa na chanya wakaamua kufoji hatima, basi hapa watakua wanakutia unajisi huku wakikuacha ukididimia kiuchumi.

Mwanzo nilikwambia mtu anaweza kugundua kipawa kitakachompeleka kwenye hatima yake bila ya kunyanyua nguvu za asili zilizomo ndani yake na akafanikiwa, lakini shida ni kwamba kugundua kipawa bila kuwa na ulinzi ni rahisi sana watu kukunajisi, nadhani umeona hapo juu, kwamba kuna watu wamezaliwa hapa duniani kwa lengo la kufanya uharibifu kwenye kila eneo, sasa na kitu kibaya zaidi hawa watu wanaopenda kufanya uharibifu ndio watu ambao huwa ni wakwanza kabisa kujua au kutambua kwamba mtu fulani tayari ameshaipata ile njia inayoenda kwenye hatima yake na muda mchache baadae ataenda kuwa mtu mwenye nguvu au mtu mkubwa sana hapa duniani kiasi cha kunizidi mimi kila kitu, sasa kwakua hawa watu huwa ni watu waliojawa na chuki pamoja na roho mbaya kwa haraka sana wanakunajisi au wanakuroga kama watu wengi walivyozoea kuita, sasa ili uweze kukwepa mitego yao basi unatakiwa ujiwekee ulinzi wa kiroho na ulinzi wa kiroho utaupata kwa kufuata kanuni na taratibu za ulimwengu katika upande huo wa kiroho na kanuni hizi pamoja na taratibu huwa zinapatikana sana kwenye nyumba za ibada.

Na sio hili tu, bali pia unatakiwa uwe mtu mnyenyekevu kwa Mungu wako pamoja na kwa ulimwengu unaoishi, kwasababu endapo utajisahau ni rahisi sana kutoka nje ya reli kwasababu nguvu chanya hazifungamani moja kwa moja na mambo ya kidunia kwahiyo pindi utakapofanikiwa kuziamsha unakua ni mtu mwenye nguvu sana lakini pia ili uendelee kulinda nguvu zako zisiingie kwenye uharibifu basi yakupasa uishi kulingana na matakwa ya imani yako.

Ukienda kinyume na mambo ya imani iliyotumika kuinyanyua hiyo nguvu chanya iliyopo ndani yako basi moja kwa moja utapoteza uelekeo kwa maana nguvu zako zitapungua na hapa unaweza usitetereke kifedha kwasababu bado utakua upo kwenye njia inayoelekea kwenye hatima yako lakini hapa wale watu wenye nia ovu wakitaka kukutia unajisi wanafanikiwa kwa haraka sana.

Nguvu zote za asili zilizopo ndani yetu huwa zinamiiko na miiko ya nguvu hizi huwa zinaanza kutekelezwa pale tu zinapoamshwa, na miiko yake mara nyingi ni kuhakikisha unatekeleza kanuni na taratibu za imani iliyotumika kuinyanyua hiyo nguvu iliyopo ndani yako, na hapa ndio utakuta kuna watu wamenyanyua nguvu zao hasi kupitia kwa waganga wenye uwezo wa kunyanyua nguvu hizo, na baada ya kuzinyanyua wanapewa masharti kadha wa kadha, unakuta mtu anaambiwa asinywe pombe kwa maana mizimu haimuhitaji kufanya hivyo au unakuta mtu anaambiwa atoe sadaka kila baada ya muda fulani na hapa sio sadaka ya damu tu, bali wapo ambao huambiwa watoe sadaka za kuwasaidia watu wenye uhitaji wa chakula mavazi na fedha, na wale waliopo kwenye nguvu chanya kama wamezifungua nguvu zao kupitia msikiti au kwa kupigwa dua na mashekhe ndio utakuta watu hawa wanaambiwa kila ikifika ijumaa hawatakiwi kufungua maduka na ni lazima waende kwenye ibada na kadhalika.

Kwahiyo endapo wewe ukishindwa kufuata hizo kanuni na taratibu za imani ya kiroho iliyotumika kuinyanyua nguvu iliyopo ndani yako, basi kuwa na hakika utajitia unajisi wewe mwenyewe na hii itaenda kufanya mwisho wako kuwa mbaya.

Licha ya utofauti huo ila kuna kitu hapa nataka nikwambie, ya kwamba wapo watu wenye nguvu chanya ambao waliwahi kupata changamoto za kifedha yaani baada ya kuanza kuiendea ile njia inayoelekea kwenye hatima yao huku wakiwa bado hawajafanikiwa kuinyanyua ile nguvu yao ya asili kwaajiri ya ulinzi walikutana na changamoto ya kufanyiwa unajisi yaani kurogwa, na baada ya kurogwa waliamua kwenda kwa wataalam wenye ujuzi na mambo ya kiroho lakini upande wa giza na wakafanikiwa kufunguliwa.

Sasa hii huwa inatokea hivi, kwamba wewe asili yako ni nuru ila nuru hii bado hujaifanya ichomoze ila umebahatika kujua hatima yako ya kuwa hapa duniani na umeanza kuifuata, wakati unaifuata hauna ulinzi na hapo akatokea mtu akakuwekea ukuta au giza katikati ya njia yako na hii hupelekea mito yote ya baraka ishindwe kupitisha maji kuja kwako na hapa ndio huwa watu wanasema nyota yako imechafuliwa, na ukienda kwa mtaalam mwenye ujuzi wa elimu hiyo ya mambo ya giza ambae ni mganga basi atakachofanya ni kuuondoa ule ukuta uliopo kwenye safari yako na wala haangaiki na wewe moja kwa moja, na akifanikiwa kuuondoa ndio pale sasa unakuta mambo yanarudi upya kama mwanzo yaani unafunguliwa, na hapa utasema yule mtaalam ni kiboko, wakati ki uhalisia yeye ni mtu wa giza kwa hiyo alichofanya ni kujihusisha na yale mambo ya giza ambayo yaliwekwa katikati ya safari yako, na wala si kujihusisha na wewe moja kwa moja.

Ubaya wa hiyo njia ni kwamba huwa inawafanya watu wengi wawe ni washirikina sana, kwasababu hawana ulinzi wa kiroho na waganga huwa hawawezi kuwapa ulinzi ili wakienda wasirogwe au kutiwa unajisi tena, na hii ndio huwa inapelekea kila wakienda kwenye maeneo yao ya kazi wanakaa kidogo wanawekewa uzibe tena kwenye zile njia zao, kwa hiyo watarudi tena kwa mganga na hii ndio inakua hivi maisha yao yote hasa kama hawatoshtuka mapema kutafuta namna ya kuinyanyua ile nguvu ya asili iliyopo ndani yao ili wapate ulinzi wa milele.

Pia kuna watu wengine ambao wanatokea upande huo huo wa nguvu chanya ila walishawahi kwenda kwa mganga na wakafanikiwa kutatua shida zao.

Hapa sasa nazungumzia yule mtu ambae hajanyanyua nguvu za asili zilizomo ndani yake na wala hajui hatima yake ni nini, kwa hiyo anapitia kipindi kigumu sana cha maisha ya utafutaji wa fedha, na anaamua aende kwa mganga ambae yeye ni mtaalam wa mambo ya gizani, lakini asili ya waganga wengi huwa hawasemi ukweli kwamba hawezi kukusaidia hasa unapoenda na shida inayohusiana na maswala ya umiliki wa fedha na mali, kwakua wanajua kila mtu katika majira fulani fulani kwenye mwaka ni lazima mto wa vipawa vyake unaoelekea kwenye ile hatima kuu lazima ufurike hadi kufikia zile kingo zake zipasuke na kuanza kusambaza hizo baraka maeneo mbalimbali na kipindi hiki ndio ambacho huwa ni cha bahati, kwani shida zote za kifedha ulizo nazo huwa zinapata ufumbuzi kwenye nyakati hizi, sasa mganga yeye atakachofanya ni kuendelea kukupa dawa huku akiendelea kukupangia tarehe kwamba katumie hii siku saba kama hujaona mafanikio urudi, na mambo yatakua hivi hadi siku moja utaona mafanikio kwa maana yale majira yako ya bahati yanapofika na yanakukuta unatumia dawa za mganga wako msanii, na wewe kwakua haujui unaamini kweli mganga ameweza kupata ufumbuzi wa tatizo lako wakati kiuhalisia hata ungekua umekaa ndani wakati wa majira hayo huwa fedha zinakufuata katika hali ya kushangaza sana na ambayo hujawahi itarajia.

Neno la kuchukua hapa ni kwamba usikubali kupumbazwa na haya mambo, kwa maana hayana muendelezo na yatazidi kukuchelewesha kwenye kufikia lile lengo kuu ambalo wewe umeumbwa uje ulitekeleze hapa duniani, kwa hiyo jitahidi kujitafuta kuanzia sasa ili uweze kujua kipawa chako ni kipi na uanze kukifuata ili ukaishi yale maisha ya hatima yako.

Na pia ningependa nieleweke kwamba, ninaposema imani za kiroho simaanishi kwamba ni lazima ziwe za kanisani, msikitini au kilingeni ila imani za kiroho zipo nyingi kwa maana ukienda India utakutana na watu wenye imani tofauti tofauti za kushangaza, pia ukienda China utakutana na imani nyingi za tofauti tofauti na za kushangaza na hata wewe kwenye ukoo wenu huwa mko na imani zenu tofauti tofauti na za kushangaza, kwahiyo hizi imani zote endapo zikifanikiwa kuamsha ile nguvu iliyopo ndani yako, basi jua nguvu yako ya asili uliyo nayo inafungamana moja kwa moja na imani hiyo kwahiyo unachotakiwa kufanya ni kufuata taratibu za hiyo imani na kama wewe nguvu uliyo nayo si ya upande huo utahangaika kwenye huo upande miaka na miaka ila hautafanikiwa kuinyanyua ile nguvu iliyoko ndani yako.

...Nitaishia hapa kwenye hiki kipande na tukutane kwenye kipande kinachofuata. Bado nitaendelea kuwepo hapa kwenye nguvu za asili kwa maana hii ndio brash kwenye kiatu ulichopaka kiwi na ndio clear kwenye gari ulilopaka rangi, ni mbolea kwa mazao yako shambani, pia ni maji kwenye kiu yako kwa maana kwamba kwa hatima pekee utafanikiwa ila kwa hatima jumlisha nguvu za asili utafanikiwa zaidi.
 
KIPANDE CHA ZIADA (BONUS).

Kuna kitu niliahidi kwamba nitakisema na nimeangalia katika mtiririko wa hii mada nikaona inakosa sehemu ya kuingia kwahiyo kwakua niliahidi nimeona sio mbaya niweke hiki kipande cha ziada ili nielezee kidogo kwanini watu wamekimbilia kwa Yesu na Muhammad huku wakiwa wameacha mizimu ya babu zao kule kijijini.

Sasa iko hivi kuna utofauti wa mitetemo ya mfumo nyota baina ya watu fulani na watu fulani na utofauti huu ndio ambao unaamua nani azaliwe kwenye ukoo upi na nani azaliwe kwenye ukoo upi bila kujali huo ukoo ni tajiri sana au maskini sana au ni wachawi sana au ni wacha Mungu sana ila kwakua mfumo nyota wako uko na muunganiko na watu wa ukoo huo basi kwenye ile probability ya roho gani ikazaliwe wapi basi kinachozingatiwa pale huwa ni mfanano wa mitetemo ya mfumo nyota na mimba ikitungwa na mtu wa familia hiyo basi roho mfanano katika mfumo nyota inaenda kuingia pale.

Kwahiyo wewe umezaliwa kwenye huo ukoo kwasababu mfumo nyota wako na watu wa ukoo huo unafanana.

Sasa kinachotokea ni nini? Ni kwamba kwakua mfumo nyota wenu unafanana basi hata mnapounganisha mitetemo yenu huwa inapokelewa na malaika wa aina moja.

Kwahiyo wale malaika ambao wako katika mfumo nyota wako na malaika ambao wako katika mfumo nyota wa mama yako na ndugu zako wengine huwa ni wa moja, kama mwanafunzi wa kozi hii na kozi ile ambavyo wanatofautiana kuwa na ma supervisor tofauti, au kama watu wa nchi hii na nchi ile wanavyotofautiana viongozi.

Na ndio maana unakuta kwenye ukoo wenu huwa mko na mila na desturi fulani ambazo huwa mnazifuata na zinawapa yale matokeo ambayo mnayataka ila mtu wa kabila au ukoo mwingine akija na akataka kufuata hizo mila na desturi zenu hafanikiwi.

Kuna watu kwenye koo zao wanayomizimu ya babu zao ambayo wanaifuata kiibada na wanafanikiwa kwayo ila mtu mwingine akienda kufanya ibada kwenye hiyo mizimu ambayo si ya asili yake basi anajikuta kuambulia patupu.

Mganga wa kienyeji anapotaka kukutibu huwa angaangalia tatizo lako kama ni tatizo la kawaida basi atakutibu kwa njia za kawaida ila kama tatizo lako linatokana na asili ya kwenu basi kuna mawili either akurudishe kwenye asili yenu au aangalie namna ya kujiungamanisha kiroho na mzimu wa kwenu na akifanikiwa basi atakupa tiba halafu atakupa na neno la kwenda kufanya kijijini kwenu, unakuta anakwambia uende ukafagilie kabuli la babu yako mzaa babu yako na kadhalika (wazee wa mambo ya asili hapa wananielewa vizuri sana)

Sasa Yesu alipokuja yeye alikuja kuukomboa ulimwengu, hajaja kuukomboa familia au ukoo fulani ila alikuja kuukomboa ulimwengu kwa ujumla.

Kwahiyo roho ambayo ilikua ndani ya Yesu Kristo ni roho ambayo mitetemo yake inapokea mawimbi ya watu wa duniani kote, kwahiyo roho zote za hapa duniani zikijiungamanisha kwa jina lake basi moja kwa moja mitetemo inafika hadi kwenye ile njia ya mfumo nyota ambao yeye yupo.(Hii ni sababu moja wapo ya kwanini baadhi ya watu huwa wanamuita Yesu ni Mungu)

Lakini hii sio sababu ya kwanini watu wanaacha mizimu ya babu zao na kufuata Yesu au Mtume Muhammad, ila sababu ni kwamba hawa watu ni watu ambao dunia au jamii ya watu wengi duniani ambao wanawafuata yaani wafuasi wao wanaamini ya kwamba hawa watu walifanikiwa kuziendea zile njia za hatima zao yaani yale mambo ambayo wameumbwa kuja kuyafanya hapa duniani kwa uadilifu mkubwa na wamefanikiwa kwa asilimia zote kuzifuata njia za hatima zao pamoja na kuishi maisha ya hatima zao, kwahiyo walisaidia kuongeza mitetemo chanya katika huu ulimwengu ambayo inaendelea kuufanya huu ulimwengu uendelee kuwa sehemu salama ya kuishi.

Lakini sasa mzimu au mizimu ya babu zako kule kijijini ni ngumu kujua kama kweli roho zao zilibeba hatima ya upande wa nuru au upande wa giza, kwa maana kama itakua ilibeba hatima za nuruni basi unakua uko salama ila kama ni zile za gizani unaweza kujishangaa unavaa maroho ya ajabu ambayo yatakusumbua maishani. Kwahiyo ili kuepusha hii probability na dhahma ya kubeba mzigo ya laana ya ukoo au familia watu wanaona bora waende kwenye huo upande ambao watu wengi wanathibitisha kwamba wahusika wake yaani Yesu na Muhammad walikua na hatima chanya kwahiyo ni wazi roho zao ziliuhishwa na kupata uzima wa milele.

Kwa wale ambao mnauhakika na asili zenu msiogope kuzifuata kwa maana ukijiungamanisha moja kwa moja na Yesu Kristo na ukajiungamanisha na malaika wa asili ambae yuko kwenye mitetemo ya mfumo nyota wako huwa majibu ya maombi yako yanawahi kurudi haraka kwa malaika wa asili yako kuliko kwa Yesu kwa sababu kwa Yesu kunahitaji watu walio na imani zilizo tukuka sana(hapa niko serious wala sikutanii kwa maana mfumo nyota wako umeunganishwa moja kwa moja na malaika wote wa asili yako na unapotaka kujiungamanisha kwa Yesu au Muhammad inamaana unajiungamanisha nao kwa jina, kwahiyo ukitaja jina basi ile mitetemo inaenda kuunga pale moja kwa moja ila kitu kikubwa hapa na cha msingi ni kwamba hapa imani lazima iwe ya kutosha sana)

Na kitu kingine kizuri kuhusu kujiungamanisha na malaika wa asili yako ni kwamba haijalishi imani yako iko vipi kwa maana si wewe ambae unaenda kupeleka hayo maombi ila wapo wateule kwenye hizi koo ambao ndio mnawaita wazee wa mila na hawa ndio huwa wamepewa hizo mamlaka na wanajua namna ya kukuunganisha na hao malaika wa asili yako, kwahiyo uwe unaamini watakuja au uwe hauamini watakuja.

Lakini sasa shida ya wateule wetu hawa wengine wakutusaidia kuunganisha mitetemo yetu ya mfumo nyota na Yesu au Muhammad huwa waliowengi si wateule halisi ila wanatumia hiyo njia kupata umiliki wa fedha na mali. Na watu wengi huwa wanauchezea huu upande kwasababu ni upande ambao unafungamana na dunia nzima kwahiyo hata yale madhara ya moja kwa moja kwa hawa wateule wa uongo huwa hayawapati kwasababu ukitaja tu jina ndio unajiungamanisha ila huwezi kufikia ile mitetemo kama imani yako iko chini na hautahukumiwa kisa imani yako iko chini au kisa hukufikia ile mitetemo kwahiyo kinachotokea waliowengi wanakuombea huku wakiyaunganisha maombi na mitetemo ya mfumo nyota ambao ile mitetemo ya Yesu ipo ila sasa imani zao ziko chini sana kwahiyo muunganiko hautokei wala na badala yake maombi hayo huwa ni sawa na kelele za bure tu.

Ila sasa kule kwenye wale malaika wa mifumo nyota ya koo na koo huwa wateule wa uongo hawapati nafasi sana kwa maana huwa ukikiuka miiko madhara yake yanatokea hapo hapo kwa maana huko hujiungamanishi kwa jina tu ila pia kwa mifumo maalumu iliyo wekwa ndio watu huita mila na mifumo hii huwa iko na taratibu zake pamoja na miiko kwahiyo zote huwa zinatakiwa kuzingatiwa na mteule asipozingatia basi lazima atalipia hapo hapo.

NB:
Kuna watu huwa wanasema Yesu na Muhammad si mababu zetu ni mababu wa Kiyahudi na Kiarabu kwahiyo tuache kuabudu mababu za watu ila nataka leo nikuambie tu hapa hatuabudu babu wa nani ila tunaabudu ile hatima ya kilimwengu ambayo ilibebwa ndani ya roho zao na baada ya roho hizo kuuhishwa ziliweza kutoa mitetemo yenye uwezo wa kupokea mawimbi kutoka kwenye kila mfumo nyota wa asili ya mtu na pia ukijiungamanisha kwa jina tu mitetemo yako inafika kwenye mfumo nyota ambao wao wapo moja kwa moja.
 
KIPANDE CHA PILI CHA NYONGEZA

Uumbaji wa ulimwengu huu ulikamilika baada ya Mungu kumuumba mwanadamu kwa mfano wake kwahiyo endapo Mungu asingemuumba mwanadamu kwa mfano wake basi hadi leo hii Mungu angekua anaendelea kufanya uumbaji.

Kwahiyo kitendo cha kumuumba binadamu kwa mfano wake inamaanisha kuna nguvu fulani za uumbaji na uanzishaji aliziweka ndani ya mwanadamu.

Kwahiyo hata wewe unazonguvu za uumbaji na uanzishaji ila nguvu hizi huwezi kuziona kwasababu zimefichwa kwenye upande wa asili yako yaani upande wako wa kiroho na wewe umetekwa na maisha ya kidunia kwahiyo unaishi zaidi maisha ya upande wako wa damu na nyama kuliko upande ule wa kiroho.

Nadhani niliwahi kukuambia mara nyingi kwamba mwanadamu yuko na pande kuu mbili yaani upande wa kiroho ambao ndio upande halisi wa mwanadamu na mambo yote ambayo yanampasa kuyafanya kwenye hii dunia ili aweze kutoa mchango wake wa kuongeza ile mitetemo chanya itakayoendelea kuifanya dunia iwe sehemu salama ya kuishi yapo, na upande wa pili ni huu wa damu na nyama upande ambao tunautumia kujiungamanisha na ulimwengu na ndio upande ambao tunautumia kushuhudia na kuishi maisha ambayo mengi yalikua ni hatima za watu wengine na ndio hayo ambayo yanatupumbaza hadi kusahau hatima zetu ni nini.

Na kwa maana hiyo basi kila kitu ambacho unakiona hapa duniani, ambacho kinapendwa na watu na unauhakika hiko kitu kipo hapa kwaajiri ya kuongeza mitetemo chanya na kusaidia kuifanya dunia iwe sehemu salama ya kuishi kuwa na uhakika kwamba kitu hiko kilizaliwa siku moja wakati mtu fulani anazaliwa yaani hiko kitu kiliwahi kuwa hatima ya mtu fulani.

Hapa namaanisha hivi, tuchukulie mfano mchezo wa mpira wa miguu ambao ndio mchezo unaoongoza kupendwa na watu wengi duniani kote, huu mchezo haukuumbwa na Mungu wakati anafanya uumbaji wa ulimwengu ila uliumbwa na Mungu baada ya kumuumba binadamu kwa maana ya kwamba mchezo huu hapo nyuma kidogo haukuwepo ila baadae ndio huu mchezo ulianza na ulianza baada ya mtu mmoja ambae alizaliwa akiwa na hatima ya mchezo huu ndani yake na yeye alipoanza kuiachia hatima yake kwa watu wa dunia na baada ya watu kuona jambo alisemalo linaleta maana basi wakaanza kuyafuata yale ambayo muanzilishi aliyasema na kuendeleza zaidi na zaidi hadi mchezo huu ukawa mchezo wa dunia nzima.

Simu unayotumia kusoma hili andiko ilizaliwa siku moja wakati mtu fulani ambae ndani yake alikua na hatima ya uanzilishi na uumbaji wa Simu alizaliwa.

Mitandao ya kijamii ambayo inakufanya uwe busy kila wakati ilizaliwa siku moja wakati mtu fulani ambae ndani yake alikua na hatima ya uanzishaji na uumbaji wa mitandao hiyo alizaliwa.

Hii platform ambayo mimi nimeweka hili andiko langu na wewe unalisoma ilizaliwa siku moja ambayo mtu fulani aliyekuwa na hatima ya uanzishaji na uumbaji wa platform hii alizaliwa.

Kwahiyo hii inamaanisha nini? Hii inamaanisha kwamba kwenye hii dunia kuna watu ambao wanazaliwa wakiwa na hatima mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwepo hapa duniani lakini pia kuna watu ambao wanabeba hatima za mambo ambayo yalishawahi au yanaendelea kufanyika duniani na hii yote ni kuendelea kuleta muendelezo na kuipa uhai hatima hiyo ambayo inaongeza mitetemo chanya kwenye ulimwengu na kuufanya uendelee kuwa sehemu salama ya kuishi.

Mungu hakuumba Dini ila aliumba dini baada ya kumuumba mtu, kwahiyo dini ya kikristo au ya kiislam zilizaliwa siku moja wakati mtu fulani na fulani wanazaliwa na walipozaliwa waliziendea zile njia za hatima zao kwa uadilifu mkubwa na kuishi kwa unyenyekevu kwenye hizo hatima zao.

Hatima nyingi mpya yaani zile ambazo hazijawahi kuwepo kabisa duniani huwa zinakuja kulingana na uhitaji wa ulimwengu kwa wakati huo na kwa kusema hivo basi kaa ukijua kwamba hakuna jambo lolote jipya linaloanza kwenye huu ulimwengu kibahati mbaya isipokua nyakati za hilo jambo kuanza zilikua tayari zimefika.

Na ukiona jambo lilianzishwa hapa duniani halafu ghafla likakosa watu wa kuliendeleza unatakiwa ujue kwamba jambo hilo ni labda lilikua haliongezi mitetemo chanya kwa dunia kwa maana lilikua si jambo lakimungu au lilitakiwa lije halafu lipotee mara moja yaani bila ya kuwa na muendelezo wowote.

Kwahiyo Mungu alimaliza kuumba hii dunia ila Mungu ndani ya wanadamu bado wataendelea kuumba hii dunia kutokana na mapungufu au mahitaji ya dunia kwa wakati husika na lengo ni kuendelea kuifanya dunia iwe ya kuvutia na sehemu salama ya kuishi.

Utofauti wa maendeleo baina ya nchi na nchi hii huonesha namna ambavyo watu huwajibika kuziendea hatima zao na ambavyo watu hawawajibiki kuziendea hatima zao kulingana na mifumo ya kielimu iliyopo ndani ya nchi husika.

Nchi ya China ni moja kati ya nchi ambazo zilitawaliwa na Japan na mjapani alipoondoka China aliwaacha watu wa Jamuhuri ya China katika hali mbaya sana ya kiuchumi kwa maana wajapan walikua wanahudumu katika maeneo yote nyeti yaani kuanzia hospital, jeshini kwenye mabank mashule na kadhalika kwahiyo walivyoondoka China walijikuta hawana wataalam wa kwao ila walikua wanatumia wataalam wa kijapan kwahiyo lile pengo likawa linaonekana hasa kwenye maeneo nyeti kama hospital na ndio hapa sasa Mao Tse Tung alipoamua kuwaacha watu wafanye kazi kulingana na vipawa vyao halisi na vipawa hivi ndio ambavyo vilianza kuwapeleka watu kwenye hatima zao na hapa ndipo wataalam wa mambo mbalimbali wakaanza kuzaliwa na nchi ikaanza kutengamaa kwenye kila eneo.

Kwahiyo Mao aliona hana muda wakuwachukua watu na kuanza kuwaandaa kimfumo yaani kuwatengeneza kwa kuwapa hatima tofauti na zile ambazo wao wanazo kama tufanyavyo huku kwenu na maeneo mengi duniani (hasa nchi za kiafrika), ila yeye aliona njia rahisi ni kuwauliza wao wenyewe waseme kwamba maeneo gani wao ni wazuri ambayo wanahisi wakipewa ujuzi wa awali watakua na uwezo wa kushika kwa haraka na kufanya kazi inayotakiwa, na nilikwambia hapo awali kwamba jambo lolote ambalo ni la hatima yako kulielewa huwa haihitaji nguvu nyingi kwahiyo mbinu hii ilifanikiwa kwasababu hiyo na hata wataalam ambao walipatikana hawakua wataalam wakubabaisha ila ni wale wataalam ambao walizaliwa kuja kufanya hiko wanachofanya yaani the choosen one, na hapa ndipo ambapo taifa la China lilifanikiwa kwasababu lilithamini na kuzipa nafasi hatima zilizomo ndani ya watu wake.

Kwanini nimekutolea huu mfano hapa? Nimekutolea huu mfano ili ujue kwamba yawezekana unaona mapungufu kadhaa kwenye hii dunia au kwenye nchi ambayo wewe upo, sasa yakupasa ujue kwamba hayo mapungufu ambayo unayaona yasingekuwepo kama kila mtu angeamua kutimiza wajibu wake wa kuzifuata na kuziishi zile njia na maisha ya hatima yake.

Kwahiyo hii mifumo ya kielimu ambayo tunayo si mifumo rafiki sana kwa maana inachangia kwa kiasi kikubwa kuwatengenezea watu hatima ambazo si hatima zao halisi, na hii ndio inapelekea wahitaji wa ajira kuwa wengi kuliko ajira zenyewe wakati kiasili sivyo ilivyotakiwa kuwa.

Na hapa nataka nikwambie hili jambo kwa uhakika mkubwa ya kwamba dunia haikupasa kuwa na upungufu wa ajira kwasababu si kila mtu duniani aliumbwa ili aje aajiriwe kwahiyo wako watu ambao hatima zao hazifungamani kabisa na upande huo wa kuajiriwa ila kwakua watu hutengenezwa yaani hufanywa kuwa marobot katika utendaji kwa maana mfumo ndio unaokuchagulia hatima yako na wala si wewe mwenyewe ingawa kuna wakati unaweza kuhisi ni wewe ndio ulichagua huo upande ila kiuhalisia wala si kweli bali umechagua huo upande kwakua umewahi kumuona mtu au kusoma au kuhadithiwa na wewe ukapata kuhamasika kuufuata huo upande na umejikuta unafuata hatima ambayo si yako.

Kwahiyo yawezekana kabisa kwenye hiko kiti ulichokalia hapo ofisini umekalia kiti ambacho alitakiwa kijana mwingine akikalie na wewe ulitakiwa uwe kwenye ofisi yako ukiwa umeajiri vijana wengine wengi tu, sasa uwepo wako hapo umefanya ushindwe kuiendea hatima yako na kushindwa kwako kufanya hivo kuna mitetemo chanya ambayo ilipaswa iongezwe na wewe inapungua na kupungua kwa mitetemo hiyo chanya kunapelekea baadhi ya familia kufa njaa kwasababu yako kwa maana hatima zao zilikua ni kutumika kwaajiri ya hatima yako yaani kuajiriwa na wewe kwahiyo ule muunganiko wa mitetemo chanya uliopaswa kuletwa na wewe inakosekana na kufanya njia ya kuzifikia hatima zao iwe ngumu kuonekana.

Najua ni ngumu kuamini kwasababu bado unatumia akili za kawaida ila nakuambia wakati utakapoamua kukaa katika hali ya utulivu wa akili na kuamua kuyaondoa yote ya ulimwengu huu na kunyanyua ile mitetemo yako ya kiroho hapo ndipo utakaponielewa na kujiona kwamba umechelewa sana kuyajua mambo haya.

Narudia tena, watu wengi wanaishi maisha ambayo mfumo umewatengeneza waishi na wao wakakubali kubaki hapo, lakini kuna watu hatima walizobeba ni kubwa kuliko taasisi au kampuni wanazozifanyia kazi ila ni vile tu mfumo umewapumbaza.

Nilikwambia kwamba watu ambao wamebeba hatima za kuajiriwa kwenye haya maofisi huwa hawapati tabu na wala hawatumii nguvu kabisa kwenye mambo ya shule hasa kwenye yale masomo ya upande ule ambao hatima zao zipo.

Sasa kuna watu ambao mfumo wa elimu uliwakataa kutokana na asili zao ila wao wakalazimisha mfumo uwakubali kivyovyote vile na kweli mfumo ukajitahidi kuwakubali ingawa kwa kuunga unga na watu wa namna hii ndio hawa ambao wanakalia viti ambavyo hawakustahili kuvikalia, wameamua kuzizima hatima zao halisi na kuziwasha hatima feki na wengi wa namna hii huwa hawana furaha na kazi walizo ajiriwa nazo, kwasababu kama hatima zao ni kubwa kuliko hizo nafasi wanazo zihudumu basi kikawaida viwango vyao vya umiliki vyapaswa kuwa vikubwa kwahiyo kutokana na hii sasa, mara zote mshahara wanaoupata unakua hautoshi kuwafanya waishi yale maisha ya hatima zao na hapa ndipo panapowafanya walalamike kila siku na hii hali huwafanya washindwe kuwa na furaha na kazi zao.

Lakini pia, kuna watu ambao hawakuwa vizuri shuleni na wakakubali matokeo kwamba mimi shule haipandi na badala yake unakuta wakaamua kujitafuta na kuupata ule upande ambao wao wako vizuri yaani ule upande ambao uliumbwa kwaajiri yao na ghafla unashangaa kuna taasisi au kampuni fulani inayofanya mambo yanayoendana na kile ambacho mtu huyu ambae shule hakuwa bora inamuona na haraka sana inampa ajira.

Mtu huyu anafurahi kwa maana anapata uhakika wa kupokea mshahara kila mwezi na ukizingatia shule hakuwa vizuri basi anaona hii ni bahati sana kwake na wale wanaomuajiri watamlipa mshahara mdogo kwa kisingizio cha kwamba hana vyeti na yeye wala haoji ila anasaini na kuanza kazi.

Sasa mshahara mdogo lakini anajibana hivo hivo na kwakua hana vyeti anakosa machaguo kwahiyo anafanya kwasababu anaamini hawezi kupata kazi popote.

Kwahiyo mtu wa namna hii kile alichokibeba ndani yake kisipokua na nguvu ya kuishinda ile nguvu ya kilimwengu anaweza akafanya kazi hiyo maisha yake yote hadi anazeeka.

Kwa maana watu wa namna hii huwa ni muhimu sana kwenye hizo taasisi zinazowaajiri ila huwa haziwaambii ukweli kwa maana wanataka waendelee kuwakandamiza ili wawatumie kwenye kutimiza hatima zao kama taasisi na ndio maana ni kawaida sana kuwaona watu wa namna hii wakifanya kazi kwenye taasisi moja kwa miaka mingi sana yaani watu wanaajiriwa wanafukuzwa ila wao wapo tu, na yote hii sio kama wanapendwa au wanaonewa huruma ila ni kutokana na vipawa vyao vinaisaidia sana hiyo taasisi.

Lakini mtu wa namna hii zile nguvu za kile alichokibeba ndani yake zikichanua kama zilivyochanua kwa mzee colonel sanders baada ya kuajiriwa kama mpishi kwa miaka mingi huku akiwa analipwa mshahara mdogo kuliko ile thamani anayoiongeza kwa taasisi hiyo, ila siku alivyokaa chini na kuanza kujitafakari na kuona kwamba licha ya kufanya kazi kwa miaka mingi lakini hakuwa na pesa inayoendana na nguvu alizozitumia kwa miaka yote hiyo hata walau japo robo au theluthi tu, uchungu ukamjaa na akajiona hana thamani hapa duniani hadi kufikia kujawa na mawazo ya kutaka kujiua lakini hatima yake ilikua na nguvu sana wakati huu na hapo hapo akajiuliza mimi ni nani (hapa alikua anataka kujua yupo duniani kufanya nini kwahiyo alitaka kujua hatima yake) na nini hasa nnachoweza kukifanya kwenye hii dunia ambacho watu wengi hawawezi kukifanya kama mimi (hapa alikua anatafuta kipawa ambacho atakitumia kama njia ya kumpeleka kwenye hatima yake).

Baada ya majadiliano ya muda ya mzee huyu, baina ya yeye na nafsi yake baadae lile swali la mimi ni nani likapata jibu kwamba mimi ni mpishi na upande ambao nauweza sana ni kukaanga kuku, kwenye huo upishi ni nini hasa ambacho naweza kukifanya vizuri zaidi kuliko watu wengi yaani kipawa changu ni nini na jibu lake likaja kuchanganya viungo mbalimbali vya mapishi kwa namna ya kipekee (kwa namna ya kipekee kwa maana alikua anajua kuchanganya viungo kwa namna tofauti tofauti na kwa kupitia kipawa hiki baadae akapata formula ya viungo ambayo wateja wake waliipenda na formula hii hakuna mtu yeyote aliyekua anaijua kwahiyo hii ikafanya ladha ya kuku anaokaanga na kuuza yeye iwe ya utofauti na kuku wengine wanaouzwa mtaani na hii ndio ilimpa utambulisho na kufanya watu waanze kutamani kujua formula yake ya ukaangaji wa kuku hao na hapa ndipo kipawa hiki kilivyotumika kumpeleka moja kwa moja kwenye maisha ya hatima yake).

Na mara tu baada ya kupata majibu ya maswali yake furaha na nguvu vikamrudia tena na moja kwa moja akaishika njia ya kuelekea kwenye hatima yake kwa uadilifu mkubwa na kweli baada ya kuifuata njia hiyo aliweza kukutana na bahati yake moja kwa moja kwa maana nilikwambia kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na ile nguvu ya umiliki wa fedha na Mali ambayo ilijificha kwenye hatima yake ikafunguka na hadi anakufa huyu mzee alikua ni billionaire huku akiacha migahawa yake ikifunguliwa maeneo mengi duniani na migahawa hii ndio hiyo ya KFC.

Sasa jiulize hiyo migahawa ya KFC imeajiri watu wangapi duniani kote? Je, huyu mzee angeendelea kubaki pale alipokua ameajiriwa unadhani familia zinazopata mahitaji yake ya muhimu kutokana na mishahara inayotoka kwenye migahawa hiyo zingekua vipi?

Kwahiyo hivi ndivo namna ambavyo hatima inavyosaidia kuongeza mitetemo chanya ambayo husaidia kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

Na kwenye stori hii jambo lingine kubwa ni kwamba huyu mzee alikua na hatima kubwa kuliko ile kampuni ambayo ilimuajiri hapo mwanzo kwa maana alibeba hatima ya kilimwengu na nnao uhakika huyu mzee baada ya kuona anaanza kupata mamlaka ya kumiliki fedha kwa kiasi ambacho hakukitarajia tena bila kutumia nguvu kubwa ambayo mwanzo alikua anaitumia kule alikokua anapika alijilaumu sana kwamba Kwanini hakuianza hiyo biashara mapema.

Sasa kuna watu wa aina ya huyu mzee wengi tu katika maeneo mbalimbali iwe ya ajira au hata huko mtaani wanaingia huku na kule wakijaribu kutafuta ila hawapati kwakua bado hawajakaa chini na kujiuliza maswali ambayo huyu mzee alijiuliza na alipopata majibu yake wala hakusubiri bali hapo hapo alichukua hatua.

Ila najua ingekua ni wewe ndio unajigundua hatima iliyomo ndani yako ni ya upishi na kipawa cha kukufikisha kwenye hatima hiyo ni kuchanganya changanya tu viungo wala usingeizingatia kwa maana ungejua haiwezi kukufikisha kokote kwakua ungeanza kujifananisha na watu wanaofanya hiyo biashara ila wako na maisha ya kawaida huku ukiwa umesahau kwamba hao wanaofanya hiyo biashara ni wanaifanya tu ila yawezekana si biashara ya hatima zao na ndio maana wako kawaida (watu wengi wenye vipawa fulani huwa wanayo kawaida ya kuvichukulia tu poa kwamba huwa wanaona ni jambo la kawaida kwa maana wanaamini mtu yeyote anaweza akawa nacho hiko kilichopo kwake, mfano hapo kwenye kuchanganya viungo mtu anaweza kuona ni jambo tu la kawaida ambalo kila mpishi anaweza kulifanya ila kiuhalisia ni kwamba haiko hivyo, kwahiyo usikichukulie poa hiko kipawa chako hata kama unawaona wengi wanacho kaa ukijua kwako kuna upekee ambao haupo kwa hao wengine).

Kwahiyo nikusisitize tu kwamba hata siku moja usije ukaidharau hatima yako wala kile kipawa ambacho utakitumia kuiendea hatima hiyo na wala usijifananishe na watu wengine ambao wanafanya hiko ambacho wewe unaamini ndio kitu ulichoumbwa kuja kukifanya hapa duniani kwa maana watu hujaribu kila biashara ila wengi biashara wanazozifanya si biashara za hatima zao na ndio maana ni kawaida sana kukuta biashara moja inayofanywa na watu watatu au wanne kwa njia zile zile ila kati ya hao wote utakuta mmoja ndio ambae anamafanikio makubwa kuliko wenzake.

Ukiuliza Kwanini watakuambia ni bahati, ndio hata mimi nakiri ni bahati kwasababu anachokifanya kimefungamana na yeye yaani ni biashara ya hatima yake na kwenye hatima yako ndiko bahati yako iliko siku zote.

Kumbuka wako wachezaji wengi wa mpira wa miguu lakini yupo Lionel Messi mmoja tu duniani, sasa ukifuatilia historia ya huyu jamaa katika ukuaji wake ingekua wewe ndio mzazi wake wala usingeweza kumruhusu kabisa afanye michezo ya ajabu ajabu na badala yake ungemlinda kama yai fulani hivi kwahiyo ungemlazimisha tu aende shule arudi nyumbani kwa maana yeye ni mbovu mbovu (kiTanzania Tanzania ndio anawekewa na kinembo chekundu kwenye shati lake la shule, kwa maana ya kwamba haruhusiwi kuchapwa, kufanya kazi za nguvu wala kushiriki katika shughuli zozote za kimichezo, Je, unauhakika huyo mtoto unaemlea hivo hatima yake imefungamana moja kwa moja na mambo ya kielimu? Usikute ni Messi au Mohammed Ali mwingine huyo ameletwa katika mfumo huo wa ubovu kama mnavyowaitaga).

Mtoto ni wako lakini kilichopo katika uhalisia wake yaani upande wake wa kiroho jua hakijatoka kwenye ulimwengu huu na hakijakaa ndani ya huyo mtoto kibahati mbaya, kwahiyo haijalishi hali yake ya kiafya ila kama unaona njia zake zimpasazo kupita ni hizo basi msimamie ili aweze kuziendea kama wazazi wa Lionel Messi walivyofanya na hapa sizungumzii mpira peke yake ila nazungumzia kwenye kila aina ya kipawa chenye hali au ukubwa unaoonekana kukinzana na mtoto au mtu husika.

Yupo kipofu mpiga ngoma na ala zingine za muziki, yupo mtu ambae hana miguu wala mikono ila ni public speaker wa kimataifa na yuko na team ya watu wengi ambao amewaajiri na anawalipa mishahara na watu hao wako na miguu pamoja na mikono yao timilifu, na wengi wanashangaa wakidhani ni jambo la ajabu lakini ni kwakua hawajui kwamba mtu halisi si hili umbo na shepu ionekanayo katika ulimwengu huu wa damu na nyama ila mtu halisi ni roho iliyomo ndani ya umbo hili linaloonekana.

Sasa hatima yako ni nini? Kwanini uko kwenye dunia hii? Ni kitu gani maalumu ambacho kimezaliwa siku ile ambayo wewe ulizaliwa ambacho chapaswa kufanyika ili kiweze kusaidia kuongeza mitetemo chanya ambayo itaongeza nuru na furaha kwa uso wa dunia na kuifanya iendelee kuwa sehemu salama ya kuishi? Nadhani ni wakati sasa wa kukaa katika hali ya utulivu wa akili na kuanza kujitafakari ili uhalisia wako uweze kujidhihirisha na mara tu utakapojidhihirisha chukua hatua ya haraka kuuendea kwa maana huwezi kujua ni muda gani wa ukomo ambao ulipewa kuja na kukifanya hiko kilichomo ndani mwako umebakia.

…Msomaji wangu, natamani niendelee kuandika zaidi na zaidi kwasababu ninayo mengi ya kuandika ila kwa leo wacha niishie hapa huku nikiendelea kuombea ile mitetemo ya juu sana iliyo katika mfumo nyota wako ikaimarike na kukuonesha njia zile zikupasazo kupita ili ukakutane na bahati yako pamoja na nguvu ya umiliki wa fedha na Mali na ukayaishi yale maisha ya ndoto zako hadi pale ukomo wako wa kuishi hapa duniani utakapofika huku kile ulichokifanya au kukianzisha kikiendelea kuongeza mitetemo chanya hapa duniani itakayopelekea roho yako ikapate kuuhishwa na kupata uzima wa milele.
 
Hivi

DNA kimwili au codes za mwili na
DNA za kiroho au code za roho

Zinatofauti Gani,
 
Mbegu za uzazi ,zinasiri Gani Katika hatima ya mtu,

Utakuwa, Kuna ule ushirikina wa,

Kuchukua mbegu za mtu kuzipereka Kwa mganya Ili kukombs Hatma au Nyota ya mtu au Kila kitu Cha mtu kinasambaratika kwenye maisha yake,

Mbegu ya uzazi au nywele za kichwani zote Zina DNA,

NAOMBA ufafanuzi kidogo, watu wanastawi Kwa kuiba mbegu, iyo ikoje
 
HIVI kimfani,

Mtu anataka kuimarisha uhusiano wa kiroho na yesu ,

Kiasi kwamba ,mtu aweze kuongea nae na kumuona kumshuhudia Kwa macho

Hio ikoje,

Na kingine,

Mtu kuweza kujifunza mambo ya kiroho mapya mbalimbali mwenyewe,

Inawwzekanaje
 
Thecoder somo hili linanikumbusha neno la mathayo 23:11
"Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu"
 
Hivi

DNA kimwili au codes za mwili na
DNA za kiroho au code za roho

Zinatofauti Gani,
DNA za kimwili ni kuonesha asili ya mtu na mtu kwa namna ya mwili yaani damu na nyama na DNA za kiroho ni kuonesha asili ya mtu na mtu kwa namna ya mfumo nyota na malaika shiriki.
 
Wataalam wa mambo ya kiroho katika upande huo wa giza huwa wanakua na uwezo tofauti na huwa wanakua na namna tofauti ya kufungua codes au kuzifunga.

Ila walio wengi huwa wanadeal sana na mambo ambayo yako na asili ya uhai ndani ya mtu kwamfano kucha, Nywele na manii ni vitu vilivyo na asili ya uhai.

Hii wacha niiandikie kipande Cha ziada nielezee kidogo kwahiyo vuta subra.
 
HIVI kimfani,

Mtu anataka kuimarisha uhusiano wa kiroho na yesu ,

Kiasi kwamba ,mtu aweze kuongea nae na kumuona kumshuhudia Kwa macho

Hio ikoje,

Na kingine,

Mtu kuweza kujifunza mambo ya kiroho mapya mbalimbali mwenyewe,

Inawwzekanaje
Uhusiano na upande wako wa kiroho ndio utakao kufanya uwe karibu na Yesu Ila kumuona kabisa ni hisia tu na wala mimi sina uhakika kama itawezekana kwasababu yesu ni roho hana mwili huu wa 3D kwahiyo kumuona ni ngumu ingawa Kwa hisia unaweza kumuona Ila siwezi kuthibitisha kwasababu sijawahi kushuhudia mimi au watu ambao wameleta ushahidi unaoeleweka.

Ila ukirejea mtume Mohammad namna ambavyo aliijenga lifestyle yake ya kukaa katika hali ya utulivu wa mara Kwa mara katika yale mapango ya Al nur na hali hii ikapelekea hadi kuonana moja Kwa moja na malaika Gabriel (Gibril) pale mapangoni na kumpa namna mpya ya maisha na ndio uislam ukazaliwa pale.

Kwahiyo ukiishi maisha ya upande wako wa kiroho huwa kunakua na illusions zinakujia mara Kwa mara na hisia ambazo mara nyingi huwa ni thabiti kabisa na utaanza kuona vitu Kwa namna ya tofauti ambayo watu wengi au wewe mwenyewe ulikua unaona hapo awali.

Na kuhusu kujifunza mambo haya ya kiroho unaweza ukajifunza Kwa kuanza kuishi maisha ya upande huo Kwa maana ukiujua upande wako wa kiroho ni rahisi kuujua upande wa mwingine Ila pia unaweza kujiunga na madarasa ya masomo ya siri ya kiroho naskia pia wanafundisha mambo ya namna hii ingawa mimi sijui sana Kwa maana sijawahi jiunga huko.
 
Thecoder somo hili linanikumbusha neno la mathayo 23:11
"Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu"
Kabisa mkuu... kwenye article ya pili au ya tatu kutoka sasa utauona huu mfano nimeuweka pale, pamoja na mifano kadhaa na nimejitahidi kujenga hoja kwa wepesi sana... tuendelee kuwa pamoja.
 
SEHEMU YA SITA.

kwahiyo tukiweka andiko kwenye usawa ni kwamba swala la umiliki wa fedha na mali linaweza kufunguliwa kwa kutumia maombi, dua au kilinge ila pia linaweza lisifunguliwe kwa njia hizo.

Kwa maana ya kwamba ufunguzi wa umiliki wa fedha na mali hufunguliwa kwa njia hizo pale tu ambapo mtu anaetaka kufunguliwa ameshaanza kuziendea zile njia za hatima yake ila wakati yupo kwenye hiyo safari aliweza kukutana na watu ambao wamemuwekea uzibe na mara nyingi watu wa hivi ni wale ambao bado hawajafanikiwa kuzinyanyua zile nguvu zao za asili.

Lakini endapo mtu atakua bado hajaanza kuziendea zile njia za hatima yake huwa hata akiombewa vipi au kupigwa dua vipi hawezi kupata ile nguvu anayoihitaji katika upande huo wa umiliki wa fedha na mali kwa maana maombi ya umiliki huwa hayamfuati mtu husika ila yanafuata hatima iliyomo ndani ya mtu, sasa kwakua wewe bado hujaanza kuifuata basi baraka zako zitaishia kwenye hatima yako na kuendelea kujaa katika upande huo kila wakati ambao utaomba kwaajiri ya umiliki wa fedha na mali.

Kwamaana hiyo basi kwa sasa nadhani kila mmoja anajua dalili ya awali ya kutambua mtu aliyeanza kuielekea hatima yake ila je, ni kwanamna gani unaweza kumtambua mtu ambae amefanikiwa kuinyanyua nguvu ya asili iliyomo ndani mwake? Sasa tusome hapa chini.

NAMNA YA KUMTAMBUA MTU AMBAE AMENYANYUA NGUVU ZA ASILI ZILIZOMO NDANI YAKE.​


Dalili ya kumtambua mtu ambae ameanza kuifuata njia ielekeayo kwenye hatima yake huwa ni kwanamna anavyofanikiwa kwenye mambo yake bila kutumia nguvu lakini watu hawa huwa hawana ulinzi wa kiroho kwahiyo endapo wakakutana na vikwazo kidogo katika njia zao ni rahisi kubadili muelekeo ilihali bado hawajafika popote, hapa ndio utaona mtu alikua anafanya biashara fulani na alikua anapata pesa sana lakini kwa hali ya kushangaza mtu huyu anapatwa na changamoto kidogo ambazo hazijulikani chanzo chake ni nini na zinaleta mvurugano kwenye biashara na ghafla mtu huyu anajikuta anafanya uamuzi wa kufunga biashara na haya yote huwa yanatokea kwa haraka sana.

Na baada ya kufunga biashara unakuta huyu mtu anakua anashinda tu kijiweni au ndani, huku akiwa hana wazo tena kuhusu ile biashara na hata wenzie au ndugu wakimuambia airudie ile biashara kwani ilikua inampa mafanikio sana huwa watu hawa wanaishia kucheka tu huku wakisema kwa wepesi nitairudia tu, na hizi ndio huwa kauli zao siku hadi siku.

Sasa watu wa namna hii ni kwamba walifanikiwa kuitambua njia inayoelekea kwenye hatima yao ila walichokua wamekosa ni kuamsha nguvu zilizopo ndani yao ili ziwapatie ulinzi katika hiyo safari ya kuelekea hatima wakati watakapokutana na changamoto watakapokua katikati ya hiyo safari yao.

Kwahiyo kazi kubwa ya nguvu yako ya asili ni ulinzi, lakini hii nguvu haikupatii pesa ikiwa peke yake ndio maana kuna watu ambao wameshainyanyua nguvu ya asili ambayo iko ndani yao ila wameshindwa kufanikiwa kwenye upande wa kifedha kwasababu bado hawajajua hatima ya wao kuwa hapa duniani ni ipi.

Watu hawa utawaona wanaenda kanisani kila siku au kama ni msikitini basi ni swala tano na ni kweli ni watu ambao hawarogeki na wachawi wanaogopa kuwasogelea, ila sasa shida yao ni kushindwa kuijua njia kuu inayoelekea kwenye hatima yao ili nao waweze kufanikiwa kwenye eneo la kiuchumi.

Kwahiyo kinachoweza kukupa fedha na mali ni kipawa kilichopo ndani ya hatima yako lakini nguvu yako ya asili ndio inayokupa ulinzi na kukuunganisha moja kwa moja na huu ulimwengu.

Kuna watu ambao huwa wanaanza kufika katika hatima bila kujua njia zilizowafikisha hapo, yaani mtu anajikuta tu kwamba yeye tayari anaanza kuitimiza hatima bila kufuata njia.

Najua inachanganya ila ngoja niiweke hivi ili unielewe vizuri hapa, yaani kama ni mtu tunasema labda alilala usingizi fofofo katika safari hadi anakuja kuamka anajikuta yupo ndani ya nyumba tayari, katika mtaa ambao yeye ni mgeni na mkoa au nchi ambayo hajawahi kufika, mtu huyu ukimuambia arudi alikotoka hawezi kufanikiwa kwasababu hajui njia ya kupita, kwahiyo atajikuta tu anatekeleza majukumu yaliyompeleka kwenye hilo eneo kwa kupitia msaada wa watu ambao atakua anawauliza njia wakati anapotaka kutoka kwenda kwenye majukumu yake.

Kwahiyo watu ambao huwa wanajikuta kwenye mazingira ya namna hii huwa wasipokua makini wanaweza wakaishi maisha yao yote ya hapa duniani wakiwa ni masikini wa kutupwa kuanzia wanazaliwa hadi wanaporudi kwenye ulimwengu wa juu.

Watu hawa wengi huwa wanaangukia kwenye eneo la kiroho, utakuta mtu ni kiongozi mkubwa sana wa mambo ya kiroho lakini maisha yake huwa yamejaa dhiki sana, na mara nyingi watu hawa huwa wanaishi kwa kutegemea misaada kutoka kwa watu wengine, unakuta kama ni mtu wa kanisa au msikiti basi anaishi kwa kutegemea sadaka na kimsingi sadaka huwa ni zakusaidia huduma ya kiroho na si kwaajiri ya matumizi binafsi ya mtu, na kama viongozi wengi wa kiroho wangefuata sheria hii basi wengi wao wangekua ni watu wenye maisha ya kawaida sana (hapa ndipo ambapo panapelekea viongozi wengi wa kiroho kujitia unajisi wao wenyewe bila kujijua).

Na hapa naomba nieleweke sana, sijamaanisha kwamba ukiwa kiongozi wa kiroho au dini kama mlivyozoa kuita ni lazima uwe masikini, ila nilichomaanisha wengi wanakua masikini kwasababu njia walizo pita ili kufika hapo walipo hawazijui, sasa ili waweze kufanikiwa basi ni lazima wa hakikishe wanazitafuta njia zote zinazozunguka hilo eneo ili waweze kuzitumia kwenye kupokelea baraka na neema za umiliki wa fedha na mali.

Au inabidi warudi nyuma kwanza, yaani watoke hapo kwenye hatima yao waanze kufuata njia ambazo ndio vipawa na wakishafanikiwa kuzifuata hizo njia kwa kurudi nyuma na kipindi watakapozijua sasa, ndio warudi tena kwenye eneo ambalo ukomo wa hatima zao lilipo.

Nadhani umeshawahi kusikia au kumuona mtu mmoja ambae mwanzo alikua ni muhubiri mzuri wa neno la Mungu lakini baada ya muda unaona tu ghafla ameacha kuhubiri na anafanya shughuli zingine ambazo zinamfanya awe bize na kushindwa kuifanya kazi ya hatima yake na ukimuuliza ni kwanini aliamua kuacha kuhubiri neno la Mungu atakuambia maisha yalikua magumu sana kwahiyo ameamua kutoka ili atafute pesa kwanza.

Lakini pia wapo watumishi wengine wa mafundisho haya ya kiroho ambao walijikuta wakiwa tayari wako kwenye eneo la mwisho wa hatima zao ila walichokifanya wao sio kurudi nyuma bali waliamua kuangalia zile njia zilizopo kwenye hilo eneo ili waweze kuona njia ipi kati ya zile zilizopo imebeba kipawa kilichopo ndani yao ili waweze kuitumia kupokelea baraka za umiliki wa mali na fedha na ndio hapa sasa utakuta mtu ni mchungaji au ni sheikh au ni mganga wa kienyeji mzuri ila pia yuko na kipawa cha uandishi wa vitabu basi anachofanya ni kufundisha hayo mafundisho ya kiroho lakini pia anaandika vitabu na kuviuza kwa waumini wake ili apokee zile baraka za umiliki.

Pia kuna wengine unakuta ni walimu wa mambo mbalimbali kwamba anatekeleza yale majukumu yake ya msingi aliyoletwa duniani kuyafanya lakini pia unakuta anakipawa cha kufundisha, wapo walio na vipawa vya kufundisha mambo ya uchumi, wapo wenye vipawa vya kufundisha madrasa, pia wapo walio na vipawa vya kufundisha mambo yahusuyo mahusiano na ndoa, pia wapo walio na vipawa vya kufundisha mambo yahusuyo uganga na uchawi, pia wapo wenye vipawa vya uimbaji pamoja na kufundisha watu kupiga ala mbalimbali za muziki, na kadhalika na kadhalika, kwahiyo kupitia hivi vipawa vyote hawa watu ndio wanavitumia kupokelea zile baraka za umiliki wa mali na fedha.

Na kwa mimi jinsi nionavyo nadhani njia hii ni bora sana (hasa kama itatumiwa kwa kuzingatia misingi na maadili ya imani husika na pasipo kuvuka mipaka yoyote ya imani hiyo ili kuepuka kujitia unajisi), kwa maana unatimiza majukumu ya hatima yako huku na wewe unaendelea kuzitumia zile njia zilizopo maeneo hayo kuendelea kupokea baraka za kumiliki mali na fedha, kuliko yule ambae yeye aliamua kuifuata njia kwa kurudi nyuma kwa maana atakaa huko aendako lakini lazima atalazimika kurudi tena ili ayatimize yale majukumu ya kimungu yaliyomleta hapa duniani.

Licha ya hayo ila pia kwenye kundi hili hili kuna watu ambao wao baada ya kujikuta tayari wapo kwenye eneo la mwisho la hatima zao, yaani eneo la utekelezaji, wao waliamua kuendelea na kazi ya utekelezaji na wala hawakujisumbua kurudi nyuma wala kuangalia njia zilizopo katika eneo hilo ili kuona ni ipi kati ya hizo wanaweza kuitumia kwaajiri ya kupokea baraka za umiliki wa mali na fedha, na hali hii ikawafanya wawe na maisha duni sana.

Nadhani umewahi kushuhudia au kusikia hadithi ya mganga mmoja ambae alisifika sana kwenye kuwapa watu nguvu za kiroho na kuwafanikisha kwenye umiliki wa mali na fedha lakini yeye anaishi kwenye kibanda cha nyasi. Sasa hawa ni mfano mzuri ya watu ambao wamejikuta wapo kwenye hatima zao pasipo kujua njia zilizowafikisha hapo ni zipi, watu hawa huwa wengi wameridhika na hayo maisha ya kusaidia watu wengine na wao wanaishi kwa kutegemea misaada kutoka kwa wale watu ambao wanawasaidia kiroho.

Kwa maana mara nyingi huduma zao huwa ni bure, sasa wale wanaowiwa kuwapa chochote kitu nao ndio hutumia hizo fedha kwaajiri ya kuendesha maisha. Na hapa nazungumzia wale waganga kweli kweli achana na hao matapeli ambao wametokea kwenye kundi lile la watu wenye nguvu hasi zilizo sawa na zile nguvu chanya ambao wameamua kuutumia upande wao hasi na kujiingiza kwenye mambo ya kiganga ili wajipatie fedha na mali, ila hapa nazungumzia waganga halisi.

Najua hapa kuna mtu mmoja anaetokea upande chanya anashangaa ninaposema waganga halisi, kwasababu yeye haamini kama wapo waganga wa kweli ila anachoamini waganga wote ni matapeli na hii ni kutokana na ile jaribu jaribu aliyowahi ifanya kwa waganga mbalimbali kushindwa kuzaa matunda, lakini nataka nikuhakikishie kwamba wewe hukufanikiwa kwasababu umebeba nguvu za asili ambazo hazifungamani na upande huo, kwahiyo kamwe haziwezi kuamshwa kupitia waganga ila wapo wenzio waliobeba nguvu za asili ambazo zinafungamana na upande huo na ndio maana huinuliwa kwa kupitia waganga, kwahiyo unachotakiwa kufanya ni kuendelea kubaki kwenye misingi ya imani yako lakini unachotakiwa kujua ni kwamba waganga halisi walio na nguvu za kiroho katika upande huo wapo.

Kamwe usije ukachanganya hivi vitu na kamwe usije ukawalaumu viongozi wa kiroho kwamba kwanini hawafanikiwi kifedha ili hali wao tayari mitetemo ya nguvu zao za asili ipo juu sana.

Kwahiyo dalili moja wapo ya kukujulisha kwamba mtu fulani amezinyanyua zile nguvu za kiroho zilizomo ndani yake ni kwamba hatetereki kwenye mambo anayoyafanya, watu watampiga vikumbo huku na huku ila yeye ataendelea kubaki imara na kama huyu mtu ni jirani yako kwenye maswala ya kibiashara basi unaweza kuhisi ni mchawi au freemason kwa maana nyota yake inakua inang'aa sana na hii upelekea kwenye biashara watu waanzie kwake kwanza kuulizia bidhaa fulani zikikosekana ndio wanakuja kwako (na hapa sasa nawazungumzia wale ambao tayari wamefanikiwa kunyanyua nguvu zao za kiroho lakini pia tayari wameweza kuzijua zile njia zinazokwenda kwenye hatima zao).

Pia ni watu ambao hawayumbishwi kiimani kirahisi na wanaishi kwa kufuata miiko ya imani zao kwa kadri zinavyowahitaji waishi. Pia kama nilivyosema hapo juu kwamba hawarogeki hawa watu na kama ni wale ambao wameanza kuamsha nguvu zao za asili kiroho kabla ya kugundua hatima zao huwa wanakua na bahati bahati sana kwasababu nyota zao huwa zinang'aa, ingawa kwenye upande wa kumiliki fedha na mali kwao inakua shida kwasababu bado hawajazijua njia za kupita kuelekea kwenye hatima zao.

Na licha ya kwamba wanakosa nguvu ya kumiliki lakini bado huwa hawayumbi kiimani kwahiyo kama ni kanisani utamuona anaenda kila siku huku akiwa na tumaini kuu la ipo siku moja na mimi Mungu atanionekania kwenye upande huu wa kumiliki fedha na mali, lakini ukweli ni kwamba watu hawa kufanikiwa kwao hutegemea zaidi msaada, labda kutoka kwa watu wa hatima zao au kutoka kwa viongozi wao wa dini wenye uelewa na mambo haya yanayohusu hatima, na ikitokea wakakosa msaada basi wataishi maisha yao yote katika hali hiyo hiyo ya kukosa nguvu za umiliki wa fedha na mali.

Kwahiyo hautakiwi kumlaumu mchungaji au shekhe wako ya kwamba mbona anakuombea kila siku lakini haufanikiwi kwenye upande wa fedha, mafanikio ya kumiliki fedha na mali hutegemea hatima na ili uweze kufikia hatima lazima uwe na kipawa, na ni kweli labda kipawa chako kinaweza kuonekana kwa njia ya maombi ila usipopewa msaada wa kukijengea misingi na kukuambia kwamba hiki ndio kikupasacho kufanya ili uende kwenye hatima yako hauwezi kufanikiwa, kwasababu wachungaji wengi au viongozi wa imani zingine wao wanachojua ni kuomba tu, na hii yote ni kwasababu wanaamini kila jambo linatatuliwa kwa maombi na lenyewe hujidhihirisha waziwazi, yaani ile kimiujiza ujiza, lakini kwa kadri wanavyoomba wanafanikiwa kuzinyanyua zile nguvu zako za asili kwasababu hizi zipo kwenye ulimwengu wa kiroho na huwa zinanyanyuka zikiwa kwenye ulimwengu wa kiroho.

Ila sasa pengine wakati huu wa maombi inawezekana hata kile kipawa chako ambacho kipo kwenye ulimwengu wa kiroho ila chenyewe ni lazima kivutwe kuja kwenye ulimwengu wa damu na nyama, kikajitokeza, lakini kwakua viongozi wengi wa kiroho huwa wanajihusisha sana na mambo yaliyo kwenye ulimwengu wa kiroho na hii huwafanya akili na hisia zao zipotelee huko kwahiyo kitu chochote kinachojitokeza hadhalani kwenye huu ulimwengu tuliopo huwa hawakizingatii sana.

Na ubaya wa vipawa huwa vinakuja kwa mtindo wa siri, sasa kinaweza kikaja ila ukashindwa kukitambua au unaweza ukakitambua ila ukawa hauko na uhakika kama ni chenyewe au si chenyewe, na ukikutana na kiongozi wa kiroho ambae hana elimu juu ya mambo ya hatima na vipawa basi atakachofanya yeye ni kuendelea kukuwekea mkono kichwani kukuombea ili kama ni chenyewe basi kijidhihirishe, lakini sasa unataka kijidhihirishe vipi wakati tayari kimeshajitokeza? Hapo kinachotakiwa ni kupewa muongozo na kusaidiwa kukijengea misingi ili uanze kuishi maisha ya kuelekea kwenye hatima yako.

Watu wengi wa kwenye makanisa ya kiroho huwa wanaingia sana kwenye mtego wa kufuata vipawa ambavyo si vipawa vyao halisi bali ni vipawa ambavyo wamejifunza kutokana na mtindo wao wa maisha ya kikanisa kanisa, kwa maana mtindo wa makanisa mengi ya kiroho ni kusoma neno la Mungu, kuhubiri, pamoja na kuimba kwenye vikundi vya kwaya vilivyopo kanisani, sasa huu mtindo huwa ni mtindo endelevu kwahiyo kuna vijana ambao kwakua kila siku wanauona mtindo huu wa maisha ya kanisa basi nao hujikuta wakitamani kuwa kama muimbaji fulani au mchungaji fulani, na hii hali huwapelekea vijana hawa kuhisi ndio vipawa vyao halisi wakati ukiwachunguza kiundani unaona si vipawa vyao bali ni vipawa walivyojifunza kutokana na mtindo wa maisha waliouzoea, na vimeenda kuziba vile vipawa vyao halisi walivyoumbwa kuja kuvipita kuelekea kwenye safari za hatima zao.

Kuna wengine hujikuta kabisa wanahisi wako na vipawa vya kichungaji na kweli watapambana hadi watafika kwenye huo upande ila ndio hawa ambao wakioata nafasi ya kufika huko, huwa wanafanya mambo ya ajabu yale ambayo yako nje ya miiko ya uchungaji na mwishowe wanajikuta wakijinajisi wao wenyewe kwa hali ya kujua au kutokujua.

Na hapa nisisitize tena, kwamba tujitahidi sana kusikiliza sauti za ndani ya mioyo yetu lakini tukiwa katika hali ya umakini sana kwa maana hizi sauti ndio ambazo hutokea kwenye ulimwengu wa kiroho na mara nyingi huwa hatima zetu tunaanza kuzijulia huko ila hakikisha sauti unayoisikia ndani yako sio ile sauti ambayo umeipandikiza mwenyewe kutokana na mtindo wa maisha fulani ambayo yamefanya ujifunze na kutamani kuwa na aina hiyo ya kipawa, pambana sana uweze kujua hatima ya wewe kuwa hapa duniani ni nini ili uweze kuibua hiko kipawa kitakachokupeleka moja kwa moja hadi kwenye hatima hiyo uliyoumbwa kwayo.

HATARI YA KUIFUATA NJIA IELEKEAYO KATIKA HATIMA YAKO KABLA YA KUFUNGUA NGUVU YAKO YA ASILI.​


Dunia ni uwanja wa vita za hatima kwahiyo wakati wewe unapambana kwenye kuijua hatima yako hapa duniani ili uweze kuitimiza pia yupo mwenzako nae anafanya hivyo hivyo, na nilikwambia kuna watu ambao wamebeba hatima za kimungu na kuna watu ambao wamebeba hatima za kishetani na hawa wote wanapambana kuzitimiza hatima zao kulingana na namna ile inayofaa.

Vita hii ni kubwa sana na ni vita ambayo hupiganwa kwenye ulimwengu wa kiroho sasa wewe yawezekana umeshaipata au kuiona ile njia inayoelekea kwenye hatima yako lakini huendi kanisani,msikitini wala kilingeni au kwenye imani yoyote ambayo unaiamini kwasababu tu unajiona umeshafanikiwa kiuchumi lakini nikuambie tu mafanikio yako yanakua si ya uhakika kwasababu wakati wewe unatembea kuifuata njia inayoenda kwenye hatima yako kuna watu wanakuja nyuma yako wakiwa na gari zao na wako kasi sana ila mbele yao wanakuona wewe umewazibia njia, sasa na kama ujuavyo hii ni vita kwahiyo hakuna namna watakuacha salama zaidi ya kukugonga na wakisha kugonga ndio huwa tunasema umetumika kuitimiza hatima ya mtu mwingine na mtu mwenyewe ni huyo ambae amekugonga.

Na nikuambie tu kwamba wapo watu wengi duniani ambao wanatumika kutimiza hatima za watu wengine, na kwenye hapa kwenye kutumika kutekeleza hatima za watu wengine huwa kuna namna kuu mbili za kutumika.

Kuna ile namna chanya ya kutumika na mtu ili aweze kufanikisha hatima yake kwa mfano shabiki wa msanii fulani kwa maana kila wimbo wake anaoutoa wewe lazima uuskilize basi pale huyo msanii anakutumia wewe ili yeye aweze kutumika hatima yake, pia hapa tulipo yaani kwenye hii platform ni kwamba wewe na mimi tunatumika ili kumsaidia mtengenezaji wa platform hii aweze kutimiza hatima yake, hata wewe unaposoma hili andiko langu pengine unanisaidia mimi ili niweze kutimiza hatima yangu ya kufikisha huu ujumbe kwa jamii ili mitetemo chanya iweze kuongezeka.

Lakini pia ipo namna has ya kutumika na watu ili waweze kutimiza hatima zao, yaani unakuta mtu anataka utajiri na ameenda kwa mganga na mganga akamwambia ili afanikiwe lazima amtoe kafara ndugu yake fulani kwani yeye ndiye atakaemsaidia kwenye kumpa mwanga wa kumulikia njia yake inayoelekea kwenye hatima iliyomleta duniani, sasa huyu ndugu yake asipokua na nguvu za kiroho basi atatolewa kafara na moja kwa moja anakua ametumika katika kuitimiza hatima ya ndugu yake.(watu wengi ambao wanatumia njia hii ni wale ambao wanafoji hatima, kwa maana ya kwamba wao hawakufanikiwa kuzijua hatima zao au wao kwenye biashara wanazofanya haziendani na wao kwahiyo wanapoenda kwa wataalam wa kiroho wa upande huo wa giza huwa hawana muda wa kuwaambia kwamba biashara wafanyazo haziendani na wao au hawana hiyo elimu ila badala yake wanaangalia kwenye circle ya mtu anaetaka huo umiliki wa fedha na Mali kupitia biashara hiyo na kama wataona mtu ambae anafungamana moja kwa moja na hiyo biashara ndio wanamchukua na kuanza kumtumikisha ili kuweza kufanikisha hatima zao na hapa ndio tunasema huyo aliyemuua mwenzie amefoji hatima)

Wapo watu ambao hatima zao kubwa ni kuwa madaktari wakubwa wa kufanya majaribio ya kutengeneza magonjwa mbalimbali, na mara nyingi magonjwa haya mengi huwa ni mapya kabisa hapa duniani, sasa wanapoyatengeneza huwa yanakosa tiba ya moja kwa moja na magonjwa haya yanapoachiwa huwa yanaua watu wengi sana kwahiyo watu wengi wanaokufa kupitia hayo magonjwa tunasema wametumika kwenye kutimiza hatima ya huyo aliyetengeneza huo ugonjwa.

Kuna watu bado ni kina Sauli hawajawa kina Paulo, kwahiyo kazi yao ni kuhakikisha wanaiendea hatima yao kwa kutumia nguvu na watu hawa wanatafuta roho za watu wengi ambao wako dhaifu ili wazitumie kama chambo, na unapoingia kwenye kumi na nane zao basi utatumika moja kwa moja kwenye kutimiza hatima zao.

Na ukifa kwaajiri ya kutimiza hatima ya mtu mwingine haimaanishi unaenda mbinguni, hapana, utaendelea kubaki katika ulimwengu wa kiroho upande wa giza na utatumiwa huko kwa namna wanavyotaka wao hadi muda wako halisi wa wewe kuwa hapa duniani utakapofika ndio roho yako itarudi kwenye ulimwengu wa juu. Damu ya Abel ndio ambayo iliskika ikilia kule mbinguni lakini roho yake haikwenda, kwahiyo Kaini aliendelea kuitumia roho ya nduguye kwa namna vile alivyokua anataka yeye.(hapa tunasema miaka yako imechukuliwa mateka yaani inatumikishwa kuzimu na nikuambie tu kwamba miaka kutumikishwa si tu kwa wale ambao wametolewa kafara za kufa ila pia kuna watu wako hai ila bado miaka yao inatumikishwa kuzimu, nikipata wasaa nitawaletea andiko la kuelezea hii inatokeaje ili uweze kujipima ujue kama unaishi miaka yako ipasavyo au tayari miaka yako iko kule kuzimu inatumikishwa?)

Kwahiyo utaona jinsi vita za hatima zilivyokua kubwa na mbaya na ndio ambazo zimefanya dunia iwe kama ilivyo hii leo, kwahiyo dunia haihitaji watu dhaifu bali inahitaji watu wenye nguvu, na nikisema nguvu simaanishi kwamba unatakiwa uende gym ukatengeneze misuli mingi kwenye mwili wako, hapana, ila namaanisha nguvu za kiroho na nguvu za kiroho huwa hazipatikani tu kwa kupuuzia nyumba za ibada kwani kwa kufanya hivyo utakua umevunja miiko ya imani na kikawaida kwenye kila imani huwa kuna miiko yake sasa ili uweze kudumu na kufanikiwa kwenye upande huo wa kutengeneza nguvu za kiroho hatua ya kwanza ni kuishi kwenye misingi na taratibu za imani ambayo wewe unaifuata.

Usikubali hata siku moja kutumika kwenye kutimiza hatima ya mtu mwingine, kwahiyo jitahidi sana uweze kuinyanyua ile nguvu ya asili ambayo iko ndani yako kisha ufanye juu chini uweze kuijua hatima ya wewe kuwa hapa duniani ni ipi na uanze kuifuata, kwa kufanya hivi utaishi maisha yasiyo na mashaka kwani na wewe utaingia kwenye lile kundi la watu wachache ambao wanauendesha mfumo wa dunia kwa namna ile wanayotaka wao na hapa ndipo utakapolitimiza lile neno la kuumbwa kwaajiri ya kuutawala ulimwengu kwasababu utakua na nguvu za kufanya hivyo.

Kwahiyo kwangu mimi kati ya mtu ambae ameanza kugundua njia ielekeayo kwenye hatima yake lakini hataki kunyanyua nguvu ya asili iliyopo ndani yake ili apate ulinzi, na yule ambae ameanza kwa kunyanyua nguvu ya asili iliyomo ndani yake huwa naona aliyebora zaidi ni huyu aliyenyanyua nguvu yake ya asili kwani huyu anakua na nguvu zitakazo muweka mbali na unajisi wa aina yoyote, na kamwe hawezi kutumika kutimiza hatima za watu wengine katika ulimwengu wa kiroho ingawa hali yake ya uchumi inakua hairidhishi sana.

Ila hao wengine ambao wameanza kuzifuata hatima zao kabla ya kunyanyua nguvu huwa hata nikiwaona nawaonea huruma kwa maana naelewa hawana safari ndefu sana, kwasababu nguvu yoyote ambayo inaibuka hapa duniani huwa inaanza kuonekana kwenye ulimwengu wa kiroho, kwahiyo wale waliopo kwenye upande wa giza wakipata taarifa kwamba kuna kijana anakuja kwa kasi hapo kariakoo, yaani tayari ameshaanza kuielekea ile njia ya hatima yake, na uwepo wake hapo utafanya sisi wengine tusiuze kwanza hadi yeye atakapomaliza mzigo wote kwenye store yake, hapa ni lazima wakushughulikie, na wakiona nyota yako inafaa kuamsha mwanga kwenye hatima zao basi wanakutoa kafara ila wakikuona hufai ndio vile wanakubadili uelekeo na utashangaa unarudi kwenye umasikini wako.

Kwahiyo ili twende na tuweze kufika kwenye hatima zetu, lazima tuweze kubalance mambo, kwamba tukishagundua njia zielekeazo kwenye hatima zetu ndio tunapaswa kuwa watu wenye bidii sana kwenye masuala ya imani, tena tusifanye mambo haya ilimradi ilimradi tu, bali tuyafanye kwa mioyo yetu yote, na ndio iwe mtindo wa maisha yetu kwa maana hii ndio njia pekee ya kujikinga na wale mafedhuri watia najisi watu, na wale ambao wamebeba hatima za upande wa giza ambako ili waweze kuzitimiza hatima zao ni lazima wawatumie watu wengine ili wawafanikishie hazima zao.

Na kamwe usikubali kabisa mtu akuyumbishe kiimani kwani ukiona mtu anafanya hivyo inabidi uanze kumchunguza, kwani inawezekana yeye alichobeba ndani yake ni cha upande wa giza kwahiyo anakuona unaenda kuwa na nguvu na yeye anahitaji wewe uwe dhaifu ili akutumie kwenye kutimiza hatima yake, narudia tena kwa msisitizo, mtu yeyote anaetaka akupunguze nguvu lazima afanye juu chini aiyumbishe imani yako kwenye mambo ya kiroho, sasa na wewe ukikubali kuingia kwenye mfumo moja kwa moja anakumaliza.

Nikutie moyo wewe ambae unasali sana usishangae kwanini licha ya kusali kwako sana ila bado unateseka kiuchumi wakati kuna jirani yako au ndugu yako au rafiki yako yeye maswala ya kusali wala hayajui lakini kwenye upande wa kiuchumi ni amefanikiwa sana, nadhani hapa unaelewa kwamba inawezekana mtu huyo ni wa upande ule wa giza kwahiyo ameenda kwa babu yake akamfungua au inawezekana ni wa upande huo wako ila yeye amekua na kiburi kwasababu amepata bahati ya kuanza kuijua hatima yake kwahiyo ameipata njia inayoelekea huko na sasa hivi hataki kabisa kusikia kuhusu maswala ya kanisa au msikiti kwakua elimu ya mambo haya ya kiroho hana ila angekua nayo angekimbia kwa kasi sana ili aje kuinyanyua nguvu ya asili iliyomo ndani yake kwaajiri ya ulinzi wa milele.

Najua walio wengi huwa wanasema, kama kufa kila mtu atakufa, ni kweli kila mtu atakufa lakini sisi watu wa imani za rohoni tunasema unaokufa ni mwili wa damu na nyama ila roho kamwe haifi (na huu ndio ukweli halisi, bila kujali kama utakubaliana na mimi au utakataa, lakini ukweli hautobadilika kamwe) sasa ili uweze kuwa hai kiroho na uende katika kiwango kingine cha maisha unatakiwa ufe wakati ambao muda wa ukomo uliopangiwa kutimiza hatima yako uliyotumwa kuja kuifanya hapa duniani unapofikia tamati, ila ukifa kwaajiri ya kutimiza hatima ya mtu mwingine utaendelea kurandaranda tu hapa duniani ingawa ndugu zako hawatokuona ila roho yako haitatoka hapa hadi ule muda ambao ulipangiwa uwepo hapa duniani utakapofika, kwahiyo kama ulipangiwa uishi miaka sabini halafu ikatokea kuna jamaa akaamua kukutumia wewe ili atimize hatima yake ukiwa na miaka 25, basi kuwa na uhakika utaishi maisha yote ya miaka 45 ukiwa unaranda randa humu humu duniani ila katika ulimwengu wa giza na huko utakua mtumwa utakaetesaka siku zote.

… Kwa leo wacha niishie hapa, ila endelea kuwa hapa kwa maana bado kidogo namalizia hili andiko kwahiyo tumeanza pamoja wacha tumalize pamoja.
 
mkuu Thecoder hivi hawa wanaobet unasema vp maana wanacheza kila siku hasa football lakini mikeka inachanika ila hawaachi..hivi hawa nao wanafosi hatima au hatima zao haziko kwenye kubashiri mpira au labda wanaweza kubashiri michezo mingine kama kikapu,tennis na mingine mingi tu yaani nje ya mpira na wakashinda pesa kila siku ila. ndoivo umeung'ang'ania mpira maana nausoma uzi wao wa mikeka kule sport naonaga vilio vingi wanakula za uso wanahasira hao..sasa hii sekta ya ubashiri mikeka imekaa vp ile kihatima hatma na kipawa au nii watu aina gani inawafaa wenye hatma zipi au kuhusiana na betting ili uweze kula mipesa ile kiuhakika.?
 
Michezo ya kubashiri ni ya bahati na sibu na kwenye hii bahati na sibu huwa inawaangukia wale wenye hatima linganifu na mchezo wenyewe lakini pia kuna nyakati za mafuriko ya baraka katika mto wa hatima ya mtu na nyakati hizi ndio zile ambazo watu hupata ufumbuzi wa maswala yote yanayohusiana na fedha na katika nyakati hizi watu hupata pesa kinamna tofauti tofauti ambazo wao hawakuzitarajia kwa hiyo hata yule ambae hana hatima linganifu katika hizi nyakati huwa anaouwezo wa kupata pesa kupitia njia hiyo kwa maana nyakati za mafuriko huwa ni nyakati za bahati ya kifedha.

Lakini ukiangalia hatima linganifu zinazofungamana na maswala hayo ya betting ni burudani hasa katika upande huo wa mpira wa miguu.

Lakini pia hatima nyingine inayoweza kuingia hapa ni hatima ya ile ya maono na utabili hizi ni hatima ambazo zimejificha ndani ya baadhi ya watu ila kuna nyakati huwa zinakuja kwa namna ambayo hata wausika hawajui na watu wa namna hii huwa wengi wao hawajui hata hii michezo ila ukiwa nae karibu utakuta tu anakuambia hapo huyu atashinda huyu anatoa sare huyu atafungwa na unakuta baada ya muda wa hiyo michezo kupita mambo huwa kama vile alivyokua amesema yeye (hii hali huwa inatokea kwenye nyakati fulani na wala si hali ambayo inakuwa ndani ya mtu huyu kila siku ila akitaka iwe ndani yake kila siku basi lazima aanze kubyanyua mitetemo ya upande wake wa kiroho na hili ndio kundi lenye uwezo wa kushinda zaidi kuliko hayo makundi mawili hapo juu).
 
Thecoder katika jibu lako hili nimepata swali lingine ni kuhusu "mafuriko ya baraka katika mto wa hatima"ambapo watu kupata bahati za kifedha hata pasipotarajia japo si wengi wanatambua hili maana wengi wetu tukio hili la kufurika neema kwenye mto wa baraka wa hatima linapita tu pasipokutambua tunaona tumepata zali tu pasipo kujua kama ndio hatima hiyo..sasa swali ni je,ukiwa umejua mto wa hatima umefurika sasa utumie vp nafasi hiyo kutengeneza fedha.? swali la pili je, hiyo kufurika mto hatima inatokea kila baada ya mda gani je,kuna saa katika masaa 24 au mara moja kwa mwezi je kuna tarehe rasmi? au ni mara moja kwa mwaka ni mwezi upi? na inadumu siku ngapi huko kujaa mto wa hatima.? maswali yote haya ni kujiweka tayari kwamba mafuriko yajayo hayakupiti lazima uwin maswala ya kifedha.! au hayo mafuriko ya kujaa mito ya hatima yako ndio ya kubahatisha tu na kuhisi pasipo kalenda rasmi.?
 
Nasubiri Muendelezo,

Naitaji utuelezee,
Mafuriko ya Mito ya baraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…