Dunia ni uwanja wa vita za hatima

Dunia ni uwanja wa vita za hatima

SEHEMU YA SABA.

Tuliona sababu moja ya watu kufa ambayo ni kufa kwaajiri ya kwenda kutimiza hatima za watu wengine na hii ipo maeneo kadhaa kwenye biblia kwa mfano utaangalia lile tukio la Kaini na Abel jinsi ambayo Kain aliamua kumtumia ndugu yake ili aweze kuitimiza ile hatima yake ya ukuu.

Lakini ukiachana na sababu hii ya kufa kwaajiri ya kutimiza hatima ya mtu mwingine ila pia watu hufa kwasababu muda ambao walipangiwa kuwa hapa duniani umefikia tamati yaani ile deadline inakua imefika kwa maana nilikwambia sisi wote hapa duniani ni wageni na tupo hapa kwa lengo maalumu ambalo lipo ndani ya kila mmoja wetu na ukubwa wa lile lengo kuu au ile task ambayo imfenya mtu na mtu awe hapa ndio hasa ambayo inatoa utofauti wa muda wa mtu kuwa hapa, kwamfano kuna watu ambao wamebeba hatima ngumu na kubwa katika utekelezaji hawa huwa hata miaka yao ya kuishi huwa inakua mingi kidogo kuliko wale ambao wamebeba hatima nyepesi na rahisi katika kuzitekeleza. Na hawa ndio wale ambao mnasema wamekula chumvi nyingi kwahiyo wameishi maisha ya kumpendeza Mungu ila kiuhalisia kwenye hiko kipengele cha kumpendeza Mungu inawezekana kikawa hakikutimizwa na watu wa namna hii ila ni vile waliishi katika maisha ya kawaida ya kidunia kwa maana ili uishi kwa kumpendeza Mungu ni lazima uishi yale maisha ya hatima yako yaani utimize lile lengo kuu ambalo Mungu alikiweka ndani yako wakati uumbaji wako unafanyika.

Pia sababu ya tatu ya kwanini watu hufa ni kuvuka mipaka ya yale ambayo walipangiwa kuyafanya lakini wao walipofika hapa ule upande wao wa kiroho ukawa umefunguka zaidi na kujikuta wanafanya mambo makubwa ya kihatima hadi kuzidi yale ambayo walitakiwa wayafanye, ili kunusuru roho za namna hii ili zisipate uharibifu huwa zinachukuliwa kabla ya ile deadline haijafika. Na hawa ni wale ambao huwa mnasema kwamba wamekufa kwasababu wamemkufuru Mungu.

Pia sababu ya nne kuu ya kwanini watu hufa ni ile sababu ya kutimiza hatima iliyo ndani yako mapema kuliko ule muda ambao ulikadiriwa kisha ghafla ukaanza kutoka nje ya lengo, kwa maana kwamba unaanza kufanya mambo ambayo yako nje ya miiko ya hatima yako kwa mfano unakuta mtu anatoa huduma fulani ya kiroho ambayo haikutakiwa itolewe kwa njia ya pesa ila yeye baada ya kuona watu hufanikiwa sana kupitia huduma yake na ghafla anaanza kutoa huduma kwa pesa na pasipo pesa watu hawapati huduma basi hapa kama roho yako ni maalumu na inatakiwa iendelee kuwepo katika nyakati zijazo basi ili usijitie unajisi wale malaika wa mfumo nyota wako wanaamua kukutoa katika uso wa dunia ili uendelee kuwa salama( wengi wanaokutana na hili ni wale ambao wamebeba hatima mpya kabisa ambazo hazikuwepo duniani ila wale ambao mmebeba hatima zilizopo ukienda kinyume na miiko ya hatima yako utaendelea kusalia na mwisho wa siku utajipa uharibifu katika roho yako wewe mwenyewe). Na hawa ndio wale ambao huwa mnasema wamekufa kwasababu wametenda dhambi.

Ila pia kuna hii sababu ya tano ambayo huwa si common sana ya kwamba wapo watu ambao huzaliwa wakiwa na itirafu kubwa katika upande wao wa kiroho kwahiyo hawa unakuta wanazaliwa na hawakai sana wanarudi walikotoka na itilafu hizi zaweza kuwa nyakati za hatima walizowekewa bado hazijafikiwa au pia wapo wale ambao roho zao ziliishi hapa duniani muda mfupi na zikarudi tena kabla zile kumbukumbu za kale hazijaharibiwa kupitia watu hao na watu wa namna hii huwa wanakua na mambo mengi wanayoyajua kulinganisha na watu wengine wa dunia na sababu zingine nyingi pengine nitaendelea kuziweka katika vipande vingine vya ziada. Na vifo vya watu wa namna hii huwa kila mtu anaongea lake.

Kwahiyo nimekupa hii ili ujue kwamba si kila mtu anaekufa ni kwamba amekufa kwaajiri ya kwenda kutimiza hatima ya mtu mwingine isipokua wengine hufa kwasababu moja wapo kati ya hizo nne zingine ambazo nimekuelezea kwa ufupi sana hapo juu.

Na katika ulimwengu wa kiroho nilikwambia kwamba wale wenye hatima hasi na wale wenye hatima chanya wote wananafasi ya uhuisho wa roho zao wakati watakapo maliza hatima walizotumwa kuzitimiza hapa duniani, isipokua ni upande tu ndio tunagawana kuna wale ambao ni magugu na wale ambao ni ngano.

Na katika hizo hizo ngano huwa kuna ngano ambazo mbegu zake ni bora sana na kuna zile ambazo mbegu zake ni dhaifu lakini pia zipo zile ambazo zimetoa mbegu zilizooza, sasa wakati unafurahia wewe kuwa ngano ni lazima ufikirie pia kwamba wewe ni ngano ya aina gani kati ya zile zenye mbegu bora, au zile zenye mbegu dhaifu na zile zilizo na mbegu zilizooza.

Na kwenye maisha ya hapa duniani hautakiwi kuhukumu na inawezekana ulikua unahukumu kwakua ulikua haujui mambo haya ila naamini sasa umepata kuyajua kwamba kutokana na utofauti wa hatima tulizo beba ndio hupelekea mambo yawe hivi, kwamba wakati wewe unamuona mwenzio anadhambi kufanya vitendo vya namna fulani fulani ila wakati huo huo mwenzio yeye kwa kupitia vitendo hivyo afanyavyo katika ulimwengu wake yeye anaonekana ni shujaa kama vile Sauli alivyokua anawaua watumishi wa Mungu nyakati zile.

Pia lazima ujiulize kwanini Sauli licha ya kuwa na dhambi ya giza ila Mungu alimsamehe na kumuacha amtumikie? Jibu ni kwamba Sauli hakuwa na makosa kwasababu yeye alichokua anakifanya ni kutimiza ile hatima iliyokuwa ndani yake kwa wakati ule, ila baada ya kutiwa upofu wa ile hatima mbaya ambayo alikua anaelekea kuitimiza na kufunguliwa macho ya kuona hatima impasayo kwenda kuitimiza aliifuata njia yake kwa nguvu zile zile na hari ile ile ila wakati huu alikua anatimiza hatima ya kiungu iliyofunuliwa ndani yake.

Kwahiyo duniani sio kila mtu ni wa Mungu ila wangine ni mapandikizi ya shetani na kwa kuthibitisha hili embu tuone huu mfano ambao Yesu mwenyewe aliwatolea wanafunzi wake.

MATHAYO 13:24-30

Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake. Lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.

Baada ya huo mfano twende katika mfano mwingine pale katika ufunuo ili niweze kukufungulia codes vizuri.

UFUNUO WA YOHANA 12:7-10.

Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

Kwahiyo kumbe shetani yaani ibilisi baada ya kushindwa vita kule mbinguni aliweza kutupwa duniani. Sasa hiki kitendo tu cha Ibilisi yaani shetani kutolewa kule mbinguni na kutupwa duniani kina ashiria kwamba dunia haina huruma na wewe na kamwe haitakaa iwe na huruma na wewe, kwa maana hata aliyekuumba hana huruma na wewe isipokua amekuweka hapa kwakua anaimani kubwa na wewe kwasababu wewe ni miongoni mwa wanajeshi wake ambao wamefuzu kwenye yale mafunzo ya kijeshi ya kupigana kwenye vita hii kubwa ya mapambano dhidi ya hatima, chukulia tena mfano huu mdogo, kwamba nchi ambayo inapeleka wanajeshi wake katika uwanja wa vita, unadhani inaweza kumchukua mwanajeshi ambae wana uhakika bado hajafuzu kwenye mafunzo ya kijeshi? Jibu ni hapana bali huwa wanachukua wale wote ambao wanauhakika kwamba wamefuzu kwenye mafunzo ya kijeshi, na wao kama nchi wanakua na imani kubwa na wanajeshi hao, na tumaini lao siku zote ni kwamba wataenda kwenye uwanja wa mapambano na watakaporudi lazima watarudi na ushindi.

Sasa nini kinatokea wakati unapokua umefika katika uwanja wa vita, wale waliokutuma hawatokua na muda na wewe ila watakachokifanya ni kupokea yale maombi ambayo utayaomba kwao kupitia redio call na wao watakachokifanya ni kukutekelezea kwa wakati ili undelee kupambana mwisho wa vita urudi na ushindi kwenye nchi yako, kwahiyo unachotakiwa kufanya ni kupambana na sio kulia lia kwa maana kwenye uwanja wa vita kila mmoja anapambania hatima yake yeye mwenyewe, na ikitokea ukafanikiwa kushinda ukirudi kwenye nchi yako basi utatunukiwa medali ya ushindi na ushujaa na ikitokea ukafia kwenye uwanja wa kivita basi utazikwa na shughuli yako itakua imeishia hapo.

Mfano huo huo wa wanajeshi na nchi, ndivyo ilivyo kwako wewe na yule aliyekuumba yaani Mungu, ukijijua uko hapa duniani ujue umeaminika na matarajio makubwa ya ushindi yapo juu yako, kwahiyo hautakiwi kulia lia kwa maana hakuna atakaekuelewa kwasababu kila mmoja hapa duniani yupo kwenye vita ya kutimiza hatima yake, na machozi yako pia hayatafanya aliyekuumba akuhurumie ila atakachofanya ni kupokea maombi yako ambayo utayapeleka kwake kupitia njia ya kiroho yaani unatakiwa ujiungamanishe na malaika walio katika mfumo nyota wako, na yeye atakutekelezea yale uyaombayo ili uendelee kupambana na mwisho wa siku uweze kurudi na ushindi wa ile hatima kuu ambayo alikuumba ili uje uitekeleze hapa duniani, na baada ya ushindi ndipo utakapo pata kutunukiwa zawadi ya uzima wa milele na ukishindwa kwenye hii vita basi roho yako itazikwa na ile zawadi ya uzima wa milele haitakua juu yako.

Sasa basi tukirudi kwenye hayo maandiko, tunaona baada ya shetani kutupwa hapa duniani ambako ni kama shamba la bwana liliopandwa ngano, na hizo ngano ndio wale wote ambao wamebeba hatima chanya za kimungu ndani yao, lakini sasa shetani ambae ni adui alivyokuja nayeye akaamua kupanda magugu yaani wale watu ambao wako hapa duniani kwaajiri ya kutimiza zile hatima hasi nao walipandwa kwenye shamba lenye mbegu bora ili tu kuweza kuvuruga kwa maana ngano ikiwa bado haijamea ukiichanganya na magugu huwezi kujua ipi ni ngano na ipi ni gugu na ndio maana tukikaa mimi na wewe na yule tukitazamana wote tunaonekana binadamu wa kawaida ila kumbe ndani yetu yapo magugu na magugu ni wale ambao wamebeba hatima hasi yaani hatima za kishetani ndani yao.

Halafu anasema, wale wafanya kazi wakamfuata na wakamuambia tuyatoe magugu na tuache ngano, ila yeye akawaambia wakifanya hivyo watachanganya kwa maana wanaweza kung'oa mche wa ngano wakahisi ni gugu ila alichosema waache tu hadi ngano zitakapo mea ndipo zitapoonesha utofauti na yale magugu na hapo ndipo atakapowaambia wang'oe hayo magugu wayafunge na waende kuyachoma moto.

Wewe ambae umekuja hapa duniani kutimiza hatima ya kimungu unatakiwa kukomaa ili ujitenge na magugu, kwa maana ya kuinyanyua ile nguvu iliyopo ndani yako na pia ushike njia uanze kutimiza ile hatima iliyofanya uumbwe kwani hatima ya zile ngano zilizopandwa kwenye lile shamba ni kuhakikisha zinamea na kutoa ngano, ila zikiishia njiani na zikashindwa kutengeneza ngano basi zitang'olewa pamoja na magugu ili zikachomwe moto, na pia ukumbuke kuna watu aina ya kina Sauli ambao wao wamebeba nguvu zilizo na uwiano, sasa endapo uking'oa miche yao ukadhani kwamba ni magugu wakati wakiwa bado hawajamea basi moja kwa moja utakua umechanganya kwa maana licha ya kwamba ni kina Sauli lakini kadri wanapomea wanauwezo mkubwa wa kubadilika na kuwa kina Paulo.

Sasa ukirudi kwenye lile shamba utagundua kwamba kuna vita kubwa ya hatima ya kumea kwa maana kuna yale magugu ambayo huwa yanatambaa, sasa yakikutana na mche wa ngano ambao ni dhaifu wanautumia kutambaa juu yake ili yaweze kustawi na mche huu utakufa au utamea kwa shida na utashindwa kutengeneza ngano kwahiyo kipindi cha mavuno kikifika nao utang'olewa pamoja na lile gugu lililoutumia kutimiza hatima yake ya kumea zaidi, na hivi ndivyo itakavyo kuwa kwa wewe ambae unakubali kuwa dhaifu ili watu wengine wakutumie kwenye harakati zao za kutimiza hatima.

Kwahiyo ili uweze kushinda hii vita ili kipindi hata roho itakapoacha mwili iweze kwenda kwenye ulimwengu wajuu ni lazima uweze kufikia hatima yako, na ufanikiwe kunyanyua zile nguvu zilizomo ndani yako kwasababu nimeshakwambia usiponyanyua hizi nguvu za asili zilizomo ndani yako hautaweza kufikia hatima kwa maana vita ya hatima iliyopo hapa duniani ni kubwa sana na mara tu utakapogundulika umeanza kuielekea njia ya hatima yako lazima uje kujaribiwa ili wajue umejipanga panga vipi, na kwakua wewe hauna nguvu basi utashindwa kukwepa mitego na hatimae watakurudisha nyuma.

Kwani hata shetani alipoona Yesu anaanza kuielekea ile njia inayoenda kwenye hatima yake basi aliamua kumfuata, kipindi Yesu alipokua kwenye mfungo na akaanza kumjaribu, sasa kwakua Yesu tayari alishafanikiwa kuinyanyua ile nguvu ya asili ambayo ilikua ndani yake huu mtihani wa majaribu yake ibilisi kwake haukua mgumu kwenye namna ya kuuvuka.

Sasa kama Yesu tu alijaribiwa baada ya kuonwa ameanza kuifuata ile njia inayoelekea kwenye lengo kuu la yeye kuletwa hapa duniani, wewe ni nani mpaka ushindwe kujaribiwa? Kuishi maisha ya hatima yako huwa sio rahisi na ndio maana utaona wengi ni masikini hapa duniani ila wachache wanaofanikiwa ni wale wa upande hasi ila wa huku upande chanya bado wanajikongoja lakini mambo yanawezekana endapo tu utaamua kuishi maisha ya kufuata sheria za kiimani hasa ile inayofungamana na wewe kwa maana iliyotumika kunyanyua nguvu yako ya asili.

... Naishia hapa kwa leo ila nitarudi baada ya muda, naacha gape kidogo ili uweze kusoma kwa kutafakari na ujipe muda wa utulivu ujenge maswali kwaajiri ya kuuliza.
 
Ukipata mda jaribu kutueleza kwa mifano hapo kwenye kunyanyua nguvu iliomo ndani Yako..case study tumia Imani ya kikristo,kiislam na kishetani..

Hzo nguvu zinanyanyuliwaje?? Baada ya mtu kujipata , vip ananyanyua hzo nguvu??
 
Mtoa maada msaada plz!!

Hatma yangu naijua na naitekeleza vizur tu, shukran kwa mwenyenz Mungu..kipawa nimepewa Cha biashara nipo na biashara mbili zote zina fanya kazi katika mazingira tofauti.. tatizo langu sijui nistick na biashara ipi kati ya hzi!!

Biashara ya kwanza.. nakopesha mikopo, ni biashara naipenda zaidi katika ulimwengu huu..nipo na ofisi na wafanyakaz watatu na vibali vya serikali...
Biashara hii natumia nguvu kubwa sana kuifanya iendelee sababu naipenda toka ndani yangu, nguvu kubwa nayotumia ni ikiwepo kukwepa baadhi ya Kodi za serikali na kukopesha kwa riba tofauti na Ile ya muongozo wa B.o.t ,pia napambana sana dhidi ya wakopaji wadhulumaji mara kadhaa nadhulumiwa but biashara inaendelea..

Inanipa matokea but nawaza sana daily in a long run ntatumia hii nguvu kuiendesha hadi lini??na naipenda sana hii biashara..

Biashara ya pili..nauza nguo za ndani za wanawake na watoto..umo yupo wife na mabinti kadhaa na vijana kadhaa .. biashara hii siipend toka moyon mwangu but ni biashara inayonipa matokeo bila kutumia nguvu(labda sabb mm siendi uko masokoni hvo naona situmii nguvu sabb nasubir tu mauzo yaletwe)

biashara hii nafanya kama buckup ya Ile ya mikopo chochote kikitokea Kule natoa pesa uku napeleka Kule sabb Ile naipenda toka moyoni..

Asa nimefika hatua nataka kufocus na biashara Moja kama njia ya kuelekea kwenye hatma yangu..je kwa maelezo hayo ya juu juu mtoa maada waona ni ipi biashara inayofungamana na mimi..au je kuna uwezekano wa mtu kuwa na fungamano na biashara zaid ya Moja kuelekea hatma yake??

Je kukwepa Kodi za serikali na kubadili viwango vya riba vilivyowekwa na b.o.t katika biashara inayofungamana na ww ni sahihi? Yaan ni changamoto katika biashara!!? ama naforce biashara nayoipenda but haifungamani na Mimi??
Thanks 🙏 🙏 🙏
 
Swali zuri.

Biashara hizi mbili ziko kwenye category tofauti hili kwanza unatakiwa ulielewe.

Lakini pia ni kweli mtu anaweza akawa anafungamana na biashara zaidi ya moja ila ni lazima biashara hizi ziwe zinatoka kwenye Ile asili yake.

Na kuhusu wewe kufanikiwa kwenye hiyo biashara ya nguo inawezekana kabisa unafanikiwa kwa sababu unatumia mgongo wa huyo mkeo, yaani yeye ndio anafungamana na hicho mnachojifanya moja kwa moja au na wewe pia yawezekana asiLi yako iko huko ila bado haujajua.

Na wewe na hiyo biashara unayoipenda sana inawezekana ikawa ndio biashara inayofungamana na wewe ila unatumia nguvu kwa sababu bado haujaitengenezea mfumo mzuri wa kuifanya kiurahisi au ikawa ni biashara isiyofungamana na wewe ila ni vile tu mazingira yamekutengeneza kuona kama ndio yenyewe.

Mazingira yako na kawaida ya kutengeneza hatima za watu kwamfano kama umezaliwa kwenye familia ambayo kaka yako wa kwanza ni mchezaji mpira mzuri na wewe ukawa unatumia muda mwingi kuwa nae na unaona vile anapay bills hapo nyumbani basi automatic na wewe utaanza kurise interest kwenye huo upande na utajikuta hadi moyoni unatamani kuwa kama huyo kaka yako, na hii huwa inaendaga hata kwenye maswala ya elimu Kwa maana ya kwamba yule mtoto wa kwanza kwenye familia kama alibahatika kufika chuo kikuu basi kile akichosomea huwa kinakua ndani ya vichwa vya wadogo zake wengine ambao wako shuleni bado, Kwa hiyo kama ni udaktari au uhandisi basi wanajikuta kwenye familia nusu ya watoto wanaangukia kwenye huo upande hata Kwa kufosi.

Na Kwa case hii sio tu kwenye familia ila pia hata marafiki waliotuzunguka nao huwa wanachangia sana kutuingiza kwenye aina hii ya mtego.

Sasa basi, Kwa case yako hii...

Ili tuweze kuwa na uhakika juu ya hili inabidi unitafute tupige story angalau siku mbili tatu... story tu za kawaida baada ya hapo nitakupa jibu la moja kwa moja kwamba hiyo ndio au sio na kama ndio basi tutafanya mazungumzo kuanzia hapo Ili kuona namna ambavyo unaweza kuifanya bila kutumia nguvu kubwa na stress.

NB:
Kuigundua biashara ya hatma yako haimaanishi kwamba hautotumia nguvu wakati unapoenda kuianza hiyo biashara, ni lazima kuna nguvu fulani uiweke kwanza kwa maana sababu ya wewe kuanza hiyo biashara haitakua sababu ya wateja kuja kukuungisha.

Lakini pia unapoanzisha biashara hakuna mtu yeyote ambae atakua anajua kwamba sehemu fulani yupo mtu fulani ambae ame fungua biashara fulani ila watajua pale tu utakapowajulisha.

Biashara ni dunia ndani ya dunia na moja kati ya sheria kuu ndani ya dunia ya Biashara ni kusaidiana na mtu wa kwanza ambae anatakiwa aoneshe nia ya dhati ya kuanza kumsaidia mwenzake ni wewe uliyeona mtu fulani yuko na tatizo fulani ambalo utatuzi wake ni hiI bidhaa au huduma niliyo nayo mimi (na hapa ndipo ambapo kuna kazi na nguvu kidogo lazima itumike ili kulifanya hili lieleweke).

Lakini pia niliwaambia kwamba kwenye hizi biashara zihusuzo hatima huwa zipo biashara ambazo hazimkatai mtu yaani ni biashara ambazo mtu wa asili yoyote anaweza kuzifanya na akapata matokeo, na nilisema nitakuja na uzi kuzioodhesha biashara za namna hii ila pia hii biashara unayoifanya wewe ni moja kati ya biashara ambazo zinaangukia kwenye category hiyo. (Kwa maana hii ni biashara ya pesa Kwa pesa).
 
Asante kwa ufafanuzi!!!🙏🙏🙏🙏
 
Thecoder, unaamini juu ya uwepo wa moto wa milele? Maana kunamahala unasema roho zitakazotimiza hatma zitapata uzima wa milele na zile zisizotimiza zitazikwa, naomba ufafanuzi
 
Natumai mko salama.

Kama kichwa cha habari kinavyosema kwamba dunia ni uwanja wa vita za hatima kwahiyo kila mtu ambae yuko hapa duniani anapaswa kujua kwamba yuko vitani na swala la kushinda au kushindwa ni juu ya mtu mwenyewe.

Sasa iko hivi...

Kimsingi ni kwamba kila mwanadamu ambae yuko kwenye hii dunia hayupo hapa kwa bahati mbaya na inawezekana wazazi waliomzaa mtu huyo wanaamini wamemleta huyo mtu hapa duniani kibahati mbaya ila kiroho hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya.

Maadam umezaliwa na uko hapa duniani basi kaa ukijua kuna mission unatakiwa uitimize na hii mission ndio ambayo tunaita hatima na pindi utakapoitimiza mission hiyo basi hapo ndio utakapopata uhuisho wa roho yako na kuifanya iwe hai milele na roho ambayo iko hai ndio roho ambayo husikia inaposemeshwa na ndio maana katika asili za kiafrika hasa hapa nyumbani Tanzania unakutana na kitu kinaitwa mizimu.

Sasa mizimu ni nini? Mizimu ni roho ambazo ziliishi kwenye milli ya watu fulani kwa uadilifu kwa maana ziliweza kujua zipo hapa duniani kwa lengo gani yaani hatima yao na wakapigana vita ya kuiendea hiyo hatima na wakafanikiwa kwa kiasi kikubwa na pindi deadline yao ya kuishi hapa duniani ilipofika zile roho zao ziliweza kuuhishwa na kupata uzima wa milele.

Kwahiyo Sasa katika ile mitetemo ya mfumo nyota ya koo na koo ukiweza kujiungamanisha kiroho na roho za babu ambao unawajua walikua manguli katika upande wa kutibu au kwenye jambo lolote lile ambalo lilikua hatima ya babu huyo ila ilimradi tu uwe na uhakika kwamba alifanya kweli makubwa na sifa zake hadi leo bado zipo hapo kijijini basi ukijiungamanisha tu na roho za watu wa namna hii huwa zinasikia na zinatoa majibu papo kwa hapo.

Nimesema uwe na uhakika kwasababu usije ukaenda kujiungamanisha na mtu ambae huna uhakika nae na ukaenda kuvaa roho za ajabu zikakutesa kwenye maisha yako na hapa ndipo ambapo watu wengi wanachukia haya mambo ya mizimu kwasababu huwa ni ngumu kujua babu yako mzaa babu yako alichokifanya kama kilisaidia kuongeza positive energy hapa duniani au laa (hapa nitapazungumzia vizuri huko mbele na utajua kwanini watu wanakimbilia kwa Yesu au Muhammad huku wakiacha mizimu ya babu zao kule kijijini).

Kwasasa turudi hapa kidogo...

Kikawaida binadamu huwa yuko na pande kuu mbili yaani ya damu na nyama na ya kiroho.

Upande wa kiroho ndio Upande ambao umembeba mtu halisi na ndio upande ambao unamuunganisha mtu na ulimwengu wa asili yake na upande huu huu unapokuwa hapa duniani huwa unatumika kama redio call na kwanini kama radio call basi nitakwenda kukuelezea hapo mbele kidogo. Na upande wa damu na nyama ndio upande ambao unamuunganisha mtu na ulimwengu huu wa vita za hatima.

Wakati mtu anapozaliwa huwa anakua anaishi zaidi kwenye ulimwengu wa kiroho kuliko ulimwengu huu wa damu na nyama ila kadri anavyokua na kujifunza mambo mapya ile mitetemo yake ya ulimwengu wa asili yake inapungua na ya ulimwengu huu inaongezeka hadi kufikia kwenye ukubwa toshelezi na hapa ndio mtu anaanza kuishi maisha ya ulimwengu huu wa damu na nyama na kusahau namna ya kuishi ulimwengu wa kiroho.

Na kutokana na kwamba binadamu anaishi zaidi katika ulimwengu wa damu na nyama kuliko ulimwengu wa kiroho hii imefanya wengi wetu tushindwe kuelewa lengo na dhumuni la sisi kuwa hapa duniani na badala yake tunaishi kulingana na mfumo wa kidunia na kushindwa kuelewa hatima zetu ni nini.

Na kitu cha kikuu na chaumuhimu zaidi kuhusu hatima ni kwamba kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na vitu vyote ambavyo unapaswa kuvimiliki hapa duniani vipo kwenye hatima yako.

Kwahiyo watu wote ambao wanaziendea njia za hatima yao iwe kwa kujua au kwakutokujua huwa hawahangaiki kwenye swala la fedha kama ambavyo watu wanaoishi kwenye maisha yaliyo nje ya hatima zao hufanya.

Na ninaposema hatima kuna watu wanadhani nazungumzia kitu fulani ambacho ni maalumu sana yaani kitu ambacho hakiwezekani kugundulika kirahisi raising hivi, ila naomba nikutoe wasiwasi na nikwambie tu kwamba hakuna umaalumu wowote kwenye hatima kwasababu hatima ni mambo yote ambayo yanaweza kufanyika hapa duniani ili kuongeza nguvu chanya na kuifanya dunia iwe sehemu salama.

Kwa maana hiyo kuna watu hatima zao ni kuburudisha na kuna watu hatima zao ni kuvumbua mambo kadha wa kadha na kuna watu hatima zao ni kutibu watu wengine na kuna watu hatima zao ni kufundisha mambo mbalimbali na kadhalika.

Na ili uweze kufikia hatima yako lazima upite kwenye njia fulani na hiyo njia ndio huwa tunaiita kipawa au kipaji.

Ndio, ni kipaji kwahiyo wala usishtuke kwasababu hata wewe unachokipaji ambacho ukikitumia kitakupeleka moja kwa moja kwenye hatima yako na mara tu utakapofika kwenye hatima yako basi watu wote watajua kwamba yupo au alikuwepo mtu fulani ambae alifanya makubwa sana kwenye mambo haya ya burudani hasa upande huu wa mpira na mtu huyo aliitwa Leonel Messi au Christiano Ronaldo.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye mambo haya ya uvumvuzi wa mambo ya kisayansi ambae aliitwa Isaac Newton.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye haya mambo ya muziki wa rege ambae aliitwa Bob Marley.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye upande wa mashoati na movie za kupigana za karate aliitwa Blue Lee.

Kwahiyo hii inakwenda zaidi na zaidi na kuwafikia vizazi na vizazi huku wakiishi na kuutukuza ufalme wako kwenye upande huo wa hatima yako bila kujali mwaka ambao deadline yako ilifika na wewe kurudi kwenye ulimwengu wa asili yako huku roho yako ikiuhishwa na kupata uzima wa milele.

Na lazima ujue pia kwamba ukubwa wa hatima baina ya mtu na mtu huwa umetofautiana yaani kuna watu wamebeba hatima za kidunia ila wapo waliobeba hatima za kibara na wapo waliobeba za kiukanda lakini pia wapo waliobeba za kinchi na wapo waliobeba hatima za kimkoa, kijiji, kiukoo na kifamilia.

Ili ujue hatima yako ni ya ukubwa gani basi mambo utakayoyafanya kiwepesi sana yaani bila kutumia nguvu utaona yanaenda yanafika kwenye ngazi fulani ila utakapotaka uvuke hiyo ngazi uende ngazi nyingine utaona unatumika nguvu kubwa sana lakini matokeo yake hayawi kama pale awali ambapo ulikua hautumii nguvu nyingi ila mambo yalikua yanaenda parefu, hapo unatakiwa ujue kwamba wewe ukubwa wa hatima yako mwisho wake ni hapo.

Na hapa najua umeanza kunielewa pia ninaposema kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na pindi utakapoigundua hatima yako na kuifuata ile njia inayoelekea huko basi moja kwa moja utaanza kuona wepesi wa mambo katika upande wa umiliki wa fedha na Mali.

Kwahiyo kumbe mateso ambayo watu wengi wanayapata kwenye upande wa kifedha huwa sababu moja wapo ni kuishi maisha yaliyo nje ya hatima zao na hii hufanya watumie nguvu sana kwenye swala la utafutaji huku wakiambulia kidogo kisicholingana na nguvu walizotumia.

Na unakutana na mtu anasali sana lakini bado mambo hayakai kwenye line, na hii sio kwasababu maombi yako hayafiki kule lahasha maombi yako yanafika ila nimekwambia kila roho iko na codes na hizi codes ndio hatima yako iko humo ndani na Kimsingi ulimwengu wa juu haukutambui wewe kwa sura na umbo lako la damu na nyama ila unakutambua wewe kwa codes zilizopo rohoni mwako, kwahiyo unavyoomba ile mitetemo inaenda moja kwa moja hadi kwenye ule mfumo nyota wa asili yako na majibu yanaporudi yanarudi kwakufuata ile code ambayo ipo ndani ya roho zako kwa maana hiyo kama maombi ni kubarikiwa kwenye utafutaji wako baraka itaongezwa kwenye ile hatima iliyopo ndani yako.

Kwahiyo ikiwa wewe hatima yako ni udaktari halafu ukashindwa kuifuata hatima hiyo na ukaamua uende upande mwingine labda wa ujenzi na mambo yakakuwia magumu huko hadi kufikia hatua ya kupiga goti chini ili ujiungamanishe mitetemo ya mfumo nyota ya asili yako basi kuwa na hakika kwamba maombi yako yatafika na majibu yatarudi ila wewe utakua unapishana mwenyewe, yenyewe yanaenda kwenye afya wewe upo kwenye ujenzi.

Sasa hili ndio lengo la uumbaji, ni kwamba roho ilitengenezwa kwa codes na kila kitu kikawa kimewekwa ndani yake kisha unaletwa hapa duniani na unapumbazwa na mambo ya dunia hadi unasahau roho yako imebeba kitu gani maalumu na chaupekee ambacho unatakiwa kukifanya ili uweze kuongeza nguvu za mitetemo chanya itakayosaidia kuifanya dunia kuwa sehemu salama.

Na ukumbuke kwamba kwenye kila hatima iliyopo ndani ya mtu huwa imewekwa na deadline yake na hiyo deadline ikifika basi muhusika anarudi kwenye ulimwengu wa asili yake yaani anakufa kama mnavyosemaga.

Sasa mpumbazo huu wa dunia ukikukumba kwa kiasi kikubwa na ikapelekea ukaenda hadi siku ya deadline yako, basi hapo ndio utakua upande wa zile mbegu ambazo si bora na mbegu ambayo si bora huwa mkulima anakua na option mbili either aitupe au aipe nafasi ya pili.

Ikitupwa haitoonekana tena shambani milele na milele ila ikipewa nafasi ya pili basi mkulima atajaribu kuipanda tena ili aone kama italeta matunda au laa na ndio hapa Sasa unakutana na roho ambazo zipo kwenye miili ya watu ila roho hizo zilishawahi kuwa hapa duniani hapo kabla (watu wenye roho za namna hii wapo wengi tu).

Ngoja leo niishie hapa kwanza ila nimeanzia huku mbali kidogo ili nitakapounganisha ili niweze kukuelezea ni kwanamna gani dunia ni uwanja wa vita za hatima uweze kunielewa vizuri.

Maelezo haya unayapata kitabu gani ??
 
Thecoder, unaamini juu ya uwepo wa moto wa milele? Maana kunamahala unasema roho zitakazotimiza hatma zitapata uzima wa milele na zile zisizotimiza zitazikwa, naomba ufafanuzi
Siamini kwenye Moto wa milele na haupo huo Moto unaosemwa na watu.

Ukisoma vizuri kuna pahala nimetolea mfano mdogo wa mbegu na mkulima lakini pia nikatolea mfano mdogo wa mwanajeshi vitani ili kuifanya imara hoja hiyo ya uzima wa milele.

Roho huwa zinatreatiwa kwa namna tatu, ya kwanza ni kuzaliwa kufa na kurudishwa tena duniani, ya pili ni kuzaliwa kufa na kuondolewa kwenye mfumo moja kwa moja kwa Maana ya kwamba zimeharibika kwa hiyo zinaondolewa katika mfumo wa dunia na ya tatu ni zile roho ambazo zinauhishwa na kupata uzima ule wa milele.

Hizi roho ambazo zinapata uzima wa milele huwa hazirudi duniani kuzaliwa upya ila zinakua na muunganiko wa moja kwa moja na dunia, ndio nikasema kuna maeneo watu huziita mizimu na wengine huita malaika na kadhalika.

Kwahiyo roho zilizo nyingi huenda na kurudi ila chache ndio hupata bahati ya uhuwishaji na ndicho hiki ambacho hupiganiwa na watu wengi kwenye maeneo mbalimbali ya ibada.
 
Telegram kuna channel ya vitabu inaitwa alive online library... nenda hapo utakikuta.
sawa..na vp hii Dunia ni uwanja wa vita muendelezo wake ndio imeisha au ni mda mrefu sana umepita huko telegram vitabu kwa lugha ya kiingereza si wote wataelewa kuliko ww ulivyopost hapa...fanya muendelezo mkuu
 
Hiko ni chakiswahili sio kingereza na muendelezo nitauweka coz huu ni uzi ambao nitakua naweka mambo yote yanayohusiana na maswala hayo.
 
Natumai mko salama.

Kama kichwa cha habari kinavyosema kwamba dunia ni uwanja wa vita za hatima kwahiyo kila mtu ambae yuko hapa duniani anapaswa kujua kwamba yuko vitani na swala la kushinda au kushindwa ni juu ya mtu mwenyewe.

Sasa iko hivi...

Kimsingi ni kwamba kila mwanadamu ambae yuko kwenye hii dunia hayupo hapa kwa bahati mbaya na inawezekana wazazi waliomzaa mtu huyo wanaamini wamemleta huyo mtu hapa duniani kibahati mbaya ila kiroho hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya.

Maadam umezaliwa na uko hapa duniani basi kaa ukijua kuna mission unatakiwa uitimize na hii mission ndio ambayo tunaita hatima na pindi utakapoitimiza mission hiyo basi hapo ndio utakapopata uhuisho wa roho yako na kuifanya iwe hai milele na roho ambayo iko hai ndio roho ambayo husikia inaposemeshwa na ndio maana katika asili za kiafrika hasa hapa nyumbani Tanzania unakutana na kitu kinaitwa mizimu.

Sasa mizimu ni nini? Mizimu ni roho ambazo ziliishi kwenye milli ya watu fulani kwa uadilifu kwa maana ziliweza kujua zipo hapa duniani kwa lengo gani yaani hatima yao na wakapigana vita ya kuiendea hiyo hatima na wakafanikiwa kwa kiasi kikubwa na pindi deadline yao ya kuishi hapa duniani ilipofika zile roho zao ziliweza kuuhishwa na kupata uzima wa milele.

Kwahiyo Sasa katika ile mitetemo ya mfumo nyota ya koo na koo ukiweza kujiungamanisha kiroho na roho za babu ambao unawajua walikua manguli katika upande wa kutibu au kwenye jambo lolote lile ambalo lilikua hatima ya babu huyo ila ilimradi tu uwe na uhakika kwamba alifanya kweli makubwa na sifa zake hadi leo bado zipo hapo kijijini basi ukijiungamanisha tu na roho za watu wa namna hii huwa zinasikia na zinatoa majibu papo kwa hapo.

Nimesema uwe na uhakika kwasababu usije ukaenda kujiungamanisha na mtu ambae huna uhakika nae na ukaenda kuvaa roho za ajabu zikakutesa kwenye maisha yako na hapa ndipo ambapo watu wengi wanachukia haya mambo ya mizimu kwasababu huwa ni ngumu kujua babu yako mzaa babu yako alichokifanya kama kilisaidia kuongeza positive energy hapa duniani au laa (hapa nitapazungumzia vizuri huko mbele na utajua kwanini watu wanakimbilia kwa Yesu au Muhammad huku wakiacha mizimu ya babu zao kule kijijini).

Kwasasa turudi hapa kidogo...

Kikawaida binadamu huwa yuko na pande kuu mbili yaani ya damu na nyama na ya kiroho.

Upande wa kiroho ndio Upande ambao umembeba mtu halisi na ndio upande ambao unamuunganisha mtu na ulimwengu wa asili yake na upande huu huu unapokuwa hapa duniani huwa unatumika kama redio call na kwanini kama radio call basi nitakwenda kukuelezea hapo mbele kidogo. Na upande wa damu na nyama ndio upande ambao unamuunganisha mtu na ulimwengu huu wa vita za hatima.

Wakati mtu anapozaliwa huwa anakua anaishi zaidi kwenye ulimwengu wa kiroho kuliko ulimwengu huu wa damu na nyama ila kadri anavyokua na kujifunza mambo mapya ile mitetemo yake ya ulimwengu wa asili yake inapungua na ya ulimwengu huu inaongezeka hadi kufikia kwenye ukubwa toshelezi na hapa ndio mtu anaanza kuishi maisha ya ulimwengu huu wa damu na nyama na kusahau namna ya kuishi ulimwengu wa kiroho.

Na kutokana na kwamba binadamu anaishi zaidi katika ulimwengu wa damu na nyama kuliko ulimwengu wa kiroho hii imefanya wengi wetu tushindwe kuelewa lengo na dhumuni la sisi kuwa hapa duniani na badala yake tunaishi kulingana na mfumo wa kidunia na kushindwa kuelewa hatima zetu ni nini.

Na kitu cha kikuu na chaumuhimu zaidi kuhusu hatima ni kwamba kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na vitu vyote ambavyo unapaswa kuvimiliki hapa duniani vipo kwenye hatima yako.

Kwahiyo watu wote ambao wanaziendea njia za hatima yao iwe kwa kujua au kwakutokujua huwa hawahangaiki kwenye swala la fedha kama ambavyo watu wanaoishi kwenye maisha yaliyo nje ya hatima zao hufanya.

Na ninaposema hatima kuna watu wanadhani nazungumzia kitu fulani ambacho ni maalumu sana yaani kitu ambacho hakiwezekani kugundulika kirahisi raising hivi, ila naomba nikutoe wasiwasi na nikwambie tu kwamba hakuna umaalumu wowote kwenye hatima kwasababu hatima ni mambo yote ambayo yanaweza kufanyika hapa duniani ili kuongeza nguvu chanya na kuifanya dunia iwe sehemu salama.

Kwa maana hiyo kuna watu hatima zao ni kuburudisha na kuna watu hatima zao ni kuvumbua mambo kadha wa kadha na kuna watu hatima zao ni kutibu watu wengine na kuna watu hatima zao ni kufundisha mambo mbalimbali na kadhalika.

Na ili uweze kufikia hatima yako lazima upite kwenye njia fulani na hiyo njia ndio huwa tunaiita kipawa au kipaji.

Ndio, ni kipaji kwahiyo wala usishtuke kwasababu hata wewe unachokipaji ambacho ukikitumia kitakupeleka moja kwa moja kwenye hatima yako na mara tu utakapofika kwenye hatima yako basi watu wote watajua kwamba yupo au alikuwepo mtu fulani ambae alifanya makubwa sana kwenye mambo haya ya burudani hasa upande huu wa mpira na mtu huyo aliitwa Leonel Messi au Christiano Ronaldo.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye mambo haya ya uvumvuzi wa mambo ya kisayansi ambae aliitwa Isaac Newton.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye haya mambo ya muziki wa rege ambae aliitwa Bob Marley.

Au alikuwepo mtu ambae alifanya makubwa sana kwenye upande wa mashoati na movie za kupigana za karate aliitwa Blue Lee.

Kwahiyo hii inakwenda zaidi na zaidi na kuwafikia vizazi na vizazi huku wakiishi na kuutukuza ufalme wako kwenye upande huo wa hatima yako bila kujali mwaka ambao deadline yako ilifika na wewe kurudi kwenye ulimwengu wa asili yako huku roho yako ikiuhishwa na kupata uzima wa milele.

Na lazima ujue pia kwamba ukubwa wa hatima baina ya mtu na mtu huwa umetofautiana yaani kuna watu wamebeba hatima za kidunia ila wapo waliobeba hatima za kibara na wapo waliobeba za kiukanda lakini pia wapo waliobeba za kinchi na wapo waliobeba hatima za kimkoa, kijiji, kiukoo na kifamilia.

Ili ujue hatima yako ni ya ukubwa gani basi mambo utakayoyafanya kiwepesi sana yaani bila kutumia nguvu utaona yanaenda yanafika kwenye ngazi fulani ila utakapotaka uvuke hiyo ngazi uende ngazi nyingine utaona unatumika nguvu kubwa sana lakini matokeo yake hayawi kama pale awali ambapo ulikua hautumii nguvu nyingi ila mambo yalikua yanaenda parefu, hapo unatakiwa ujue kwamba wewe ukubwa wa hatima yako mwisho wake ni hapo.

Na hapa najua umeanza kunielewa pia ninaposema kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na pindi utakapoigundua hatima yako na kuifuata ile njia inayoelekea huko basi moja kwa moja utaanza kuona wepesi wa mambo katika upande wa umiliki wa fedha na Mali.

Kwahiyo kumbe mateso ambayo watu wengi wanayapata kwenye upande wa kifedha huwa sababu moja wapo ni kuishi maisha yaliyo nje ya hatima zao na hii hufanya watumie nguvu sana kwenye swala la utafutaji huku wakiambulia kidogo kisicholingana na nguvu walizotumia.

Na unakutana na mtu anasali sana lakini bado mambo hayakai kwenye line, na hii sio kwasababu maombi yako hayafiki kule lahasha maombi yako yanafika ila nimekwambia kila roho iko na codes na hizi codes ndio hatima yako iko humo ndani na Kimsingi ulimwengu wa juu haukutambui wewe kwa sura na umbo lako la damu na nyama ila unakutambua wewe kwa codes zilizopo rohoni mwako, kwahiyo unavyoomba ile mitetemo inaenda moja kwa moja hadi kwenye ule mfumo nyota wa asili yako na majibu yanaporudi yanarudi kwakufuata ile code ambayo ipo ndani ya roho zako kwa maana hiyo kama maombi ni kubarikiwa kwenye utafutaji wako baraka itaongezwa kwenye ile hatima iliyopo ndani yako.

Kwahiyo ikiwa wewe hatima yako ni udaktari halafu ukashindwa kuifuata hatima hiyo na ukaamua uende upande mwingine labda wa ujenzi na mambo yakakuwia magumu huko hadi kufikia hatua ya kupiga goti chini ili ujiungamanishe mitetemo ya mfumo nyota ya asili yako basi kuwa na hakika kwamba maombi yako yatafika na majibu yatarudi ila wewe utakua unapishana mwenyewe, yenyewe yanaenda kwenye afya wewe upo kwenye ujenzi.

Sasa hili ndio lengo la uumbaji, ni kwamba roho ilitengenezwa kwa codes na kila kitu kikawa kimewekwa ndani yake kisha unaletwa hapa duniani na unapumbazwa na mambo ya dunia hadi unasahau roho yako imebeba kitu gani maalumu na chaupekee ambacho unatakiwa kukifanya ili uweze kuongeza nguvu za mitetemo chanya itakayosaidia kuifanya dunia kuwa sehemu salama.

Na ukumbuke kwamba kwenye kila hatima iliyopo ndani ya mtu huwa imewekwa na deadline yake na hiyo deadline ikifika basi muhusika anarudi kwenye ulimwengu wa asili yake yaani anakufa kama mnavyosemaga.

Sasa mpumbazo huu wa dunia ukikukumba kwa kiasi kikubwa na ikapelekea ukaenda hadi siku ya deadline yako, basi hapo ndio utakua upande wa zile mbegu ambazo si bora na mbegu ambayo si bora huwa mkulima anakua na option mbili either aitupe au aipe nafasi ya pili.

Ikitupwa haitoonekana tena shambani milele na milele ila ikipewa nafasi ya pili basi mkulima atajaribu kuipanda tena ili aone kama italeta matunda au laa na ndio hapa Sasa unakutana na roho ambazo zipo kwenye miili ya watu ila roho hizo zilishawahi kuwa hapa duniani hapo kabla (watu wenye roho za namna hii wapo wengi tu).

Ngoja leo niishie hapa kwanza ila nimeanzia huku mbali kidogo ili nitakapounganisha ili niweze kukuelezea ni kwanamna gani dunia ni uwanja wa vita za hatima uweze kunielewa vizuri.
Jamani mlioelewa njooni mnieleweshe.
 
Back
Top Bottom