SEHEMU YA SABA.
Tuliona sababu moja ya watu kufa ambayo ni kufa kwaajiri ya kwenda kutimiza hatima za watu wengine na hii ipo maeneo kadhaa kwenye biblia kwa mfano utaangalia lile tukio la Kaini na Abel jinsi ambayo Kain aliamua kumtumia ndugu yake ili aweze kuitimiza ile hatima yake ya ukuu.
Lakini ukiachana na sababu hii ya kufa kwaajiri ya kutimiza hatima ya mtu mwingine ila pia watu hufa kwasababu muda ambao walipangiwa kuwa hapa duniani umefikia tamati yaani ile deadline inakua imefika kwa maana nilikwambia sisi wote hapa duniani ni wageni na tupo hapa kwa lengo maalumu ambalo lipo ndani ya kila mmoja wetu na ukubwa wa lile lengo kuu au ile task ambayo imfenya mtu na mtu awe hapa ndio hasa ambayo inatoa utofauti wa muda wa mtu kuwa hapa, kwamfano kuna watu ambao wamebeba hatima ngumu na kubwa katika utekelezaji hawa huwa hata miaka yao ya kuishi huwa inakua mingi kidogo kuliko wale ambao wamebeba hatima nyepesi na rahisi katika kuzitekeleza. Na hawa ndio wale ambao mnasema wamekula chumvi nyingi kwahiyo wameishi maisha ya kumpendeza Mungu ila kiuhalisia kwenye hiko kipengele cha kumpendeza Mungu inawezekana kikawa hakikutimizwa na watu wa namna hii ila ni vile waliishi katika maisha ya kawaida ya kidunia kwa maana ili uishi kwa kumpendeza Mungu ni lazima uishi yale maisha ya hatima yako yaani utimize lile lengo kuu ambalo Mungu alikiweka ndani yako wakati uumbaji wako unafanyika.
Pia sababu ya tatu ya kwanini watu hufa ni kuvuka mipaka ya yale ambayo walipangiwa kuyafanya lakini wao walipofika hapa ule upande wao wa kiroho ukawa umefunguka zaidi na kujikuta wanafanya mambo makubwa ya kihatima hadi kuzidi yale ambayo walitakiwa wayafanye, ili kunusuru roho za namna hii ili zisipate uharibifu huwa zinachukuliwa kabla ya ile deadline haijafika. Na hawa ni wale ambao huwa mnasema kwamba wamekufa kwasababu wamemkufuru Mungu.
Pia sababu ya nne kuu ya kwanini watu hufa ni ile sababu ya kutimiza hatima iliyo ndani yako mapema kuliko ule muda ambao ulikadiriwa kisha ghafla ukaanza kutoka nje ya lengo, kwa maana kwamba unaanza kufanya mambo ambayo yako nje ya miiko ya hatima yako kwa mfano unakuta mtu anatoa huduma fulani ya kiroho ambayo haikutakiwa itolewe kwa njia ya pesa ila yeye baada ya kuona watu hufanikiwa sana kupitia huduma yake na ghafla anaanza kutoa huduma kwa pesa na pasipo pesa watu hawapati huduma basi hapa kama roho yako ni maalumu na inatakiwa iendelee kuwepo katika nyakati zijazo basi ili usijitie unajisi wale malaika wa mfumo nyota wako wanaamua kukutoa katika uso wa dunia ili uendelee kuwa salama( wengi wanaokutana na hili ni wale ambao wamebeba hatima mpya kabisa ambazo hazikuwepo duniani ila wale ambao mmebeba hatima zilizopo ukienda kinyume na miiko ya hatima yako utaendelea kusalia na mwisho wa siku utajipa uharibifu katika roho yako wewe mwenyewe). Na hawa ndio wale ambao huwa mnasema wamekufa kwasababu wametenda dhambi.
Ila pia kuna hii sababu ya tano ambayo huwa si common sana ya kwamba wapo watu ambao huzaliwa wakiwa na itirafu kubwa katika upande wao wa kiroho kwahiyo hawa unakuta wanazaliwa na hawakai sana wanarudi walikotoka na itilafu hizi zaweza kuwa nyakati za hatima walizowekewa bado hazijafikiwa au pia wapo wale ambao roho zao ziliishi hapa duniani muda mfupi na zikarudi tena kabla zile kumbukumbu za kale hazijaharibiwa kupitia watu hao na watu wa namna hii huwa wanakua na mambo mengi wanayoyajua kulinganisha na watu wengine wa dunia na sababu zingine nyingi pengine nitaendelea kuziweka katika vipande vingine vya ziada. Na vifo vya watu wa namna hii huwa kila mtu anaongea lake.
Kwahiyo nimekupa hii ili ujue kwamba si kila mtu anaekufa ni kwamba amekufa kwaajiri ya kwenda kutimiza hatima ya mtu mwingine isipokua wengine hufa kwasababu moja wapo kati ya hizo nne zingine ambazo nimekuelezea kwa ufupi sana hapo juu.
Na katika ulimwengu wa kiroho nilikwambia kwamba wale wenye hatima hasi na wale wenye hatima chanya wote wananafasi ya uhuisho wa roho zao wakati watakapo maliza hatima walizotumwa kuzitimiza hapa duniani, isipokua ni upande tu ndio tunagawana kuna wale ambao ni magugu na wale ambao ni ngano.
Na katika hizo hizo ngano huwa kuna ngano ambazo mbegu zake ni bora sana na kuna zile ambazo mbegu zake ni dhaifu lakini pia zipo zile ambazo zimetoa mbegu zilizooza, sasa wakati unafurahia wewe kuwa ngano ni lazima ufikirie pia kwamba wewe ni ngano ya aina gani kati ya zile zenye mbegu bora, au zile zenye mbegu dhaifu na zile zilizo na mbegu zilizooza.
Na kwenye maisha ya hapa duniani hautakiwi kuhukumu na inawezekana ulikua unahukumu kwakua ulikua haujui mambo haya ila naamini sasa umepata kuyajua kwamba kutokana na utofauti wa hatima tulizo beba ndio hupelekea mambo yawe hivi, kwamba wakati wewe unamuona mwenzio anadhambi kufanya vitendo vya namna fulani fulani ila wakati huo huo mwenzio yeye kwa kupitia vitendo hivyo afanyavyo katika ulimwengu wake yeye anaonekana ni shujaa kama vile Sauli alivyokua anawaua watumishi wa Mungu nyakati zile.
Pia lazima ujiulize kwanini Sauli licha ya kuwa na dhambi ya giza ila Mungu alimsamehe na kumuacha amtumikie? Jibu ni kwamba Sauli hakuwa na makosa kwasababu yeye alichokua anakifanya ni kutimiza ile hatima iliyokuwa ndani yake kwa wakati ule, ila baada ya kutiwa upofu wa ile hatima mbaya ambayo alikua anaelekea kuitimiza na kufunguliwa macho ya kuona hatima impasayo kwenda kuitimiza aliifuata njia yake kwa nguvu zile zile na hari ile ile ila wakati huu alikua anatimiza hatima ya kiungu iliyofunuliwa ndani yake.
Kwahiyo duniani sio kila mtu ni wa Mungu ila wangine ni mapandikizi ya shetani na kwa kuthibitisha hili embu tuone huu mfano ambao Yesu mwenyewe aliwatolea wanafunzi wake.
MATHAYO 13:24-30
Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake. Lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Baada ya huo mfano twende katika mfano mwingine pale katika ufunuo ili niweze kukufungulia codes vizuri.
UFUNUO WA YOHANA 12:7-10.
Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
Kwahiyo kumbe shetani yaani ibilisi baada ya kushindwa vita kule mbinguni aliweza kutupwa duniani. Sasa hiki kitendo tu cha Ibilisi yaani shetani kutolewa kule mbinguni na kutupwa duniani kina ashiria kwamba dunia haina huruma na wewe na kamwe haitakaa iwe na huruma na wewe, kwa maana hata aliyekuumba hana huruma na wewe isipokua amekuweka hapa kwakua anaimani kubwa na wewe kwasababu wewe ni miongoni mwa wanajeshi wake ambao wamefuzu kwenye yale mafunzo ya kijeshi ya kupigana kwenye vita hii kubwa ya mapambano dhidi ya hatima, chukulia tena mfano huu mdogo, kwamba nchi ambayo inapeleka wanajeshi wake katika uwanja wa vita, unadhani inaweza kumchukua mwanajeshi ambae wana uhakika bado hajafuzu kwenye mafunzo ya kijeshi? Jibu ni hapana bali huwa wanachukua wale wote ambao wanauhakika kwamba wamefuzu kwenye mafunzo ya kijeshi, na wao kama nchi wanakua na imani kubwa na wanajeshi hao, na tumaini lao siku zote ni kwamba wataenda kwenye uwanja wa mapambano na watakaporudi lazima watarudi na ushindi.
Sasa nini kinatokea wakati unapokua umefika katika uwanja wa vita, wale waliokutuma hawatokua na muda na wewe ila watakachokifanya ni kupokea yale maombi ambayo utayaomba kwao kupitia redio call na wao watakachokifanya ni kukutekelezea kwa wakati ili undelee kupambana mwisho wa vita urudi na ushindi kwenye nchi yako, kwahiyo unachotakiwa kufanya ni kupambana na sio kulia lia kwa maana kwenye uwanja wa vita kila mmoja anapambania hatima yake yeye mwenyewe, na ikitokea ukafanikiwa kushinda ukirudi kwenye nchi yako basi utatunukiwa medali ya ushindi na ushujaa na ikitokea ukafia kwenye uwanja wa kivita basi utazikwa na shughuli yako itakua imeishia hapo.
Mfano huo huo wa wanajeshi na nchi, ndivyo ilivyo kwako wewe na yule aliyekuumba yaani Mungu, ukijijua uko hapa duniani ujue umeaminika na matarajio makubwa ya ushindi yapo juu yako, kwahiyo hautakiwi kulia lia kwa maana hakuna atakaekuelewa kwasababu kila mmoja hapa duniani yupo kwenye vita ya kutimiza hatima yake, na machozi yako pia hayatafanya aliyekuumba akuhurumie ila atakachofanya ni kupokea maombi yako ambayo utayapeleka kwake kupitia njia ya kiroho yaani unatakiwa ujiungamanishe na malaika walio katika mfumo nyota wako, na yeye atakutekelezea yale uyaombayo ili uendelee kupambana na mwisho wa siku uweze kurudi na ushindi wa ile hatima kuu ambayo alikuumba ili uje uitekeleze hapa duniani, na baada ya ushindi ndipo utakapo pata kutunukiwa zawadi ya uzima wa milele na ukishindwa kwenye hii vita basi roho yako itazikwa na ile zawadi ya uzima wa milele haitakua juu yako.
Sasa basi tukirudi kwenye hayo maandiko, tunaona baada ya shetani kutupwa hapa duniani ambako ni kama shamba la bwana liliopandwa ngano, na hizo ngano ndio wale wote ambao wamebeba hatima chanya za kimungu ndani yao, lakini sasa shetani ambae ni adui alivyokuja nayeye akaamua kupanda magugu yaani wale watu ambao wako hapa duniani kwaajiri ya kutimiza zile hatima hasi nao walipandwa kwenye shamba lenye mbegu bora ili tu kuweza kuvuruga kwa maana ngano ikiwa bado haijamea ukiichanganya na magugu huwezi kujua ipi ni ngano na ipi ni gugu na ndio maana tukikaa mimi na wewe na yule tukitazamana wote tunaonekana binadamu wa kawaida ila kumbe ndani yetu yapo magugu na magugu ni wale ambao wamebeba hatima hasi yaani hatima za kishetani ndani yao.
Halafu anasema, wale wafanya kazi wakamfuata na wakamuambia tuyatoe magugu na tuache ngano, ila yeye akawaambia wakifanya hivyo watachanganya kwa maana wanaweza kung'oa mche wa ngano wakahisi ni gugu ila alichosema waache tu hadi ngano zitakapo mea ndipo zitapoonesha utofauti na yale magugu na hapo ndipo atakapowaambia wang'oe hayo magugu wayafunge na waende kuyachoma moto.
Wewe ambae umekuja hapa duniani kutimiza hatima ya kimungu unatakiwa kukomaa ili ujitenge na magugu, kwa maana ya kuinyanyua ile nguvu iliyopo ndani yako na pia ushike njia uanze kutimiza ile hatima iliyofanya uumbwe kwani hatima ya zile ngano zilizopandwa kwenye lile shamba ni kuhakikisha zinamea na kutoa ngano, ila zikiishia njiani na zikashindwa kutengeneza ngano basi zitang'olewa pamoja na magugu ili zikachomwe moto, na pia ukumbuke kuna watu aina ya kina Sauli ambao wao wamebeba nguvu zilizo na uwiano, sasa endapo uking'oa miche yao ukadhani kwamba ni magugu wakati wakiwa bado hawajamea basi moja kwa moja utakua umechanganya kwa maana licha ya kwamba ni kina Sauli lakini kadri wanapomea wanauwezo mkubwa wa kubadilika na kuwa kina Paulo.
Sasa ukirudi kwenye lile shamba utagundua kwamba kuna vita kubwa ya hatima ya kumea kwa maana kuna yale magugu ambayo huwa yanatambaa, sasa yakikutana na mche wa ngano ambao ni dhaifu wanautumia kutambaa juu yake ili yaweze kustawi na mche huu utakufa au utamea kwa shida na utashindwa kutengeneza ngano kwahiyo kipindi cha mavuno kikifika nao utang'olewa pamoja na lile gugu lililoutumia kutimiza hatima yake ya kumea zaidi, na hivi ndivyo itakavyo kuwa kwa wewe ambae unakubali kuwa dhaifu ili watu wengine wakutumie kwenye harakati zao za kutimiza hatima.
Kwahiyo ili uweze kushinda hii vita ili kipindi hata roho itakapoacha mwili iweze kwenda kwenye ulimwengu wajuu ni lazima uweze kufikia hatima yako, na ufanikiwe kunyanyua zile nguvu zilizomo ndani yako kwasababu nimeshakwambia usiponyanyua hizi nguvu za asili zilizomo ndani yako hautaweza kufikia hatima kwa maana vita ya hatima iliyopo hapa duniani ni kubwa sana na mara tu utakapogundulika umeanza kuielekea njia ya hatima yako lazima uje kujaribiwa ili wajue umejipanga panga vipi, na kwakua wewe hauna nguvu basi utashindwa kukwepa mitego na hatimae watakurudisha nyuma.
Kwani hata shetani alipoona Yesu anaanza kuielekea ile njia inayoenda kwenye hatima yake basi aliamua kumfuata, kipindi Yesu alipokua kwenye mfungo na akaanza kumjaribu, sasa kwakua Yesu tayari alishafanikiwa kuinyanyua ile nguvu ya asili ambayo ilikua ndani yake huu mtihani wa majaribu yake ibilisi kwake haukua mgumu kwenye namna ya kuuvuka.
Sasa kama Yesu tu alijaribiwa baada ya kuonwa ameanza kuifuata ile njia inayoelekea kwenye lengo kuu la yeye kuletwa hapa duniani, wewe ni nani mpaka ushindwe kujaribiwa? Kuishi maisha ya hatima yako huwa sio rahisi na ndio maana utaona wengi ni masikini hapa duniani ila wachache wanaofanikiwa ni wale wa upande hasi ila wa huku upande chanya bado wanajikongoja lakini mambo yanawezekana endapo tu utaamua kuishi maisha ya kufuata sheria za kiimani hasa ile inayofungamana na wewe kwa maana iliyotumika kunyanyua nguvu yako ya asili.
... Naishia hapa kwa leo ila nitarudi baada ya muda, naacha gape kidogo ili uweze kusoma kwa kutafakari na ujipe muda wa utulivu ujenge maswali kwaajiri ya kuuliza.