Dunia ni uwanja wa vita za hatima

Thecoder kwa hiyo ukienda labda kwenye interview ya kazi ambayo siyo hatma yako na ukiwa umejiandaa sana kwa kusoma, kusali na kufunga pamoja na kuelewa mkono na watumishi ni rahisi kupigiwa chini na mtu ambaye hajajiandaa, hajasoma, hajasali, hajafunga na hana mkono wa mtumishi, ila kinachokushinda no kwamba eneo ni la hatma yake sio yako japo wewe umeinua nguvu za rohoni, kwa nini inakua hivyo?
 
Inakua hivyo kwasababu ya hatima.

Hili swali nimelijibu mara nyingi kwamba kinachoombewa si pesa ila ni njia za pesa ambazo zipo ndani ya kila mtu kupitia hatima yake.

Pia nataka ujue ya kwamba duniani si kila jambo huwa linaombewa na mambo yote ambayo yapo ndani ya mtu tangu alipozaliwa huwa hayavutwi kwa maombi ila yanavutwa kwa kuyaendea kwenye njia zake but mambo ambayo huwa yanaombewa ni yale mambo ambayo hayakuwa ndani ya mtu tangu alipozaliwa kwamfano ukiwekewa unajisi ni rahisi sana kutoka kwa njia hizo za maombi.

Skia, ukienda dukani ukawa umenunua shati au tishet nyeupe then ukaivaa ila ikatokea wakati uko kwenye mitikasi yako madoa yakiingia utaenda kununua dawa ya madoa na utayatoa hayo madoa, na kinachotokea ni kwamba hiyo dawa ya madoa itadeal na madoa tu na wala si vitu vingine ambavyo vilikuja na hiyo nguo kutoka kiwandani na hivi ndivyo maombi yanavyofanya kazi.

Kwahiyo unapoombewa kwenye kazi ambayo si ya hatima yako huwa kinachotoea ni kuoverride kwa maana unaongeza baraka kwenye kazi ya hatima ila si kwenye kazi ambayo si ya hatima yako thou kuna baadhi ya sababu za hapa na pale zinaweza kupelekea ukapata hiyo kazi ila si kwasababu ya hayo maombi.

Kubadili asili ya kitu kilichopo ndani ya mtu au ulimwengu na kufanya kifanye kazi kwa namna tofauti hapa huwa tunasema muujiza umetokea au mtu ameamua kufosi hatima ambayo si yake.

Muujiza si kila mtu anaweza kuufanya na Kubadili hatima kuna utaratibu wake na kuihodhi haiwezekani bila kafara.
 
Ngoja niwasaidie ambao wameshindwa kukipata kule telegram
 

Attachments

Mzee umetisha yaani unavyo tirilika nikama vile unanijua aiseee 🤔

This 👇👇 unaweza Vipi kuziepuka Roho hizi !? Au ndio hatima yako so haiepukiki!?
 

Attachments

  • Screenshot_2024-12-20-09-08-31-566_com.quoord.jamiiforums.activity-edit.jpg
    256.3 KB · Views: 11
Ulimwengu wa Roho wa Nuru ndio unaongoza ulimwengu wa mwili.

Hatma yako ili uifikie lazima ushinde vita na vita hiyo ni ya Rohoni ni vita kati ya ulimwengu wa Giza na Nuru, na ukishinda utaiona hatma ila ukishindwa hutaona hatma yako.

Kazi kwako kuchagua ulimwengu wa Giza au Nuru ili uifikie hatma yako...

NB: Dunia hujaja kucheza ni uwanja wa vita ila isiyoonekana.
 
Ulimwengu wa Roho wa Nuru ndio unaongoza ulimwengu wa mwili.
sio watu wote wanaishi kwa uadilifu kwa maana kuuruhusu ule ulimwengu wa kiroho uweze kuuongoza mwili na hata wale ambao waliwahi kufanikiwa hawakuwahi kuishi upande huo kwa asilimia 100 bali walio wengi wanahama na ndio asili ya kila mwanadamu na hili unaweza kuliona hata kwenye manabii na mitume ambao waliaminiwa sana kuishi kwa uadilifu kilichokuja kuwaangusha wengi wao ni kushindwa kuuacha mwili uendelee kuongozwa na roho na badala yake kuna nyakati waliuacha mwili uiongoze roho na ndio maana mwanadamu ni kiumbe ambae haaminiki kwa maana huwa anaswitch kwa haraka sana kwa sababu asili ya ulimwengu inafavor sana upande wa mwili kuliko ule wa kiroho...na huu ndio ugomvi mkubwa kati ya mamlaka za juu na mwanadamu.
 
Imani na Toba ya kweli yaani msamaha pekee ndio unafanya Manabii na wanaomuamini Mungu waweze kuendelea kuishi kiroho na kimwili.

Pia kufunga chakula ni njia nzuri ya kujiweka kiroho zaidi.

Ukiwa kiroho zaidi unakuwa na taarifa za mambo yajayo yaani kama Kuna kazi au adui anakujia unapata taarifa..
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...


Cc: Mahondaw
ni asili, kwa maana mtu ni copy ya ukuu halisi kama ilivyo wewe na mwanao, utaweza kumpa maagizo na kuyafuata pale ambapo atakua kwenye ule umri wa kutokujua lipi jema na lipi baya pamoja na kutokuyamaster vizuri mazingira ila akishafikia umri fulani neno lako kwake haliwi na uzito ule wa kama mwanzo na hata yale mambo mengi ambayo ulikua unamkataza asiyafanye atayafanya... kwahiyo utaona hapo kwamba mwanzo alikua anafuata order zako ila anapojitambua anafuata za kwake mwenyewe na kurudi kwako kila anapokwama.
 
upo sahihi, na hiyo ndio nguvu ya kuishi maisha ya rohoni... kuishi maisha ya rohoni ni kuishi maisha asili ya uumbaji wa ulimwengu, kwa maana hautendi jambo lolote kwa akili za mazoea bali kwa akili halisi ambazo ndizo zilizokuwa sababu ya mtu kuumbwa.
 
Mpaka sasa naamini mimi naishi na roho ambayo iliwahi kuwepo

mimi ni kijana naweza sema ni GEN Z lakini kila nikiwa napiga story na vijana wezangu nahisi kabisa kuna generation gap between me and them

Lakini nikiwa naongea na wazee au watu walionizidi umri wanakuwa wakiniona kama ni genius na muelewa sana pia upendwa na wazee kiufupi ni kwamba.

The more I talk to people of my age I realise I have a generational gap with my own generation

Vipi kuhusu hili mtaalam.

Maana mimi ni moja kati ya vijana ambao napenda sana kufuga ingawa naishi mjini lakini napenda wanyama na nature kwa ujumla mpaka sasa niliona kama maisha yangu yanafaa kuwepo kijijini

Lakini kila nikikaa na vijana wenzangu nikawaambia kuhusu maswala ya nature ufugaji na kadhalika huwa wananiona kama nina akili nyingi lakini mi kama na data




Thecoder
Thecoder
Thecoder
 
Thecoder uko wapi kwani.....
 
Jitafutie muda wa kukaa mwenyewe katika utulivu wa akili kuna vitu vingi sana utavuvuta ndani yako na huo uwezo ambao wanauona uko nao sasa utaongezeka zaidi.

Kati ya dalili moja wapo ya kugundua kama ulishawahi kuwepo hapa au laa ni hiyo ya kuwa na machaguo ya rika kwamba wewe mwenyewe tu ukikaa na watu wa rika lako unaona kama si watu sahihi ila ukikaa na watu wenye umri mkubwa kuliko wewe unajiona unafurahia sana maongezi lakini pia ukikaa na watu wa rika lako wanakuona kama uko na ukale fulani ambao hauendani na wao so automatic wanakua hawavutiwi sana na wewe.

Jitahidi ufuge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…