Dunia ni uwanja wa vita za hatima

Dunia ni uwanja wa vita za hatima

nakushauri sana unyanyue nguvu chanya ili uweze kuishi kwa kufuata sheria za ulimwengu kwani utafanikiwa zaidi.
Ushauri ni mzuri lakini hujasema mazee ni sheria za ulimwengu upi kwani umesema kuna ulimwengu wa nuru na giza. Tafadhali fafanua zaidi ili tuweze kuelewa
 
Thecoder katika jibu lako hili nimepata swali lingine ni kuhusu "mafuriko ya baraka katika mto wa hatima"ambapo watu kupata bahati za kifedha hata pasipotarajia japo si wengi wanatambua hili maana wengi wetu tukio hili la kufurika neema kwenye mto wa baraka wa hatima linapita tu pasipokutambua tunaona tumepata zali tu pasipo kujua kama ndio hatima hiyo..sasa swali ni je,ukiwa umejua mto wa hatima umefurika sasa utumie vp nafasi hiyo kutengeneza fedha.? swali la pili je, hiyo kufurika mto hatima inatokea kila baada ya mda gani je,kuna saa katika masaa 24 au mara moja kwa mwezi je kuna tarehe rasmi? au ni mara moja kwa mwaka ni mwezi upi? na inadumu siku ngapi huko kujaa mto wa hatima.? maswali yote haya ni kujiweka tayari kwamba mafuriko yajayo hayakupiti lazima uwin maswala ya kifedha.! au hayo mafuriko ya kujaa mito ya hatima yako ndio ya kubahatisha tu na kuhisi pasipo kalenda rasmi.?
Maswali mazuri ila nadhani umefuatilia vizuri hili andiko na kama ndivyo basi kuna sehemu nimeelezea hapo juu japo kwa uchache.

Lakini iko hivi, mafuriko ya mto wa baraka ambao uko kwenye ile njia inayoelekea kwenye hatima yako huwa hayana muda maalumu kutokea na hii hutegemeana sana na maombi ambayo mtu huyafanya au wazazi au ndugu wanamfanyia mtu huyu ili aweze kufanikiwa katika upande huo wa mambo ya kifedha na kwakua mtu huyu anafanya mambo yaliyokinyume na yale ya kwenye hatima yake basi anajikuta anapishana na hizi baraka na accumulation inaenda kutokea hadi kupelekea hizo kingo za huo mto kupasuka.

Kwahiyo kwa makadirio ya kawaida huwa ni kwa mwaka mara moja kila mtu huwa anakutana na hizi nyakati ila kwa wale ambao huwa wanafanya sana maombi ya umiliki huwa hizi nyakati zinaweza kuwatokea mara kwa mara na muda ambao hiki kipindi kinadumu huwa inategemea na ukubwa wa hayo mafuriko yenyewe ila inaweza ikakaa mwezi au miezi kadhaa.

Na pia nilikwambia kipindi hiki ndio kipindi ambacho mtu anauwezo wa kukutana na watu wa hatima yake, kwamba unaweza ukakutana na mtu ambae hamkuwa mnafahamiana hapo awali ila baada ya kukutana nae ukashangaa ile connection yenu ikawa na utofauti na ghafla ukashangaa anakusaidia kutatua shida zako za kiuchumi na hapa ndio utakuta kama wewe hatima yako ni kuajiriwa basi utaona anakupatia kazi au kama hatima yako ni kuhusu kuanzisha cha kwako basi utaona anakusaidia kuanzisha hiyo biashara na kadhalika.

Ukakutana na watu wa namna hiyo basi kaa ukijua kwamba majira ya mafuriko yamewadia Kwahiyo unatakiwa uitumie hiyo nafasi kwa unyenyekevu mkubwa kwa maana huwa hazidumu.

Na nikuibie tu siri ni kwamba watu wa hatima yako mara nyingi huwa wanaangukia kwenye wish yako, hapa na maanisha kwamba kama ni mdada anaweza akawa anawaza akutane na mbaba mtu mzima ambae ako na ukwasi wa kutosha ili aweze kumvusha katika nyakati nguvu za kiuchumi anazopitia na baada ya muda katika majira fulani utaona hii wish yako inakua kweli na pia upande wa vijana huwa mnatamanigi mkutane na wamama wenye ukwasi ili wawasaidie kuwavusha kwenye kipindi cha majira fulani na baada ya muda utaona kweli wish yako inatimia ila sasa walio wengi huwa wanajisahau na wanadhani hivi vipindi ni vya kudumu kumbe kiuhalisia si kweli ila huwa vinadumu kwa nyakati fulani na utapewa sana pesa na baada ya muda utaona kuna sintofahamu inatokea hapo katikati mnakwaluzana na mambo yanarudi katika hali yake ya kawaida.

NB: hiyo mifano ya wish niliyotumia hapo juu ni kutokana na muktadha Kwahiyo nimeona ni mifano rahisi ambayo inaweza kueleweka kwa urahisi ila wish za watu huwa ziko tofauti tofauti na wish hizo huwa zinatimia katika majira hayo ya mafuriko na pia unatakiwa ufahamu kwamba kama wish yako ni ile ya kuendelea kuongeza mitetemo chanya basi ikitokea katika haya majira huwa inakua hivyo siku zako zote za hapa duniani kwa maana ya kwamba hakuna mkwaluzano utakao tokea ambao utafanya huo muunganiko kupotea.

Usiache kufanya maombi ya umiliki wa fedha na Mali hata kama bado hujaiona ile njia inayoelekea kwenye hatima yako ili uweze kuwa na majira ya namna hii mara kwa mara.
 
Ushauri ni mzuri lakini hujasema mazee ni sheria za ulimwengu upi kwani umesema kuna ulimwengu wa nuru na giza. Tafadhali fafanua zaidi ili tuweze kuelewa
Sheria za ulimwengu huu kwa maana ukiishi kwa kufuata Sheria utaendelea kusaidia kuongeza ile mitetemo chanya ambayo hii husaidia kuifanya dunia iendelee kuwa sehemu salama ya kuishi na kwakufanya hivi basi hii itasaidia zile nguvu zako za asili ambazo umeshazinyanyua ziendelee kuwa kwenye afya njema.
 
Halafu je ni nyota inaamua wewe uishi vipi hata kama hutaki.na je kwa mfano wewe ni nyota ya punda na huridhiswi nayo je unaweza kujubadilisha na kuwa na nyota ya Mapacha
 
vipi ina maana gani kuwa na kiganja chenye alama M mKONONI.Nasikia wenye M hawarogeki je ni kweli
Hii ni topic nyingine ndefu ila kiufupi ni kwamba kiganja cha mwanadamu huwa kina alama nyingi sana na ndizo ambazo tunatumia kuangalia completeness na incompleteness ya mtu na mtu katika ile mitetemo ya mfumo nyota sasa katika hili watu wengi wenye alama M huwa wanaangukia kwenye lile kundi la watu walio complete ingawa sio kila M inaweza ikawa kwenye kundi hili.

Sasa kwenye kurogeka au kutokurogeka huwa kunategemeana sana na nguvu za asili zilizo ndani ya mtu kwamba ziko juu kwa kiasi gani bila hivyo ni utarogeka kama kawaida bila kujali alama iliyo katika kiganja chako.

Hizi alama za kiganjani huwa zinatumika sana kuangalia nani ni donor na nani ni receiver katika mahusiano baina ya wapenzi wanaotaka kwenda kwenye hatua ya kufanya agano la ndoa.
 
Halafu je ni nyota inaamua wewe uishi vipi hata kama hutaki.na je kwa mfano wewe ni nyota ya punda na huridhiswi nayo je unaweza kujubadilisha na kuwa na nyota ya Mapacha
Nyota iko kwenye asili halisi ya mtu kwahiyo unavyoishi ndivyo asili yako ilivyo mara nyingi na mfano niliusema kwenye kipengele cha maisha kwamba kuridhika au kutokuridhika kwa mtu katika vile viwango vya umiliki kunatokana na ukubwa wa hatima ya mtu husika.

Huwezi kubadili mfumo nyota ila unauwezo wa kumnyang'anya mtu mwingine na kutumia ule mfumo nyota wa asili yake na ndio hapa nilisema kwamba wale wanaotaka kufoji hatima huwa wanatumia njia Hii mara nyingi na nikasema huwa kuna watu wanatumika kutimiza hatima za watu.
 
Hii ni topic nyingine ndefu ila kiufupi ni kwamba kiganja cha mwanadamu huwa kina alama nyingi sana na ndizo ambazo tunatumia kuangalia completeness na incompleteness ya mtu na mtu katika ile mitetemo ya mfumo nyota sasa katika hili watu wengi wenye alama M huwa wanaangukia kwenye lile kundi la watu walio complete ingawa sio kila M inaweza ikawa kwenye kundi hili.

Sasa kwenye kurogeka au kutokurogeka huwa kunategemeana sana na nguvu za asili zilizo ndani ya mtu kwamba ziko juu kwa kiasi gani bila hivyo ni utarogeka kama kawaida bila kujali alama iliyo katika kiganja chako.

Hizi alama za kiganjani huwa zinatumika sana kuangalia nani ni donor na nani ni receiver katika mahusiano baina ya wapenzi wanaotaka kwenda kwenye hatua ya kufanya agano la ndoa.
mkuu Thecoder hapo uliposema alama za kiganjani zinatumika sana kuangalia nani donor au receiver kwa wapenzi waolekea kwenye ndoa..ebu tueleze kidogo kvp yaani..mfano mtu ana mpenzi wake anampango wa kumuoa kwamba anaweza kuangalia kiganja chake na akajua kama hawaendani kindoa.? je,ni alama gani inatizamwa hapo na iwe imekaa vp ili kujua kuhusu mpenzio yaani ukiona alama fulani basi huyo ni donor na alama hii reveiver hata kwa kujitazama kiganja changu..na faida za donor na receiver ni zipi ndani ya ndoa na vp ikiwa wanandoa wote ni receiver au wote wawili ni donor wanakuwa vp hawa wakifanana kila kitu.?
 
KIPANDE CHA TATU CHA NYONGEZA.

Nadhani hadi sasa wote tunajua kwamba Kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na swala la mafanikio ya kibiashara huwa yanategemea zaidi asili yako na ninaposema asili nadhani kwa sasa wote tunaelewana kwamba nazungumzia lile jambo la msingi ambalo lilizaliwa ile siku ambayo wewe umezaliwa kwa maana ya hatima au uelekeo ongozi ambao wewe unatakiwa uufuate ili uweze kutimiza lile lengo la wewe kuwa hapa duniani.

Sasa kutokana na kwamba biashara huwa inamtindo wa kuchagua watu basi kuwa na uhakika hata hawa mentors ambao huwafunza watu mambo mbalimbali ya kibiashara kwenye mazingatio ya ule upande ambao wao wamefanikiwa nao huwa hawafanikiwi kuwafanya watu wote wanaoenda kwenye madarasa yao wafanikiwe kwenye hizo biashara ambazo wao huzitumia kuwaelekeza na kuwasimamia watu wengine waweze kufanikiwa.

Kwahiyo kuna watu ambao wameshawahi kutoa pesa nyingi sana kuwalipa mentors ili waweze kuwasaidia kuwapa mbinu za kuitoa idea yaani wazo lao la kibiashara hadi kwenda kwenye ile hatua ya biashara kisha kuitoa hiyo biashara kuipeleka kwenye hatua ya biashara inayoleta faida itarajiwayo au zaidi, lakini badala yake wanaishia kupata hasara licha ya kufuata hatua zote na mbinu zote ambazo wamekua wakifundishwa na hao mentors wao.

Sasa basi...

Kama utakua umenisoma vizuri kuanzia mwanzo utaelewa ya kwamba hapa mentor hana kosa ila ni vile tu hajui kwamba biashara ni kama dunia ambayo iko ndani ya dunia kwahiyo iko na sheria zake pamoja na taratibu ambazo mtu ni lazima azifuate ili aweze kuishi na sio tu kuishi bali kuishi na kudumu katika dunia hiyo ya kibiashara.

Yaani ni...

Kwamba biashara ambayo imempa utajiri yeye haiwezi kumpa utajiri huo kila mtu ambae yuko hapa duniani, ndio maana mentors wengi huwa wanakuaga na watu wao kadhaa ambao wanapenda sana kuwatolea mfano kwamba waliwafuata wakiwa hawana kitu ila baada ya kusoma na kutumia mbinu zao watu hao waliweza kufanikiwa sana kibiashara lakini pia ukifuatilia kwa mentors hao hao utakuta kuna wimbi la watu wengi ambao wanawalalamikia kwamba ni matapeli kwa maana wamewalipa pesa nyingi ila wameshindwa kuwapatia yale mafanikio ambayo waliwaahidi kuwapatia kabla ya hayo mafunzo.

Sasa yote haya yanatokana na hatima tulizobeba ndani yetu ndizo zinazoleta huu utofauti wa nani afanikiwe kwenye biashara ipi na nani asifanikiwe na kwa maana hiyo basi kabla hujatafuta mentor hakikisha unajijua kwanza na hii itakusaidia sana kuepukana na hali ya kulaumu watu au kuwaona watu ni matapeli wakati wako kwenye hiko wanachokifanya kwa miaka na wamesaidia watu kufanikiwa katika njia hizo hizo ambazo wewe hazikuweza kukufanikisha.

Nimekua nikisema mara nyingi ila nasisitiza tena kwamba kila mtu anaouwezo wa kuanzisha biashara ila si kila biashara inayoanzishwa na mtu inaouwezo wa kuleta faida mikononi mwa kila mtu ambae ameianzisha.

Na ndio maana siku hizi...

Kuna wimbi la watu wengi ambao wamebobea kwenye maswala haya ya biashara na uchumi na wengi wamekua wakitoa ushauri wa namna tofauti tofauti za kuanzisha na kukuza biashara kuanzia hatua za awali hadi kufikia ile hatua ya ukomavu yaani hatua ambayo biashara inaanza kuleta faida na mbinu hizi huwa hazitofautiani sana kati ya mchumi mmoja na mwingine na huwa zinazoleta bure kabisa kwenye mitandao ya kijamii ila licha ya haya yote bado watu ambao wanawafuatilia watu hawa wanapata tabu sana kwenye maswala haya ya kibiashara, wanatumia kila mbinu inayofundishwa na kufuata hatua zote ila bado mambo ni magumu sana.

Sasa ukichunguza kwa umakini hizi shida na taabu watu wanazozipitia kwenye mambo haya ya kibiashara na katika watu hawa ambao wanapitia hizi shida pia wapo walimu au wakufunzi wanaofundisha watu maswala haya haya ya biashara ila nawao pia wanashindwa kuziendesha biashara zao na kuzifanya ziweze kufikia katika ile hatua ya kuleta faida inayotarajiwa au zaidi. Na hii inaashiria kwamba kuna kitu fulani cha msingi sana huwa kinakosekana kwenye vitabu vingi vya mambo ya biashara (ni kama vitabu vingi vimeruka kurasa yaani zile kurasa za awali zilinyofolewa na kujikuta tunaanzia katikati katika kujifunza mambo haya).

Najua watu ambao tayari mmefanikiwa kibiashara hamuwezi kuelewa hili lakini pia najua nyingi wenyewe licha ya kwamba mmefanikiwa ila huwa hamna maelezo toshelezi ya Kwanini mmefanikiwa katika biashara hizo mnazozifanya na ndio maana kila mara tukiwauliza huwa mnaishia kutupatia majibu yale yale kama tusikate tamaa, kujituma, kuheshinu watu na kadhalika na kusema ule ukweli haya majibu huwa ni mepesi sana kiasi ambacho watu wengi tumeshayazoea na ndio maana wapo watu ambao wanaamini kwamba utajiri ni siri.

Sasa inawezekana mawazo yao yakawa sahihi kwamba utajiri ni siri ila duniani tuko na matajiri kadhaa na ukifuatilia kwenye ile orodha ya matajiri wa dunia halafu ukirudi kwenye ndugu zao wa damu, kwa asilimia kubwa ndugu hao hautawaona hata kwenye orodha ya matajiri 1000 wa dunia, sasa tuseme ni kweli utajiri ni siri ila inamaana matajiri hawa wanafanya siri hadi kwa ndugu zao wa damu? Inamaana hata kuwafunulia kidogo ili na wao wapate hata ule upukupuku wa mwisho mwisho wanashindwa? Hii ukiifikiria ni kama haiingii akilini hivi na inatia mashaka kidogo kuamini kwamba utajiri ni siri ambayo watu wameificha ili wengine wasiijue.

Kwa maana kama nilivyosema hapo awali kwamba ukiwauliza matajiri wenyewe wamefanya fanyaje hadi kufika kwenye hayo maisha ya kitajiri waliyopo au wanayoishi huwa siku zote wanakuambia mambo yale yale, yaani kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu watu, kutokukata tamaa na mara chache utawasikia wengine wanaongeza na neno bahati.

Sasa basi, kwakua matajiri wengi wakiulizwa swali hilo moja, huwa wanakua na majibu yale yale mfanano, ambayo siku hizi masikioni mwa watu wengi huwa wanayaona kama ni majibu mepesi mepesi yasiyo na ukweli wowote, kwasababu hivyo vyote vilivyosemwa na hao matajiri hata wao wanavifanya kila siku wanapokua kwenye shughuli zao za kuwaingizia kipato, ila cha ajabu ni kwamba hawakui kiuchumi, lakini ukirudi kwenye huo mfanano wa majibu, tunaona matajiri wachache ambao wao huwa wanaongezea neno la ziada ambalo ni bahati, na hapa ndipo ambapo siri ya utajiri ilipo, kwa maana hawa waliotutajia hili neno la bahati ni kama wametuibia siri kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Kwa maana kama utakua umenifuatilia vizuri kwenye huu uzi kuanzia mwanzo nilikwambia kuhusu maswala ya hatima kwamba nguvu ya umiliki wa fedha na Mali huwa imejificha kwenye huo upande na nikasema tena kwamba kuliko na hatima yako ndiko kuliko na bahati yako na ndio maana siku zote watu au matajiri wachache husema utajiri ni bahati.

…. Nitarudi tena baadae kidogo kuleta muendelezo wa uzi mama, ila kwenye hiki kipande nimerudia rudia maneno kuweka msisitizo na lengo langu usitoke nje ya haya kwa maana tumeongea mambo mengi na yapo mengi ya kuongea na kuna kitabu kinaitwa vipawa vya hatima unaweza kukitafuta ili uendelee nacho, ni kitabu kidogo na HAKIUZWI.

Lakini pia ipo programme ya VIPAWA VYA HATIMA ikiwa na lengo la kukusaidia wewe kuweza kuijua asili yako na baada ya kuijua hiyo asili yako pia utaweza kujua zile biashara zote ambazo zinafungamana na upande huo, hii programme ni bure kabisa na itakua bure milele so usije ukadhani ni bure kwa sasa ila huko mbele itakua na malipo, HAPANA haitakuwa na malipo milele. Na ukomo wa programme hii yaani kuanzia ule muda wa kuanza kwake hadi kuisha huwa inategemea sana na muhusika kwa maana kadri ambavyo atatoa ushirikiano kwenye kufuata zile taratibu ambazo tutamuelekeza ndivo ambavyo atawahi kupata lile file lake la yeye ni nani na ameletwa hapa kuongeza mitetemo chanya katika upande upi na zipi ni biashara ambazo zinafungamana na yeye moja kwa moja, kwahiyo inaweza ikachukua wiki, mwezi, miezi hadi mwaka.

Kwahiyo kama utahitaji kujiunga na programme hii basi unaweza ukaja PM au ukatuma ujumbe kwenye hii barua pepe vipawavyahatima@gmail.com na moja kwa moja utafanyiwa ule mchakato wa awali ili kwenda kwenye hatua ya kwanza.(HII NI PROGRAMME YA LAZIMA NDIO MAANA NI BURE)

Ila pia ipo programme ya TABSTIP hii ni programme ambayo inachukua ile idea au wazo lako la kibiashara kwenda kwenye biashara na kuitoa hiyo biashara kwenda moja kwa moja kwenye biashara inayoleta faida inayotarajiwa au zaidi. Sasa programme hii inachukua watu ambao wameshapata basic knowledge ya kujitambua Kwanini wako hapa na hatima yao ni ipi na hii knowledge hupatikana katika ile programme mama ya VIPAWA VYA HATIMA kwa maana kuna watu baada ya kuijua hatima yao na zile biashara fungani wanataka waweze kupata ule muongozo wa namna ya kulichukua wazo kulipeleka hadi kwenye biashara iliyokomaa na haya yote hufanyika kwenye TABSTIP na programme hii kuanza hadi kuisha kwake ni miaka 3 ikiwa imegawanyika katika session kuu mbili na kila session huchukua mwaka mmoja na nusu huku zote zikiwa zimegawanyika katika hatua kuu sita na kila hatua itatumika kwenye kufanya transformation yaani mabadiliko ya biashara yako, na hii ndio programme pekee ambayo huwa inahusisha mchango kidogo kwa kila anaetaka kwenda nayo.(HII SIO PROGRAMME YA LAZIMA NDIO MAANA KUNA ADA)
 
hilo darasa la vipawa bya hatima baada ya kuja PM au kwenye E-mail..ni kukaa darasani au kila aliyejiunga anatumiwa andiko PM au kwa E-mail..hukufafanua vizuri kimaelezo hilo darasa la vipawa vya hatima si wote wana muda na nafasi kuwekana kitako class..
 
hilo darasa la vipawa bya hatima baada ya kuja PM au kwenye E-mail..ni kukaa darasani au kila aliyejiunga anatumiwa andiko PM au kwa E-mail..hukufafanua vizuri kimaelezo hilo darasa la vipawa vya hatima si wote wana muda na nafasi kuwekana kitako class..
Tumezingatia hili ndio maana darasa hili tumeliweka liwe la online... by the way niko naangalia namna nzuri ya kufanya ili iwe rahisi kwa kila mtu kushiriki bila kuathiri muda wa kufanya mambo mengine.
 
Back
Top Bottom