DUNIA: Pande mbili tofauti sana. Mtaji unayotaka kuanzisha biashara, kuna mtu mwingine anautumia kwa anasa kwa muda mfupi sana.

DUNIA: Pande mbili tofauti sana. Mtaji unayotaka kuanzisha biashara, kuna mtu mwingine anautumia kwa anasa kwa muda mfupi sana.

Bado natafuta

Senior Member
Joined
Oct 3, 2021
Posts
126
Reaction score
138
Habari wanajamvi, niruhusu niingie moja kwa moja kwenye mada husika. Hata hivyo, nataka kuwashukuru wale wote wanaochangia katika kuleta mawazo ya maendeleo, hata kama wewe ni mfanyabiashara mdogo, lakini ukileta wazo la kujenga, kuna watu wanafaidika zaidi kuliko wewe.


Napenda uzi usiwe mrefu sana. Siku moja katika wiki nilikuwa napita katika maeneo fulani. Nikamsikia mtu akiongea kwa simu kuhusu kuingia kwenye klabu na akasema, "Klabu ile ina burudani sana, nimeipenda sana hahaha. Na hiyo pombe ya thamani ya 600,000 ina ladha ya kipekee sana."


Maneno hayo niliyoyanasa akilini yalinifanya niwaze jinsi ya kupata mtaji. Neno lililonivutia sana ni "pombe ile ya 600,000" ni kweli kabisa.


Hili lilinifanya niulize maswali mengi kuhusu matumizi ya fedha. Kama kuna mtu anayetaka kujua jinsi ya kupata mtaji wa milioni moja, kuna mwingine anayetumia fedha hizo kwa muda mfupi, si kwa uzalishaji bali kwa anasa.


Kuna mwingine anayetamani laki moja kujaribu biashara fulani, mwingine anapoteza hiyo laki kwa masaa machache tu.


Hili jambo limechochea fikra zangu na kunipa motisha ya kutafuta kwa bidii zaidi.


Nilipokuwa nikiendelea na safari yangu kuelekea kwenye maeneo ya mageto, nilibadilisha mwelekeo na kwenda kuchunguza jambo ambalo ningelishughulikia siku iliyofuata.


Dunia ina mambo mengi ya kufikiria.
 
Maishaa ndivyo yalivyo mkuu, kilaa mtu aplay nyimbo anayowezaa kuimbaa na kuichezaa Kwa furahaa😀.ukitaka ucheze nyimbo ya mwenzio na hujaielewaa bac kamwe utaielewaa tu....
FB_IMG_1738352757712.jpg
 
Kuna jamaa aliwahi kunifuata PM akiniambia eti ninamajibu mabaya...😜 na akanifananisha na mzee asie jielewa na ndiomaana eti nina avatar mbaya...🤣
Aiseeee nilicheka sana, nikamjibu tu Asante 😊
Binafsi mimi ni content creator huko YouTube , kitu nimejifunza hata kama unafanya jambo zuri kiasi gani lazima kuwe na mitazamo tofauti, inayokukubali na inayo kupinga, nawote hao ni wafuasi wako inabidi u balance tu.
 
Binafsi mimi ni content creator huko YouTube , kitu nimejifunza hata kama unafanya jambo zuri kiasi gani lazima kuwe na mitazamo tofauti, inayokukubali na inayo kupinga, nawote hao ni wafuasi wako inabidi u balance tu.
Ni kweliii mkuu Kuna watu Wana comment za hovyo sijawahi ona
 
Siku zote maisha ndivyo yalivyo. Na haijawaji kuwa sawa. Ndani ya dunia kuna milima, kuna mabonde, kuna miti, kuna maziwa, kuna bahari, kuna wanyama, nk.

Hata wewe mtoa mada hapo ulipo inawezekana umzima wa afya tele! Isipokuwa tu umenyimwa utajiri. Lakini wakati huo huo unakuta kuna tajiri mkubwa mahali fulani anapambania uhai wake hospitali kwa sababu tu ya ugonjwa fulani usio na tiba.

Hivyo jifunze kumshukuru Mungu kwa yote. Muhimu tu siku zote uukumbuke huu msemo dunia ndivyo ilivyo.
 
Maisha ni Utofauti pia matumizi ya pesa Kila Mtu anatumia kivyake kwa uwezo wake. Mimi ninae Rafiki yangu alimpa Demu kitaani tu amempenda kampa 1.5Milioni... na Kachapa mara 2 akaachana nae anasema, itamsababishi kuachana na mke wake. Maana mke wake ataki yeye aoe mke wa pili.
 
hili bandiko lako nilitamani walione wale wote wenye kupinga ems ingewasaidia kufungua bongo zao.
 
Mkuu ya duniani ni mengi bado hujayaona.. Mimi nilichoka siku naona mtu kaingia Casino hapa Bongo kacheza kamari ya milioni mbili ikapigwa ndani ya nusu saa akaaga akaondoka zake. Si bora hata huyo ameweka heshima bar..
 
Mkuu ya duniani ni mengi bado hujayaona.. Mimi nilichoka siku naona mtu kaingia Casino hapa Bongo kacheza kamari ya milioni mbili ikapigwa ndani ya nusu saa akaaga akaondoka zake. Si bora hata huyo ameweka heshima bar..
Duuuuuh
 
Back
Top Bottom